Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Wenyewe vipi! Sema hukuwa na mizizi wala connection, unaingia kwenye ushindani humjui mjumbe hata mmoja utegemee kutusua kweli.
Hata mim nimemshangaa makonda, unashindwaje kuwamudu watu 300 ndani ya miaka 5
 
Aendelee kuimba na kuabudu labda atakumbukwa kwenye teuzi
 
Kwanza hongera kwa kujitosa mazima. Pili sidhani kama ni sahihi kusema ccm ina wenyewe. Ni vile tu kwamba hukujiandaa. Kwa maoni yangu, angalau mara baada ya uchaguzi kuisha, ndio muda muafaka kujitosa kuwania nafasi uchaguzi ufuatao. I
 
Hivi uwandike makala baada ya Magufuli anayetufaa Makonda unategemea ubaki salama mbele ya watu wenye akili?
 
Pole sana ila ndiyo mwanzo yamkin utakuwa umejifuza kitu
 

Usikate tamaa mkuu. Huu ni mwanzo wa mchakato tu.

Bado kuna nafasi ya jinsi mzee baba atakavyo amka.
 
ila ccm mmejianika sana msimu huu, taaluma zenu zipo rehanini. Tumewajua wengi saizi inabakia kuwachora tu...HONGERA KWA HATUA HIYO, naamini 2025 ukirudia utapata kura zaidi. Kinachoniuma zaidi ni dodoma mjini yule kijana wa ccm ni kichwa maji sana nashangaa anapita eti, wajinga humpigia mjinga mwenzake nimeamini. Yaani licha ya kuteuliwa kuwa naibu waziri lakini sioni cha maana anachokifanya ni mweupe kwakweli. Inamaana ccm haina wagombea wa kijanja???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…