Wamiliki wengi wa majokofu/friji wanauelewa mdogo juu ya utendaji kazi wake

Ahsante kwa maelezo murua.

Binafsi Friji yangu ina partition 2. Juu na chini. Ila takribani miezi 2 nime baini, partition 1, ya chini haipoozi vitu (matunda, nk). Ila partition ya juu ina fanya kazi kama kawaida.

Bado sija tafuta fundi. Naomba mwanga ktk tatzo hili ndg.
 
Pole sana kwa kadhia ya jokofu lako. Kama jokofu lako lina kipima jotoridi sehemu ya chini. Basi yawezekana hakifanyi kazi ipasavyo au ni kibovu kabisa. Kama jokofu ni la familia pia angalia kipima jotoridi kipo nambari ngapi. Yawezekana kuna mtu kakizungusha na kuweka kipimo cha chini kabisa.
Vilevile yawezekana mzunguko wa gesi si mzuri na sehemu ya chini haipati mzunguko sahihi. Hapo kwenye mzunguko wa gesi kuna sababu anuwai zinazoweza kupelekea hilo tatizo. Ukipata fundi mzuri anaweza kusaidia kujua chanzo cha tatizo.
Ila kabla hujamuita fundi, pia angalia kama mlango wa chini unafunga na kusiliba. Nitakupa kisa kimoja mwishoni.
Kusiliba kwa mlango wengi tunaona ni swala dogo, lakini husababisha ufanisi mkubwa kwenye jokofu lako. Unaweza kupima kwa kuangalia juhudi unayotumia wakati wa kufungua mlango. Wakati jokofu linafanya kazi, fungua mlango halafu ufunge. Jaribu tena mara ya pili kuufungua muda huohuo. Angalia kiwango cha juhudi au nguvu unazotumia wakati wa kuufungua mara ya pili. Kama unatumia nguvu fulani kuufungua, basi mlango uko sawa. Yaani unafunga na kusiliba. Ila kama unaona mlango unafunguka bila juhudi yoyote, basi kuna walakini kwenye mlango. Shughulikia kwanza mlango, hakikisha ukifunga unasiliba na unatumia nguvu kidogo kuufungua. Kama shida itaendelea angalia swala la kipima jotoridi na hatimae tafuta mtaalamu aliyekaribu.
Pia nakushauri pitia uzi huu andino baada ya andiko. Nadhani kuna watu pia wana tatizo kama lako na kuna watu wamejaribu kuwasaidia. Kuna mambo mengi ya kujifunza hata utakapomuita fundi utakuwa na misingi itakayokusaidia kubaini kama fundi huyo atakupa kile unachotarajia. Hata mimi kuna vitu nimejifunza kwenye huu uzi. Ila vitu nilivyojifunza vimenisikitisha zaidi. Nimejifunza kuwa kuna mafundi wanaamini kwenye jokofu kuna kifaa kinachotengeneza ubaridi. Nilichukulia hilo na mengine mengi kama funzo kwangu.

Mlango
Nilisema nitakupa kisa cha mlango mwishoni. Basi bwana, ni kama majuma matatu yamepita. Siku hiyo nipo nyumbani na sikumbuki nilikuwa naangalia nini kwenye jokofu upande wa chini ambako ndiko kwenye ubaridi mkali. Nikakuta vitu havina ubaridi kabisa. Kuuliza nikaambiwa sikuhizi upande wa chini haupozi kabisa. Wakati naufunga ule mlango, nikahisi hali tofauti katika ufungaji wake. Nikaufungua, ukafunguka kama vile uliegeshwa tu. Nikaanza kufuatilia, nikagundua kuna viraba fulani kwenye wigo wa mlango havijakaa vizuri. Inaonekana vilichomoka na kuna mtu akaamuwa kurudishia lakini akapachika mahali tofauti. Matokeo yake vinazuia mlango kusiliba. Nikauliza wote mule ndani wakakana kugusa mlango wa jokofu. Na mule ndani ni mama watoto na msaidizi wetu. Vile viraba vina reli yake, wakati wa kusafisha jokofu kama hauko makini vinaweza kutoka na usijue vimetokea wapi. Basi baada ya muda wa kuwaza na kuwazua, nilifanikiwa kuvipachika vile viraba kwenye reli zake. Nikafunga mlango ukashika na kusiliba. Jokofu likarudia upya wake.
 
Ahsante.

