Wana-MMU hebu niambieni mimi ni mwanaume wa ajabu?

Mimi napenda sana hiyo Socratic method kabla sijajitumbukiza katika mijadala kwa sababu huwa inanisaidia kutojiingiza katika mijadala yenye ombwe na kuishia kupoteza muda bure. Kama wewe hutaki na hao wenzako kwenye hiyo "sisi hatutaki" yako, basi ni nyinyi na ni haki yenu. Mimi pia ni haki yangu kama mimi kupenda hii njia ya udodosaji. Maisha ni kila mtu na lwake ali mradi sheria hazivunjwi. Kwa hivyo hakuna sababu ya kufokeana labda kama nyie wa "sisi hatutaki" mna u-Mao Ze Dong (madikteta uchwara) na mnataka mkitakacho nyie ndicho kiwe. Tutawapinga!!!
 
Kwangu mimi binafsi achilia mbali suala la kutotaka mtoto tu, bali hata hiyo ndoa yenyewe siitaki!

Sina mpango wa kuzaa kuolewa wala kushiriki tendo la ndoa maisha yangu yote, just single till i die!
Marehemu mama yangu mdogo alifariki akiwa na miaka zaidi ya 50. Wakati anaumwa aliwahi kunieleza sababu ya yeye kutokuwa na mtoto wala kutokuolewa na katika maisha yake yote hakuwahi kuonekana akiwa na mwanaume.

Alizaliwa na tatizo la njia ndogo sana katika uke kiasi ambacho hata kupitisha haja ndogo ilikuwa kama sindano ile tunayochomwa tuendapo hospitali tukiwa tunaumwa, na kwa bahati mbaya sana wazazi wake hawakutaka lijulikane kwa mtu yeyote nje na wao kwani katika mjadala nae aliniambia kuwa aliwahi kuwaeleza baada ya kuwa alikuwa akizikataa posa toka kwa wanaume waliohitaji kumuoa

Ukweli alikiri kuwa alitamani sana angekuwa wa kawaida kama ilivyo kwa wanawake wengine lakini haikuwa hivyo. Alipenda sana kama angeolewa na kuzaa lakini haikuwa hadi alipofariki

Kwa binadamu wa kawaida asiye na kasoro yeyote kuoa / kuolewa na kupata watoto ni jambo la hiyari ya lazima (force impression), ni jambo ambalo huwa linakuja tu mawazoni bila kujali

Ukiniambia unapenda kufanya hivo lakini kwasababu fulani hutofanya hivo naweza nikakuelewa zaidi. Kuna umri ukifika utafeel uhitaji wa hii makitu

Hata hivyo ni kila mtu ana maamuzi yake
 
We fala nani dicteta uchwara ? Magufuli ndo dicteta we ccm yenu . Acha ufala naona umenza ku cross line .
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] sasa tofauti si ni ndogo tu, yeye anataka ngono na ndoa hataki watoto ila mie sitaki vyote.
Na hujawahi kabisa kutiana katika maisha yako yote hadi sasa?
 
We fala nani dicteta uchwara ? Magufuli ndo dicteta we ccm yenu . Acha ufala naona umenza ku cross line .
Unaona sasa. Umeshaanza kutukana. Kwenye comment yangu wala sijakuita dikteta uchwara. Kaisome vizuri kisha kunywa maji baridi upoze injini kamanda. Mitandaoni humu hatujuani utatukana wangapi bro? Na kutukana watu ambao wala huwajui tena mbele ya kisimu chako ndo unajiona mwamba ama? Mungu Akusaidie na kukupa hekima [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Ni kweli mkuu kila mtu na sababu zake! Mimi nina sababu zangu lakini sababu hizo siwezi kuziweka hapa maana naweza nisieleweke ila sababu hizo wala siyo za kiafya!
 
Sawa mpendwa nimekuelewa . Usijali mtumishi kwakweli Mungu atujalie hekima sana . Asante sana bwana Socrates kwa kunikumbusha haya. Duuh
 
Ni kweli mkuu kila mtu na sababu zake! Mimi nina sababu zangu lakini sababu hizo siwezi kuziweka hapa maana naweza nisieleweke ila sababu hizo wala siyo za kiafya!
Sawa ndugu

Japo ungeshea hapa hata kwa ufupi huenda ungetupa elimu zaidi juu ya yale tusiyoyajua vile unajua elimu haina mwisho
 
Sawa ndugu

Japo ungeshea hapa hata kwa ufupi huenda ungetupa elimu zaidi juu ya yale tusiyoyajua vile unajua elimu haina mwisho
Sawa mkuu! Mungu akijaalia siku nitalianzishia uzi kwa sasa siko katika nafasi nzuri ya kulieleza hapa!
 
Asante mkuu mawazo yako ni kama ya kwangu...
 
Shida ipo kwenye umri ulionao sasa,

ntaifufua hii thread 2025 nione misimamo yako,

na ndoto zako zilikua kweli au nawewe shetani atakupitia.
 
Kwangu mimi binafsi achilia mbali suala la kutotaka mtoto tu, bali hata hiyo ndoa yenyewe siitaki!

Sina mpango wa kuzaa kuolewa wala kushiriki tendo la ndoa maisha yangu yote, just single till i die!

Wachache sana watakuelewa (Open Minded) ila wenye mawazo mgando watataka uishi kama wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…