Bila shaka somo nimelipata sasa..
Binafsi nilikuja humu kwa nia ya kutaka kujifunza, lakini pia kuweza kutoa kidogo nilicho nacho ili niweze kusaidia wengine huku nikiwa bora zaidi.
Ofcourse mimi sio mtakatifu nina mapungufu yangu kama kila mtu..
Ila leo ndio lile somo kuu limeniingia
Ya kuwa
USIPO JI MASTER WEWE MWENYEWE HAKUNA MTU NJE ATAKAYE KUSAIDIA. CHANGE YOYOTE L7AZIMA IANZIE NDANI YAKO NA WATU WAKO KWAJILI YA KU MIRROR KILE KILICHOMO NDANI YAKO.
Nilipo ingia humu, nilikuwa mtu poa sana, nilikuwa napenda kutoa ushauri na kuongea madini chungu mzima, ila baadae watu wakachukulia ile kama weakness, maana ilikuwa kama nataka kuwapangia
maisha, basi nikawa nawavumilia nikawa navumilia, ila baadae nikajua kugundua kuwa watu ni wabaya sana watu wanapenda egoism kuliko vulnerabitly.
Watu wanapenda kuweka wengine chini, kwa manufaa yao... Wanapenda kufanya mizaha kwa watu wengine ili tu wajiskie vizuri hata kama yule wanayemfanyia yuko sawa.
Nikasema nitawanyoosha, ndipo nilipo ianza hii kampeni ya kusumbua na kupenda battle na majibizano. Mimi ni mtu mwenye kusoma sana vitu na nina hazina ya vitu vingi sana kichwani so linapokuja swala la majibizano lazima usande tu. Nitakupelekea moto hatari.
Nimesumbuana na watu wengi sana ambao kila mmoja aliaga mashindano kwa namna yake,
Tuanze na
Kiranga huyu jamaa alikuwa na tendency ya kuweka logic kwenye kila jambo na anataka mawazo yake yawe viable kwenye muktadha wa logic... Ila nilimpelekea moto mpaka a kanipiga ignore...
Akaja
Seran binafsi mwanzo kabisa sikujua kama ni mwanamke, ila baadae tukianza kuzoeana na ikafika hatua tukawa marafiki, ila sasa Seran alikuwa anajitapa sana na kila nikijaribu kutongoza anacho la, basi bwana Nika tokea kuchukua tu, nikaanza kumsumbua, ikafika mahala Nika tumia ID ya Elevenn ambayo ilikua kunaswa na mods baada ya kuchanganya mafaili na ile ya de Gunner nikadakwa.
Nilimsumbua mpaka kichwa ikawaka moto, akaja kuniwekea matusi lukuki kwa pm, nami nakasema huyu kasha jaa, ngoja nimwaibishe mbele hadharani.. Mimi ndiye niliemfanya akalimwa ban. Ndo maana hadi leo hataki kabisa kunisika na nahisi a nawaambia member mimi ni mtu mbaya sana. 🤣
Haya kuna huyu jamaa
The Icebreaker alijifanya anajua sana kushambulia watu na VAR ila cha mtema kuni alikiona. Alikuwa anadhani atanibadilisha ila alinyoosha mikono na kuanza kutumia lugha za kejeli mpaka ku qoute machapisho yangu ili watu wa nione mbaya ila wapi, mwamba nikirudi unazidi kupaa kwenda juu. Ikafika hatua aka surrender..
Kuna huyu pia
Manyanza naye akaja kujaribu battle ila wapi, akaishia kujaribu kuwaambia member wanipe ignore. Nikiweka nyuzi kijiji chote ni changu. Sio kwasababu ni naweka vitu vibaya, ila energy itokayo kwenye machapisho yangu ni real. Watu wanajua bwana
Haya twende kwa wadada kuna huyu
Lamomy huyu tumevurugana sana, ila anatambua moto wangu na kuna muda huwa anajirudi tunacheka tena. Anajua kabisa akijaribu ku cross mipaka ikawaka hatoki salama.
Haya kuna pisi na wadada ambao nilikuwa nawaandikia nyuzi humu..
Binti wa zamani ShesRise_1 na mwishowe
binti kiziwi najua mnanichukia vibaya sana, ila ndo hivyo yote haya nimeyafanya kuonesha kuwa naweza kufanya lolote..
Kama mtawiwa kunisamehe sawa, ila ndo nilifanya vile tu ili ni furahi na nitumie uwezo wangu wa ki uandishi..
Nawapenda sana kama dada zangu, na sikuwa na intention za kuwa dhalilisha.
Especially
binti kiziwi aliniasa sana nisifanye nilicho kifanya ila ego yangu ili kataa kabisa. Pole sana Binti kiziwi
Ndugu zangu, wanabodi,
Maisha haya ya ID feki ni matamu na unaweza kufanya lolote nayo, ila tambua reality yako haibadiliki kwa kufeki maisha. Unatambua wewe mwenyewe kama unashidhia ugali dagaa, au unakula I star hoteli. So, unapo kuja kusumbua watu ujue kuna time kweli watu wanakereka. Kama utataka wakukimbie na wakutenge endelea kufanya hayo ila kama utakuwa mwerevu kujua kubalance utaishi nao vizuri tu.
Binafsi nimetambua hasira sio issue, na kukomoana sio kigezo cha kukubalika.
Nimeona nirudi katika ile hali ya kawaida na nitakuwa member kama wengine. Maana watu hufikia hatua wanakuchoka na sio issue wala nini.
Na cha mwisho kabisa JF sio sehemu mbaya kama nilivyo kuwa nasema, ni sehemu nzuri na kuna madini mengi mno, nimeweka bookmark ya nyuzi nyingi sana ila huwa nina procrastinate kuzzisoma, sasa naanza rasmi. No drama anymore.
Heshimu watu nawe utaheshimiwa
In love and light🪐
de Gunner
*edit.... Naona watu wamefura na kunijia juu, katika huu uzi sijatukana mtu kwa sababu ni naona haina haja tena... Nnaombeni mchukue mazuri na msiweke hisia mbaya maana sio lengo la huu uzi. Nimeelezea kitu kizuri kwa manufaa ya members wote. Najua itakuwa ngumu maana watu tunatawaliwa na ego. Mnaotukana poleni sana maana haisaidii kitu.