Wana Dodoma mkiachana na Machinga Complex, ni kipi kingine Rais Samia Kawafanyia?

Jamaa kachemka,aliamua kumsifia JPM kiaina,..asichojua ni kwamba watu wanaufahamu wa Mambo...hata baadhi ya watu ukiwasikia wanavyomnadi JPM ni kama hakuna kiongozi aliyefanya hii nchi kua hapa ilipo,...kila kiongozi kafanya kazi kwa sehemu yake na kwa ubora wake na pia madhaifu yake yapo...kuna Big Ben amejenga Taaisis karibu zote tunazoziona lkn hakua anasifiwa kama Magu mpk unashangaa akili zetu wa TZ...alichofanikiwa JPM ni kujinadi zaidi na ile kauli tumepigwa sana...kiuhalisia viongozi wote kila mmoja kuna kazi kubwa ameifanya.
 
Ulivyo mbumbumbu inashindwa kujua kwamba hapo Dodoma Serikali Inajenga mabwawa makubwa 3 ya Maji Kwa Ajili ya umwagiliaji
 
Dodoma inakuwa sana baada ya miaka kadhaa itaipiku Dar na hivi mji umepangwa. Jiwe apongezwe Kwa udhubutu wa kuhamishia shughuli dodoma aisee
 
Nakazia Yote Aliyoyasema Mleta Mada Hapa Jukwaani





Mzilankende Angekuwa Hai Labda Dodoma Ingepiga Hatua Ila Sasa Hivi Inasotasota Tu
 
[emoji107][emoji107][emoji107]
 
Nadhani promo ilikuwa kubwa sana kwa project yoyote ile aliyoifanya na uthubutu wa anko kuongelea madhaifu ya waliopita zaidi ya mazuri yao, ilimtengeneza kiasi fulani kama Hero tuliyemngojea na hiyo ndio sababu kutoweka kwake kumewafanya watu kamini kuwa hakuna jema litafanyika...

Kila kiongozi alifanya kwa ukubwa wake lakini pia walikuwa na madhaifu yao. Anko pia alijitahidi kwenye kutengeneza vitu physical ambavyo vinamuuza kirahisi kuliko pengine Ben ambaye alijenga systems ambazo direct impact inakuwa ndogo.. So, ni kumpongeza na kumkosoa kila mmoja maana wote wanastahili vyote
 
Miradi Iko kedekede ,Dom haipoi Wala haidodi ni ushamba wako na kuwa misinformed tuu.

Mwisho Magufuli hakuwa na mradi wa familia yeke hapo Dodoma na kinachoitwa miradi ya Magufuli sijui ni ipi hasa?
 
Kuna mtu humu jf anaitwa Mpwayungu village,yeye husinda kuwatukana walimu tuu !!! Wakati kwao Dodoma choka mbaya ombaomba wa kuzidi!! Poor Yuu mpwayungu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…