Wamulikwe wanaotumiwa kudhoofisha jitihada za Rais Samia Suluhu

Wamulikwe wanaotumiwa kudhoofisha jitihada za Rais Samia Suluhu

Mabibi na mabwana, mama Samia kadhamiria kwa dhati kabisa kutuvusha salama kama taifa.

Hii ni katika masuala yote msingi yakiwamo ya afya zetu na pia katika ujenzi wa taifa.

Kuhusiana na afya zetu hasa gonjwa hili linalotikisa dunia, mama Samia aliteua tume ya wataalamu ambayo tayari imeshatoa ripoti yake. Kilichobakia hapa, sasa ni utekelezaji tu.

Apongezwe sana mama Samia kwenye hili

Lingine la msingi ni ripoti za CAG kuhusiana na TPA na BOT. Hili linagusa moja kwa moja na ulipo mzizi halisi wa matatizo yetu haswa, ya kiuchumi.

Ripoti hizi na hatua husika zitakazofuata kuhusiana na ripoti hizi yatatueweka katika nafasi bora sana.

Hii nchi imekuwa ikichezewa mno kiuchumi katika awamu zote zilizopita. Tuliowaamini na waaminiwa wengi, wamekuwa ni kikwazo kikubwa. Hili bila exception awamu kwa awamu.

Yamekuwa yale ya umdhaniaye siye ndiye!

Pana haja ikibidi ya kutumia nguvu (minimum force) kuwadhibiti baadhi ya wanaoonekana kujitokeza kutaka kumkwamisha mama kwa sababu zao binafsi. Watambue kuwa urais unastahili heshima kama nilivyokuwa ikisisitizwa kwenye awamu ile.

Watu hawa wanaoonekana ni vibaraka wanotumiwa
na watu wasiolitakia mema taifa hili wakiwamo mabeberu. Watu hawa si wa kuvumiliwa hata kidogo.

Litakuwa jambo la msingi sana sote tukamwuunga mkono mama Samia anapodhamiria kulijenga taifa hili kuwa la haki kamili, kwa kutowaonea haya wenzetu wote ambao wanaonyesha kuwa mabingwa wa kukosa uzalendo.

Washindwe na walegee.

Ninawasilisha.
Huo ni uhuru wa kuongea na kutoa michango. Kukwamishwa ni yatokanayo katika kutimiza majukumu yako ya kiuongozi.
 
SSH anajikwamisha mwenyewe, uwezo mdogo wa kufikira, ukurupukaji wa kutoa maamuzi mkubwa, ubinasfi na chuki juu.
Tuna document tu maamuzi yake ili baadaye apate stahili yake.
Mosi, Kuruhusu wawekezaji waje na expatriates as per their desire.

Mbili, amewakatisha tamaa TRA kukusanya kodi, mapato yakipungua yeye ndio chanzo.

Tatu, ameweka 14 days quarantine to all foreigners, hii ina direct impact kwa utalii na biashara, ndani ya miezi 6 tu tutaona madhara.

Nne, amerudisha Ikulu Dsm, ina maana fedha yote iliyotumika kujenga Dodoma imepotea.

Tano, amekuwa modern Chief Mangungo kwa kuuza dhahabu kwa kioo, rejea makubaliono yake Kenya.
Well spoken.
 
We jamaa Ni mnafiki sana unachuki ya ajabu mkabila ,mzandiki na muhafidhina wa kiwango cha Phd.

Mwendazake hutamuona Tena mpk doom day
 
Huu ni ubaguzi wa wazi. Hivi kamanda Sirro na kile kitengo cha cybercrime waliacha kazi yao waliyokuwa wakiifanya kwa juhudi kubwa kipindi cha mwendazake?

Heshimuni taasisi ya urais. Mmeshindwa kutambua hii ni awamu ya sita, hamieni hata Burundi mkaishi huko.
Mbona na wewe unabagua. Nchi imemshinda ova.
 
Mbona na wewe unabagua. Nchi imemshinda ova.

Mimi sibagui hata kidogo kwa kukuitisha kuuweka uzalendo mbele.

Mwendazake kwa watu kupotea, taasisisi kubambikia watu kesi, yale ya kina ole wa Hai, bashite na wenzao, magonjwa hatari na nyungu, nk ni wazi kuwa nchi ilikuwa imemshinda kabisa.

Katu si mama ambaye hapa tulipo, tuko vizuri kwenye Corona na tuna subiri reports za CAG.

Awe kahusika Mpango, Majaliwa au wewe, mwizi ni mwizi tu. Segerea zitawahusu kwa nguvu ile ile aliyokuwa mwendazake kwa watesi wake.
 
Basi utasubiri sana.!
hujui kwamba CCM ni ile ile
 
Basi utasubiri sana.!
hujui kwamba CCM ni ile ile

CCM ya Corona ni vita vya kiuchumi ni hii hii?

CCM ya watu wasiojulikana ni hii hii?

CCM ya dhuluma ni hii hii?

CCM ya kina jiwe ni hii hii?

.........

CCM ya serikali ya kubambikia watu wake kesi ni hii hii?

Yapo mengi mno mkuu.

Aaah wapi?

Hi bagosha!
 
Kwa heri
 
Back
Top Bottom