Wana-CHADEMA waliokula teuzi ndani ya CCM huku UVCCM wakibaki midomo wazi

Wana-CHADEMA waliokula teuzi ndani ya CCM huku UVCCM wakibaki midomo wazi

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Hapa Tanzania kuna watu wamefanya siasa kwa miaka mingi hasa kupitia vyama vya Upinzani.

Kiukweli kufanya siasa za upinzani Tanzania na maeneo mengine kama Afrika sio kazi rahisi
Hata Hivyo pamoja na changamoto hizo bado Vijana wa Upinzani wanaonekana kuwa bora na wanafaa ktk ngazi mbali mbali za uongozi.

Tukumbushane hapa list ya vijana waliokula Teuzi na kula Kuku kwa Mrija baada ya kuhamia ccm na wakaonekana Dhahabu mbele ya Wenzao ndani ya chama na Serikalini pia.

1. Patrobasi Katambi-DC
2. David Kalulila- Kamishina PPP
3.Cecil David Mwambe- Mbunge Ndanda
4. Dr Vicent Mashinji- DC Serengeti
5. Julius Mtatiro- DC Tunduru
6. Peter Lijualikali- DC Nkasi
7. Juliana Shonza- Naibu Waziri Habari
8. Dr Wilbroad Slaa- Balozi Sweden
9.Mwita Waitara- Naibu Waziri

10. Joshua Nasar- DC

Hao ni baadhi tu..mnaweza kuongeza list.

Mwaka 2018 Pekee viongozi takribani 138 kutoka Chadema na CUF waliripotiwa kuhama vyama vyao na kuhamia CCM.
 
Nchi hii ina viongozi wangapi?hao hata asilimia 10 hawafiki ndio unasema wanaonekana dhahabu,kuna wilaya ngapi?kuna mikoa mingapi?kuna wizara ngapi ?ni wachache sana ikibidi waje na wengine .
 
Nchi hii ina viongozi wangapi?hao hata asilimia 10 hawafiki ndio unasema wanaonekana dhahabu,kuna wilaya ngapi?kuna mikoa mingapi?kuna wizara ngapi ?ni wachache sana ikibidi waje na wengine .
Wewe endelea kupost picha za wakubwa utaendelea kuwa vuvuzela wenzako wnaakula Shavu.

Subiri Uone Peter Msigwa anapigwa kitu cha maana.
 
Hapo ni suala la sungura na sizitaki mbichi hizi!
Kwenye modus operandi ya CCM na UVCCM ni kosa kubwa kuongea ukweli na kukosoa.Ukiwa MwanaCCM unachotakiwa ni kusifia tu hata mambo yasiyohitaji Sifa.
Ukijaribu kukosoa na kuelezea mawazo mbadala au kuzungumza fikra zako binafsi tayari unakuwa umejichimbia kaburi Kisiasa.
Kingine kinachoiponza UVCCM ni kwamba bila kuwa na nguvu ya Fedha au connection sahau kupata platform ya kufanyia siasa.
Je usipoonekana ni nani atakayekujua?
Upinzani unapata advantage kwa kuwa wanafanya siasa tofauti na CCM,siasa za kilibelari.Ilihali UVCCM wamekuzwa katika siasa za kihafidhina.
Kusajili wanasiasa kutoka upinzani na kuwapa vyeo kunatoa majibu ya muda mfupi tu.
Suluhisho ni kuifanyia overhaul UVCCM,iwe ni Independent wing ndani ya Chama.Vijana wafikiri kwa Uhuru zaidi,wapewe nafasi ya kushauri,waruhisiwe kukosoa na kutoa mapendekezo Yao kwa Uhuru.
Hii itasaidia Vijana kujitambua na kutambua nafasi Yao ndani ya Chama.
Moja ya jukumu kubwa la UVCCM ni kukilinda Chama na Viongozi wake,Ulinzi ni pamoja na kuhakikisha ustawi wa Chama.
UVCCM ya sasa haijui inachokifanya,haina mikakati.Wapo wapo tu,wanasubiri Mwenyekiti aseme wao watoke kumuunga mkono.Au Mwenyekiti akipigwa spana wao watoke kumtetea!
Kwa staili hii lazima Wapinzani waonekane Wana uwezo mkubwa tu,hata kama uwezo wao ni average!!
Mwisho wa siku Wapinzani watajaa ndani ya CCM,watakuwa na nguvu na hakuna atakayeweza kuwazuia.
Hapo ndipo ule utabiri wa Upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM utakapotimia.
 
Kingine kinachoiponza UVCCM ni kwamba bila kuwa na nguvu ya Fedha au connection sahau kupata platform ya kufanyia siasa.
Je usipoonekana ni nani atakayekujua?
Upinzani unapata advantage kwa kuwa wanafanya siasa tofauti na CCM,siasa za kilibelari.Ilihali UVCCM wamekuzwa katika siasa za kahafidhina.
Perfect
 
Back
Top Bottom