Wana JF kuna 15000Tsh kwa atakaejibu swali hili.

Wana JF kuna 15000Tsh kwa atakaejibu swali hili.

Aliyeona huwez kumbishia akatulia
Vs
Aliyesikia unaweza kumbishia akatulia

Aliyesikia hataki kuulizwa maswali
Vs
Aliyeona maswali anaytaka muda wowote

Aliyesikia anaweka maelezo yaliyochangnyika na mapendekezo yake kwa KIAS KIKUBWA.
Vs
Kutakuwa n kias KIDOGO sana cha maelezo yaliyochangyika na mguso wa kihisia au maoendekezo kw aliyeona

Alieona hawezkurudia mara mbili stori tofauti ya tukio moja
Vs
Aliyesikia anaweza kurudia maelezo mawili tofauti kwa tukio moja
 
(1)Aliyeona akakusimulia habali zake huwa zinakuwa kwa kipindi maalumu yaani inategemeana na uhai wa msimuliaji
(2)Aliyesikia akakusimulia habali zake hazina mda maalum inaweze ikachukua miaka na miaka
(3)Aliyeona akakusimulia mara nyingi huwa inakuwa habali ya ukweli mtupu
(4)Aliyesikia akakusimulia mara nyingi huwa habali yake inaongezwa chumvi
 
Nipe 15k yangu
  1. Uhalisia wa mazingirq
    • Aliyeona anajua mazingira na hali halisi ya tukio, hivyo anaweza kutoa maelezo ya kina.
    • Aliyesikia anategemea maelezo ya mtu mwingine, hivyo habari inaweza kuwa na mapungufu.
  2. Uhalisia wa Tukio
    • Aliyeona anawasilisha tukio kwa maono yake, akieleza hisia na maelezo halisi.
    • Aliyesikia anaweza kuleta tafsiri tofauti, kwani ni maelezo ya pili.
  3. Uhakika
    • Aliyeona anaweza kuthibitisha ukweli wa tukio aliloshuhudia.
    • Aliyesikia anaweza kuwa na shaka kuhusu ukweli wa taarifa aliyosikia.
  4. Uwasilishaji
    • Aliyeona anatumia vigezo vya kuona na kuhisi, hivyo habari inaweza kuwa na undani zaidi.
    • Aliyesikia anatumia maneno pekee, na anaweza kukosa vipengele vya kihisia.
  5. Athari kwa hadhira
    • Habari ya aliyeona inaweza kuathiri wasikilizaji kwa kina kutokana na uhalisia wake.
    • Habari ya aliyesikia inaweza kuwa na athari ndogo zaidi, kwani ni tafsiri ya pili ya tukio.
Tai dume kijana wangu upo?
 
alieona ataongeza chumvi
aliesikia atapunguza

Alieona ataonesha na vitendo
aliesikia ataigizia sauti tu

Alieona anajua tukio zima pande zote
aliesikia anajua kwa upande tu

Alieona anaweza akatabiri hitimisho
Aliesikia hawezi


naomba 15000 yangu nikale😌
 
Nipe 15k yangu
  1. Uhalisia wa mazingirq
    • Aliyeona anajua mazingira na hali halisi ya tukio, hivyo anaweza kutoa maelezo ya kina.
    • Aliyesikia anategemea maelezo ya mtu mwingine, hivyo habari inaweza kuwa na mapungufu.
  2. Uhalisia wa Tukio
    • Aliyeona anawasilisha tukio kwa maono yake, akieleza hisia na maelezo halisi.
    • Aliyesikia anaweza kuleta tafsiri tofauti, kwani ni maelezo ya pili.
  3. Uhakika
    • Aliyeona anaweza kuthibitisha ukweli wa tukio aliloshuhudia.
    • Aliyesikia anaweza kuwa na shaka kuhusu ukweli wa taarifa aliyosikia.
  4. Uwasilishaji
    • Aliyeona anatumia vigezo vya kuona na kuhisi, hivyo habari inaweza kuwa na undani zaidi.
    • Aliyesikia anatumia maneno pekee, na anaweza kukosa vipengele vya kihisia.
  5. Athari kwa hadhira
    • Habari ya aliyeona inaweza kuathiri wasikilizaji kwa kina kutokana na uhalisia wake.
    • Habari ya aliyesikia inaweza kuwa na athari ndogo zaidi, kwani ni tafsiri ya pili ya tukio.
UMECHEMKA NDUGU
 
20240822_140219.jpg


Haina maana kwa sababu naweza kuona pasipo mimi kuwa eneo husika, pia naweza kusikia pasipo eneo husika.
 