Nime fanya zoezi la mlango ni nime kagua raba za mlango ziko sawa. Na mlango una nata hivi ku ufungua.

Nime angalia kile kidude cha Temp. Control mshale upo kwenye optimal (yaani kati ya Cold na Coldest). Version ni Samsung -Digital Inverter (mpya/siyo used).

Huenda hiyo sababu ya Mzunguko wa Gesi haupo Normal.
 
Baada ya kusoma
Nmeangalia angalia kidogo fridge yangu
Nmejifunza kitu
Pia mwenyewe nna ufundi kidogo hivyo n sawa nakusema nmeongeza kitu
 
Zima yawezekana kuna barafu inazuia airflow kwenye compartment ya fridge yako (kama una non frost fridge) fanya experiment ifuatayo jioni moja zima fridge yako toa kwenye umeme, iache mpaka asubuhu ili kama kuna barafu zote zitoke, then asubuh au machana irudishe kwenye umeme uone je itafanya kazi vizuri? Ikiwa sawa basi ujie shida ni barafu iliziba air flow kwenye compartment.but why barafu? Ni kwasababu ya kuacha milango wasi muda mrefu for no reason then moisture inakua introduced ndani ya fridge na kwenda kwenye evaporator kutengeneza Frost (barafu), then barafu ina restrict airflow.
 
Ahsante

Nitafanya hiyo test mkuu.

Mm nipo Mwanza. Mafundi wa Mwanza, mlete contacts zenu.
 
Duuh basi mie nilikuwa najua yale mabarafu huwa watu wanaweka vitu vikiwa na maji maji kama ni container hufuti n.k. Basi hata nilivyonunua navyoona haina mabarafu nikajua kwa kuwa vitu tunaviweka vikiwa havina majimaji kwa nje mpaka zile container zilizohifadhia vitu. Nakumbuka long time ilikuwa umeme ukikatika unakuta maji yanachuruzuka sakafuni, nadhani hizo frost sidhani kama zipo madukani sasa hivi maana nyingi tunazonunua dukani ni non frost kwa elimu uliyotoa hapa, unless ununue kwa special request kutoka kwa muuzaji
 
mkuu friji langu ni la mtumba,.lina fridge juu na freezer chini, linagandisha fresh, changamoto yake halizimi na kuwaka, yaani ukiliwasha, kitawaka 24 bila hata kuzima, lina mfumo wa frost, na consuption ya umeme wameandika 90w, niliwasha siku nzima nione je lina kula umeme kiasi gani for 24hrs, nikaona ni kama 1.7 unit, je kwa utumiaji huo wa umeme liko sawa?
 
Mi niko na swali moja hivi nataka kujua.

Natakiwa niliche friji kwa muda gan bila kuliwasha ikiwa limetoka kwenye mtikisiko wa usafiri. Labda nikiwa limetoka mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine kwa usafiri wa kirikuu.
 
Mi niko na swali moja hivi nataka kujua.

Natakiwa niliche friji kwa muda gan bila kuliwasha ikiwa limetoka kwenye mtikisiko wa usafiri. Labda nikiwa limetoka mtaa mmoja kwenda mtaa mwingine kwa usafiri wa kirikuu.
Langu lilikua jipya lg niliambiwa masaa 7
 
Asante mkuu kwa elimu hii muruwa kuhusu friji kiukweli tunapigwa sana na hawa wanaojiita "mafundi " unaweza kumwita fundi aje kutengeneza kumbe ndo anaharibu mazima unakuta fridge huwezi kutumia tena.
 
Shukrani kwa somo zuri..nina deep freezer nilinunua mwezi wa tatu ni (jipya kutoka dukani )..toka mwezi wa tatu mwaka huu 22 toka nimelinunua mpaka mwezi wa 11 mwanzoni lilikuwa linafanya kazi vizuri kabisa maana nalitumia kwenye biashara ya barafu na ice cream shida imeanza toka wiki iliyopita ..kiufupi haligandishi tena ila kupoza linapoza na matumizi ya umeme yameongezeka toka tatizo hilo lianze msaada tafadhari
 
Mafundi wanakuja liharibu zaidi
 
Naomba kujua, nataka kuanza kuuza Gesi za friji;
1. Maduka ya kuuza Gesi za friji kwa jumla yanapatikana maeneo gani jijini Dar es Salaam
2. Gesi za aina gani zinazotumika kwenye Friji, AC, na AC za magari na zipi zilizopitwa na wakati (yani R22 au R420 n.k.)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…