Uchaguzi 2020 Wana CHADEMA tuwe tayari kwa lolote; Lissu, Mbowe, Nyalandu, Membe na gia za angani ikilazimika zisiwayumbishe tusimame pamoja

Mbowe itakuwa ashakula hela, kaanza kuwatuma vijana wake wachokoze chokoze ili waone reaction ya wanachama
 
Lissu anatosha
 
Pengine wewe ni wale wanaofuarilia mambo ya CDM na kuharibu. Siasa sio msaafu. Mkijifanya legalistic hamtafanikiwa. In fact kuna hekima inayosema: CDM hamjui bado kwamba hamtaiondoa CCM kwa siasa za ustaarabu? Kweli tukiendelea na "ustaarabu" huu Magufuli anaweza kutawala kwa miaka mingine 30. CCM wanafurahia woga wa watanzania na wachache wanaonufaika na CCM watatumia mwanya huu mpaka mwisho wa maisha yao.
 
wakutoka ccm waje kujiunga wakati ambao c wa uchaguzi,wakati wa uchaguzi wajiunge lakini wawe wanachama wa kawaida, chadema wanaviongozi walioiva wasimamishe mtu wao
 
Mkuu hiyo siyo,Membe amalizane na wale wanaomwambia amefutwa.Membe ni CCM pure hana elements za Chadema.Atumie wajumbe wa NEC na mkutano mkuu kumrejesha kwenye chama na kumpa go ahead ya kupambana na Bulldozer. Ndio maana Membe anaamini bado atanogesha mchuano katika Chama chao.
Vile vile Chadema ina Mbowe jemedari mtimkavu.
Lissu ni biashara iliobuma kwa sasa,kwani CCM watamwekea pingamizi lazima.
Nyarandu nae ametokea CCM awe na subira,ni mapema mno kwa sera ya sasa.
 
kiukweli safari hii sintakuwa tayari
 
Kuna mambo mawili ambayo wanasiasa wa upinzani na waliopo madarakani wanafikiri na yanaweza kuwa hasi au chanya,
Kwanza kumchagua mtu kwa kufuata mapenzi na chama husika bila kujua uwezo na ueledi wa unaemchagua ila tu chama kipite,
Pili kuchagua mgombea haijalishi anattokea chama gani ila tu ana sifa stahiki za kumpa kura kulingana na uwezo na weledi wake katika siasa....!
 

Kwa taarifa yako sasa wanaccm ndio waliopandikiza siasa za kikondoo ndani ya cdm. Yale maandamano ya ukuta kama sio Lowassa kutoa ushauri wa kikondoo, leo hii tungekuwa tunaheshimiana. Yaani we leo ndio umejua kuwa ccm haiwezi kutoka madarakani kwa siasa za kistaarabu? Huoni kila siku tunasema humu kushiriki uchaguzi ili kupata wagombea ni kupoteza muda, bali tudai tume huru ya uchaguzi, na kama hakuna tume huru ni uchaguzi. Sio lazima viongozi wote wapatikane kwa njia ya kura.
 
Uko sahihi Mkuu maana hawakawii kupata gizani then baada ya uchaguzi wanarbudi kuunga juhudi na maning' uniko kibao
 
Siamini kwamba ccm ndio wamepandikiza siasa za kikondoo CDM eti kwa njia ya Lowassa. Lowassa alishaondoka siku nyingi, tatizo ni sisi wana CDM kufikiri siasa siku zote lazima ufuate ustaarabu, hayo labda baadhi ya nchi za Ulaya, lakini hata wao kabla ya kufika hapo vumbi ilitimka. CDM tunaogopa hata kubadilisha gia angani je tutaweza kuingila mtaani kudai tume huru?
 

Kabla ya Lowassa na mafuriko yake uliwahi kusikia siasa zinazoitwa za kistaarabu zikisifiwa ndani ya cdm? Lowassa na mitume wake walipokuja cdm m, ndio tulisikia wakisema cdm kisiwe chama cha kiharakati bali kiwe chama cha siasa. Sasa hivi watu wameingia woga, inahitajika viongozi majasiri wa kuinua tena moral ya kutokuwa waoga. Na hili haliwezi kuletwa na mwanaccm yoyote yule. Lisu pekee ndio anaweza hilo.
 
Bila kudai na kupigania tume huru ya uchaguzi, mbinu zote mtakazochukua ni sawa na bure. "Count yourselves as losers".
 
Good.
 
Bila kudai na kupigania tume huru ya uchaguzi, mbinu zote mtakazochukua ni sawa na bure. "Count yourselves as losers".
Hakuna atakayetupatia tume huru ya uchaguzi. Naamini tume hiyo haitapatikana kwa ustaarabu bali kwa mapigano, hata CDM wakiingia madarakani hawataweka tume huru.
 

Kila unachosema hapa ni completely opposite from the reality. CCM 2015 ilikuwa imekufa ila Magufuli kafufua chama, na kasi aliyokuwa nayo chama sasa ni imara ila wabaya wake wengi wapo ndani ya chama kwani ule ulaji, madili hamna tena! Ubinafsi
ulizika vyama vya upinzani November 2015 na hatutegemei uhai kurudi tena upinza. Upinzani sasa hauna ‘base’! Yaliyokuwa yanafanywa na Edward Moringe Sokoine na Mwl Nyerere sasa yanatekelezwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…