  1. Chanzo cha taarifa:
    • Aliyeona anapata taarifa moja kwa moja kupitia kuona, hivyo anaweza kutoa maelezo ya kina zaidi.
    • Aliyesikia anapata taarifa kupitia sauti, ambayo inaweza kuwa na ukosefu wa maelezo ya kina.
  2. Uhalisia wa tukio:
    • Aliyeona anaweza kuelezea mambo kama jinsi yalivyokuwa, ikiwemo hisia na mazingira.
    • Aliyesikia anaweza kuelezea tu kile alichosikia, bila picha ya halisi.
  3. Uthibitisho:
    • Aliyeona anaweza kuthibitisha ukweli wa tukio kwa ushahidi wa moja kwa moja.
    • Aliyesikia anaweza kuleta uvumi au maelezo yasiyo na uhakika.
  4. Uelewa wa hisia:
    • Aliyeona anaweza kuelewa na kuelezea hisia za wahusika kutokana na uhalisia wa tukio.
    • Aliyesikia anaweza kuwa na ufahamu mdogo wa hisia hizo.
  5. Usahihi wa maelezo:
    • Aliyeona anaweza kuwa na maelezo sahihi zaidi kutokana na uzoefu wa moja kwa moja.
    • Aliyesikia anaweza kuwa na maelezo yasiyo sahihi kutokana na tafsiri ya mtu mwingine.
 
1. Uhalisia wa maelezo: Aliyeona ana maelezo ya moja kwa moja kutoka kwa tukio, wakati aliyesikia anategemea maelezo ya mtu mwingine ambayo yanaweza kuwa na mapungufu au kuongezwa mambo.

2. Kina cha maelezo: Aliyeona ana uwezo wa kuelezea kwa kina mambo madogo madogo, kama vile mazingira, mihemko, na matukio ya pembeni, wakati aliyesikia anaweza kutoa tu muhtasari au vipande vya habari alivyovipokea.

3. Uhakika: Aliyeona ana uhakika zaidi wa kile kilichotokea kwa sababu alishuhudia mwenyewe, lakini aliyesikia anategemea chanzo chake, na kuna uwezekano wa kupotoshwa au kuwa na shaka juu ya ukweli wa tukio.

4. Mitazamo ya kibinafsi: Aliyeona anaweza kuwa na maoni na hisia zake binafsi kuhusu tukio kwa sababu alikumbana nalo moja kwa moja, wakati aliyesikia anategemea mitazamo ya aliyeeleza kwake, ambayo inaweza kuwa ya upendeleo au kuathiriwa na hisia za mwingine.

5. Ushuhuda: Aliyeona anaweza kutoa ushuhuda wa moja kwa moja kuhusu tukio, wakati aliyesikia anaweza kutoa ushuhuda wa pili au wa tatu, ambao hauna nguvu sawa kisheria au kihistoria kama ushuhuda wa moja kwa moja.
 
ALIYEONA AKIKUSIMULIA
1: Huhusisha matendo na ishara kutokana na tukio

2: Hukutengezea taswira halisi ya tukio
3: Huhusisha hisia katika usimuliaji wake eg Huzuni, furaha, hasira n.k
4: Ataongeza chumvi kidogo sana Kwa lengo la kunogesha stori lakini maana ya msingi hubaki vile vile.
5: Hutumia kila namna kumshirikisha msikilizaji katika Taarifa yake na hupenda kuona hisia za msikilizaji kutokana na tukio analosimulia.

ALIYESIKIA AKISIMULIA
1: Hahusishi matendo kwani hajui tukio limetokeaje na mazingira ya utokeaji.
2: Hawezi kutengeza taswira halisi ya tukio kwani huwa Hana uhakika wa kile alichokisikia kama ndio uhalisia.

3: Ni ngumu kuonesha hisia katika masimulizi na wakati mwingine tukio la Huzuni anaweza kugeuza kichekesho kwani nae kasikia tu.

4: Taarifa Huwa na chumvi nyingi kutokana na kupita Kwa watu tofauti tofauti ambao nao hunogesha Taarifa Kwa kuongeza maneno.

5: Hahitaji kushirikisha sana wasikilizaji kwani lengo lake ni kusambaza Taarifa na sio kujua uzito wa jambo analosimulia.
 
Watu wa Physics tutulie tuwaachie watu WA literature waendelee ku-discuss vitu vyao... Watu WA soft science endeleeni
 
Back
Top Bottom