Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
Ndugu zangu Watanzania,
Mbowe ametia sana huruma leo alipokuwa anakamatwa na kupakiwa kwenye Gari la kifahari la polisi .Amejikuta hakuna mwana CHADEMA hata mmoja aliyejitokeza wala kuwa karibu naye kumtetea au kumsaidia kwa lolote lile ,zaidi ya kuona waandishi wa habari wakiongozwa na KIkEKE ndio waliokuwa wakimtetea Mheshimiwa Mbowe .
Mbowe amejikuta amekimbiwa na kuuzwa na vijana wake wote waliokuwa wakimjaza upepo kuwa wataandamana hata ikibidi kufa.lakini cha ajabu leo hakuna aliyetokeza Pua yake ,zaidi ya kuwaona wote wakiwa wamejificha kwa nguvu zote huko Twitter na kuchungulia Mbowe anavyokamatwa peke yake utafikiri anaongoza mkusanyiko wa kondoo.
Mbowe amejuwa na kupata somo kuwa hakuna anayemuunga mkono wala kuunga mkono harakati zake .ametambua nguvu ya ushawishi aliyonayo Rais wetu mpendwa Daktari Mama Samia Suluhu Hasssan katika Nchi hii hususani kwa kundi la vijana. Haijafahamika walikuwa wapi hata wale wanaoitwa walinzi wa mbowe ambao unakuta wamejivimbisha vifua na kununa Utafikiri wanauza na kupima sumu.
Vijana wa CHADEMA wametuma ujumbe kwa vitendo kwa Mbowe kuwa hawaungi mkono habari za maandamano na wala hawapo tayari kuvuruga amani ya Nchi .hii ndio sababu walimtelekeza peke yake na kumuacha apambane na hali yake.ndio sababu alikuta uwanja wa kukutania hakuna wanachama wala vijana wala sare ya chama chake.
Vijana wa CHADEMA pamoja na kukosa kwao umakini na kutokujitambua kwao, lakini kwenye kuvuruga amani wamegoma na kumgomea kabisa mbowe. Wamegoma kwenda kupigwa virungu halafu watelekezwe na chama bila kupewa Msaada wa aina yoyote ile.wanatambua uimara wa askari wetu na ndio maana wamegoma kabisa kwenda kupeleka pua zao .
Mpaka muda huu haifahamiki vijana hao wamejificha wapi huko ambako hawataki hata kuonekana sura zao.inaonyesha wengi walikuja Dar kushangaa jiji lilivyo na kuangalia mechi za Simba na Yanga zilizopigwa wikendi hii katika michuano ya club Bingwa na shirikisho kufuzu hatua ya makundi.
Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.
Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.