Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uliwahi kushiriki vipi kuijenga Ccm? Leo uje usererekee ubunge si ungeanzia hata udiwani! Au kwakuwa wahome ndotop manyotaWewe kama mchambuzi,mchokonozi na mchunguzi wa habari hukuona dalili ya anguko hili?!? Hukujua hukubaliki?? Kagombee kupitia ACT acha kulazimisha mapendo kijani purple nayo rangi mdogoangu.
 
Pole sana Pascal Mayalla. Kama uko 'serious' hasa na kutaka kuingia kwenye kazi za kuchaguliwa kwa kupigiwa kura, basi unahitaji kuwa na maandalizi ya kutosha katika maeneo mbalimbali. Mojawapo ya eneo la kufanyia maandalizi ni kufanya utafiti wa kisayansi ili kujua ni kwa kiasi gani unakubalika kwa wapiga kura. Vinginevyo kama utaamua kuingia kichwa kichwa, utajikuta unaangukia pua.
 
Nampongeza Pascal Mayalla kwa kutoweka genge la Waiba Kura lakini kwavile ameshaonesha nia na kuwaonesha watu yeye ni "Mzalendo" na Mwana-CCM, basi tumemwandalia kiti kwa sababu hiyo ilikuwa ndo ahadi yetu baada ya kikao chake na Ndugai kule Dodoma!!

Baada ya kikao chake na akina Ndugai tulimweleza he'd keep low profile from JF for weeks kisha arudi kivingine huku akikumbuka Chanda Chema Huvikwa Pete!!

Hapa tunajaribu kuangalia ni wakati gani mwafaka wa kumpa kiti chake, ingawaje wengine wanaamini wakati muafaka ni ule muda kuelekea uchaguzi mkuu kwa sababu watakuwa busy sana!
 
wewe ndio mmoja wa wanafiki wakubwa hii nchi. Mnafiki sana na unaendekeza njaa kishamba sana.
 
Bora amekosa maana sio kwa masifa aliyoanzisha kwa mheshimiwa.
 
Hahahaha kila nyumba ina waenyeji mhe.sio mgeni kuja nakuparamia mpaka bedrooms za waenyeji bwana.....uzoee zoee kwanza
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!

Kwanza nimekubali matokeo na kukubali kuwa ama kweli CCM Ina wenyewe!

Nipeni tu pole!.

Paskali

Uchaguzi 2020 - Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata
Pole sana mkuu kwa matokeo ambayo hukutegemea. Lakini umeonyesha ukomavu kwa kuthubutu kugombea; na baadaye kukubali matokeo. Huo ndio ukomavu ninaouzungumzia. Siyo kuanza malalamiko yasiyo na kichwa au mkia. Kila mmoja wa wagombea alikuwa anajiamini. The people have spoken. Tushukuru maamuzi yao na kuanza kuganga yajayo.
 
My uncle [emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]...
 
Wanabodi,

Hili ni bandiko la ombi maalum kwa Wana JF wenzangu, nawaombeni sana mnipe pole na msinicheke, wala msinibeze, kujaribu kugombea ubunge wa Kawe kupitia CCM, nimeambulia kura 1!

Kwanza nimekubali matokeo na kukubali kuwa ama kweli CCM Ina wenyewe!

Nipeni tu pole!.

Paskali

Uchaguzi 2020 - Pascal Mayalla aomba kura Kawe, adai akipitishwa atagawa Tshs. Milioni 10 kwa kila Kata

Kaka Paskali pole sana, kheri ww umejaribu kuingia uwanjani na kucheza na kushindwa, ni hatua kubwa kuliko yule ambaye hata kujaribu tu kuchukua fomu hajajaribu.. Pongezi kubwa, ila kaka kura 1 duuh inaelekea watu hawakujui kabisa Kawe, umepigwa mtama kweli polee 😂
 
Back
Top Bottom