Wana JF narudia tena, haribu kabisa tiketi au karatasi yenye taarifa zako kamili

Unafikiri wale wapelelezi ni wajinga hawakwenda shule? Ukiwa na kesi inayohitaji upelelezi utajua kuwa wanajua wanachofanya.
Polisi wana vitengo,kuna vitengo tofauti.
Nilishuhudia hi kwenye ile kesi ya yule billionaire wa Arusha(jina limenitoka;aliuliwa alipokwenda kuonana na wauza madini).

Sema kibongobongo resources zinatumika kesi kihusisha wakubwa tu tofauti na mbele. Ili mradi umefia kwenye nchi yao lazima wareconstuct tukio na kusaka wahusika
 
Si ndio maana wanaendelea na uchunguzi. Kwani vitu vyote hivyo wanaweza kuvipata siku moja kama unasema watatakiwa pia kuwasiliana na makampuni ya simu, wenye bus husika pia maswala ya DNA kama yanahitajika. Tuwaacha waendelee na upelelezi kwanza. Pia hatuwezi kumsemea sana huyo jamaa anaweza akawa alihusika pia tena kama inasemekana ni mtu mkimya sana na msiri sana, wengi wao huwa ni hatari sana.
 
Kosa la rafiki yako ni kushindwa kutii sheria bila shuruti.

Kwa nini azime simu baada ya kujua kuwa anahitajika kituo cha Polisi.
 
mkuu hizi njia zako mbona haziaminiki sana kwenye kukunasua na msala.kwani hiyo kuwasha Smart tv,laptop au simu unaweza usiwe karibu navyo yaani unaweza kuwasha simu au trakick device yoyote alafu unaiacha geto kwako mfano unaishi mbagala au bagamoyo kisha unaenda kupiga tukio huko mbezi.mpaka hapo ushapiga chenga hii ya kuangalia simu yako ilisoma wapi wakati wa tukio kwa wapelezi smart haiwezi kuwa na nguvu sana japo inafaa..kwa ishu ya jamaa kwa maelezo ya mtoa mada hiyo risiti yake ya basi ya EFD baada ya wezi kuvunja duka na kuiba vitu kisha hiyo risiti ya basi ya EFD wakaweka juu ya meza wakasepa zao ..hapo finger print inaweza saidia kujua nani alishika ticket mara ya mwisho.
 
Zinafanya kazi inategemea kwa angle gani umetazama.Screen time, authentication, interaction zako kwenye apps zinafanya kazi nimeona kesi kibao watu wa digital forensic wakitumia.

Inaporeconstruct tukio huwezi tegemea dhan moja pekee, vipi kama aliyepiga tukio alihakikisha ticket haiguswi na mwingine mpaka anapeleke kwenye scene? unadhani ni ngumu?

Kama mtu unafuatilia hiyo ishu ya fingerprint mbona inakwepa sana. Watu wanaingia ndani wanaua, wanachomoka polisi wanainvestigate scene hawapati ushahidi wowote.

Ndiyo maana unaona polisi mbele wanaanza na alibi ya mtu kabla ya kitu kingine chochote na nani au kwa namna gani inaweza kuthibitishwa.
 
Umenifurahisha, unawaza kwamba hawa jamaa wanapeleleza kiutalaam kama kule majuu?
Labda kama mwathirika wa wizi (mwenye mali) awe kigogo mkubwa, ndio watafanya hayo yote ya fingerprints, sijui DNA etc. Kama tukio limetokea dukani tu kwa Massawe au Mpemba wa kawaida, kanatumwa kapolisi fulani ambako kanataka pesa kutoka kwa aliyeibiwa na kutoka kwa mtuhumiwa.

Nimewahi kuibiwa kwa kwa kubomolewa milango na madirisha, na wakaondoka na vitu. Matukio mawili yalikuwa ya usiku na moja la mchana.
Katika matukio yote hayo nilikuwa nafikiri polisi watakuja na full gear na kufanya kama nionavyo kwenye CSI tv series lakini wapi bwana.
Wanafika wanakuuliza unamshuku nani? una hela ya maji? Wanazunguka zunguka tu na kusema faili sijui limefunguliwa kituoni. Kila ukienda kuulizia, mara gari halina mafuta, eti uweke mafuta kwenye defender halafu wakafanye upelelezi. Hii nchi ukiwa mdogo kiuchumi na kimadaraka, ni mateso sana.

Katika matukio hayo, tukio mmoja nilifanikiwa kumkamata mwizi mmoja kwa ushirikiano wa wananchi wenzangu na kutumia polisi wakituo kingine (kishikaji) ambapo tulianzia kwa aliyekutwa na mali iliyoibwa.
 
Sahihi kbsa
 
Hata vocha ya karatasi , chana vipande vipande tupa.
Hili ni tangazo lilitolewa kabisa ukiitumia chana, natumia vocha mara chache sana, jamaa walifanya uhalifu/mauaji wakaacha vocha kwenye tukio, kilichomkuta mtumiaji wa ile vocha anakijua mwenyewe, kuanzia hapo nikutumia nachana vipande hata 20 maana vinne vitano wataungaunisha
 
Kwa polisi wetu wa Tanzania Mtu wa Mwisho kuwasiliana au kuonana na marehemu ndo mtuumiwa mkuu hakuna cha upelelezi ni kubashiri tu
 
Mleta mada kuna uwezekano rafiki yako kahusika moja kwa moja kwenye tukio.

Yeye kukataa wito wa polisi na kuzima simu ni viashiria tosha kwamba jamaa kahusika directly ama indirectly

Anyways, Muda utaongea na ukweli utajulikana
 
Huu ni uzembe na uvivu wa wapelelezi na polisi, Ni simple tu kabla ya kukamata mtu waangalie vocha ilijazwa mda gani na tarehe ngapi, walinganishe na mda wa tukio la uhalifu, na siyo kukurupuka kukamata mtu kwakua tu umekuta vocha kwenye eneo la tukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…