Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Hata kule kweitu Mwibara yule mwanaharakati huru mbona yeye ndio alisikitisha? Nafuu Mayala kashinda kwa kura 1. Yule bwana aliokota yai. Chama kina wenyewe
 
Kuliko kusema CCM ina wenyewe, ingekuwa vizuri ukubali kuwa huna ushawishi mkuu.
Pole sana.
 
Hukujaribu bali uliingia darasani sema tu lugha yao hukuisikia vilivyo. Next time utatoboa usirudi nyuma. Aliyeshunda akipata tatizo tu usiogope kuchuka fomu
 
Mkuu mimi nikupe hongera. Wote ni washindi. Jambo kura kutosha. Ukiingia kucheza unajifunza mengi. Unajinoa unarudi kupambana
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!

Kwanza nimekubali matokeo na kukubali kuwa ama kweli CCM Ina wenyewe!

Nipeni tu pole!.

Paskali

Uchaguzi 2020 - Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata
Wakuu kwani hizi si kura maoni tu zitachakatwa huko mbeleni au? Mbona yanachukuliwa kama ndo matokeo ya mwisho chamani?
 
Hongera kwa kuingia kwenye database ya ccm huenda mbinu hii itafanya kazi na jamaa akakuona na kukuteua! Usife moyo na usibweteke kwani hajaamka bado!
 
Pole mkuu.
Usijilaumu ila jua kuwa umetengeza sifa nyingine na experience nyingine ya kisiasa.
Sehemu kama jf tuna mitazamo tofauti, so kubari yote tu mkuu.
 
Back
Top Bottom