Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Paskali, mwanzo mgumu, hata hivyo umepata uzoefu. Down side yake ni kuwa unatakiwa uwe makini na mabandiko yako hapa janvini maana mrengo wako unajulikana na umegaragazwa.
 
Huu uzi Sijui kwa nini umenichekesha balaa, pole Sana Mayalla hiyo ndio CCM bwana kutoboa sio mchezo.

Kuna watu wamewekeza humo miaka na miaka lakini bado hawajatoboa sembuse nyie mnaokurupukia dakika za majeruhi.

Umevuna ulichopanda.
 
Natamani kuendelea kuona mapambio yako jukwaani, baada ya kukiri CCM ina wenyewe.... sokapohapa!!
 
Ni ukomavu kujipima kwa wenzako kwa utaratibu wenu.

Kumbuka kuwa karibu na wananchi wa jimbo lako wakati mwingine watakukumbuka pia.

Na uchaguzi lazima apatikane mshindi, vumilia nyakati hazijaisha.
 
Wewe tumekubembeleza hapa sema unagombea wapi utaki kusema hata sasa subilia mwenyekiti atakavyoamka


ila hongera kwa kujaribu
 
Pole sana Nyanda ila mbona mnaoshabikia Magufuli wote ni kama vile mmepigwa chini kura za maoni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…