Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Mwana mkaidi hapewi pole.

Karibu tuendeleze mijadala yenye afya hapa JF. Tactic yako ya kujipendekeza kwa kumsifia Jiwe na kujipendekeza CCM is not working. Go back to the young YOU; Achana na kusifia sifia na kuabudu.
Haka kaukumbi hakamtoshi ahamie redioni, Luningani na magazetini
 
Brother Paschall Hongera kwa hatua kubwa ya Kisiasa, Umepata Uzoefu ambao kwa hakika ni Mtaji kwa Safari ya Kisiasa ijayo, usiyumbishwe na Maneno ya Mitandaoni wewe komaa ipo siku ya Neema yajja.
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 Pole mkuu. Ccm haina wenyewe bali inahitaji mbinu na ushauri tosha toka kwa wakongwe wa eneo husika.

Ukitafuta wapambe tafuta wale wa eneo lengwa, uwe na hela sasa sio unaitwa boss hata ya maji hutoi. Ni kujipanga miaka mitatu kabla ya uchaguzi huku ukiunda ngome kimya kimya.
 
mamlaka za uteuzi tayari zimekuona, ila tupe muda tujiridhishe kama uyasemayo ni kweli, by the way hakuna ulichopoteza, mpoki kapata zero , Makyembe,Magembe na wengine kibao wimbo ndo huo huo kifo cha wengi ni harusi!!
 
Umefanya nin Kawe mpaka ukagombee huko? Sikutegemea mtu kama wewe unae jitambua kwa kiasi kikubwa kujipeleka tu hujawahi hata kukutana na wajumbe wa mkutano mkuu wa kata unaenda tu kwa vile unafikiri ukiongea kwa dakika moja utaweza ku mconvice watu wakuchague

Tatizo wengi mlioenda kuchukua fomu mnawaza kama wagombea na sio kama wapiga kura, ungewaza kama mpiga kura usingeanzia ubunge. Nimefurahi mno kwa Tarimba kushinda Kinondoni amefanya mambo mengi tangu akiwa Diwani nadhani ni mfano mzuri wakuigwa. Angalia Dr Tulia ametumia sio chini ya miaka minne kujijenga kisiasa angalia kura alizovuna.

Hi decision umeifanya kwa mihemko.
 
Pole, ila nawe ulizidi kuimba na kuabudu humu ukadhani ndio utapitishwa

Halafu P zamani ulikua mtu safi sana, straight foward with no fear, mara ghafla ukabadilika ukaanza kuunga juhudi nikajiuliza umepatwa na nini

Kumbe mwenzetu uoikua unalenga ubunge
 
Back
Top Bottom