Hizi Huwa ni njia dhaifu na za kivivu kwa askari vipi kama vocha imewekwa siku mbili nyuma alafu tukio likatoke siku mbili MBELE?Pole yake sana.
Hayo maujinga yanatumiwa sana na wahalifu, lengo likiwa ni kuchelewesha ufuatiliaji wa Polisi.
Mkuu siyo tiketi na document zingine muhimu tu, hata hizi vocha za kukwangua ni mbaya sana kutupa tupa ovyo.
Ikiokotwa na hao jamaa kisha kutupwa kwenye tukio, wakifuatilia vocha ilijazwa kwenye simu gani, utakwenda na maji.
Kuja kujulikana hauhusiki, pamepitwa!
Anasema yeye alipopigiwa simu kuwa anahitajika police Kimara naye anaishi Tegeta kwanza akapata wasiwasi na alipouliza kosa lake akaambiwa atajua akifika.Anatoa taarifa Police
Ndio, na wananchi wa kwanza kufika alfajiri kwenye tukio ndio waliona tiketi yake.Tuanzie hapa... Karatasi iliyokutwa kwenye tukio (tiketi)... imefikaje huko... Yaani mtu aliiokota na kuipeleka sehemu ya tukio..??
Vipi kama wabaya wake walikuwa nje kwake au kama walikuwa jirani na kituo cha police ila wametumia gia ya upolice?Kosa la kiufundi ni kuitwa na kugoma kwenda, hapo ndipo amethibitisha amehusila..
Hivi unaitwaje police kisha usiende? Alafu uzime na simu kabisa?
The fact kwamba alikuwa maeneo ya Kimara recently nayo inazidi kutoa petroli kwenye moto unaowaka...
Kuna uwezekano wa asilimia 70 rafiki yako ni mhusika, na pengine kilichokutwa huko si tiketi, umeitaja ama imetajwa tiketi kama kutoa muunganiko wa habari...Ndio, na wananchi wa kwanza kufika alfajiri kwenye tukio ndio waliona tiketi yake.
Mashuhuda wanasema uhalifu ulitokea usiku kimya kimya.
Na police walipofika wakakutana na kidhibiti safi.
Mkuu, hii mbinu ipo sana ya kuuziwa kesi kwa kutumia taarifa zako.
Mpaka uje kutoka au wajue hujahusika....muda ushaenda sana
Inawezekana, na ndio maana pale juu nikaandika 'binadamu anabadilika' japo huyu kaka hana tabia za uhalifu.Kuna uwezekano wa asilimia 70 rafiki yako ni mhusika, na pengine kilichokutwa huko si tiketi, umeitaja ama imetajwa tiketi kama kutoa muunganiko wa habari...
Jamaa anaishi wapi? Na tukio limetokea wapi?
Hicho kidhibiti sio tiketi kwa 80%
lakini mkuu si kila simu unayopigiwa ukaambiwa imetoka polisi inakuwa kweli zingine ni mitego tu ya wahuni..kwani wakina Soka si walipigiwa simu kama hivyo wako wapi leoAeleze ukweli wote is all, then akae kimya, wala asisumbuke, ila kama kweli ni Mhalifu basi akomae, tuna wahalifu wengi tu kwenye Jamii zetu humu mtaani!
- Unaitwaje Police unazima simu?
- Unakaa kabisa home na Amani?
Dalili za Mhalifu hizo hapo 2, mtu mwema akiwa na wito police hawezi relax!
Na ndio maana kwenye post pale juu nimeandika 'binadamu hubadilika'Usimtetee sana....
kuna kesi ya dogo mmoja hivi, dem wake alikua anaapa viapo vyote "huyu hawezi kubaka namjua tangu utotoni bla bla anasali ni mpole bla bla blaaa" jamaa nmekaa nae mezani nkaongea nae vizuri tu " kuwa mkweli hili tukio umefanya au haujafanya" kwa kinywa chake akasema kafanya....kabaka.
Baadae kidem kinakuja vipi amesemaje, namie nkakipoza tu hajafanya.
Huyo jamaa yeye mwenyewe ndio anaujua ukweli
AnasemaHuyo rafiki yako siyo smart, huwezi tupa tiketi mahali popote, better destroy it before dumping.
Pia kwa nini alizima simu alipopata mwito wa polisi ? Angeenda pengine issue ingekuwa ndogo.
All in all atatoka ila na pesa itamtoka
There is no way kwamba jamaa ahusiki, japo ndio anaweza asihusike kwa asilimia zote,Inawezekana, na ndio maana pale juu nikaandika 'binadamu anabadilika' japo huyu kaka hana tabia za uhalifu.
Jamaa anaishi Tegeta kwa Masister na tukio limetokea Kimara bucha.
Na tiketi aliitupa Mbezi stand kuu ya mabasi ya mikoani
Aisee! Umenikumbusha mbali. Enzi za kukwangua vocha kabla huduma ya kununua vifurushi kwa njia ya simu haijaanzishwa. Kwa sasa nilishasahau kabisa kuongeza salio kupitia vocha.Hata vocha ya karatasi , chana vipande vipande tupa.