Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Uchaguzi 2020 Wana JF, nipeni Pole. Msinicheke wala msinibeze; nimegombea ubunge Kawe kupitia CCM nimeambulia kura 1. Ama kweli CCM ina wenyewe!

Cha msingi na muhimu Ni vile unavyojiona mwenyewe sio vile wanavyokuona wao.

Kupata kura moja sio mwisho wa mbio za siasa. Binafsi nakuona Kama shujaa wangu.

Hata mbuyu ulianza Kama mchicha, Ni kujiuliza tu nimekosea wapi, nakosea wapi ili uboreshe kura zako wakati kwingine
 
Umetia nia.. wewe ni CCM.. umeandika haya!!!.. tatizo moja kubwa uliloonyesha.. ni kwa maneno ya CCM ina wenyewe hapo ungefafanua zaidi na sio kuja kutaka kuonyesha chama kina kama ubaguzi fulani kwa kupata kira MOJA ukawahi humu. Wewe umeonyesha kuwa ni mlalamishi umepewa nafasi kuwania halafu eti chama kina wenyewe.

Ulichobidi kufanya ungenyamaza soma yanayoandikwa ungekaa chini na kujitafakari.. rudia uliyoongea. Je, ulifikiri pesa zingevutia iweje leo. Je, unanini hata umefanyia chama na wana jimbo la Kawe ni mengi. ila muhimu muda ulipewa kuongea.. je uliongea ya kuvutia.. ulijionyeshaje.

Tulia kama ni uteuzi unataka.. basi ndugu.. kuwa smati.. mwenye nia uendana na mengi.. muwe mnakuja kutuuliza tuwafunze uongozi.. ingawa mimi sio kiongozi popote kisiasa.. ila nina x-factor.

Kila la kheri mbeleni..
 
Pole ndio maana wanasema huo ni mchakato wa awali.

Nimeiona mtu Kama Methuselah Gwajima yaani yeye na kaka yake wote waliomba Ubunge Jimbo moja.

Huyu Furaha Dominick mshindi wa leo yasemekana alikuwa pia anaingiza Irani kwamba mzee baba kamtuma agombee. He must be very bold and tough.

Sizani Kama ataweza mziki wa Halima lakini
 
Maisha ni kujaribu, kitu kibaya ni kuogopa kujaribu sababu ya uoga wa kushindwa. Ukishindwa unakuwa umeshajua njia mojawapo ya kutowezekana kushinda jambo husika.
 
Back
Top Bottom