Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Wana Simba SC tutaje wachezaji tunaoona hawatufai msimu ujao

Shekhe penye ukweli lazima tuseme..wewe kama shabiki umeshawahi kuichangia vipi timu yako hadi ufikie hatua ya kupendekeza majina ya kusajili na kuachwa? maana hauna tofauti na mtu asiyejielewa..unataka usivyovifanyia kazi..
wenzetu ulaya huko mtu ni shabiki ananunua tiketi kila mechi si chini ya 50000 na ananunua jezi rasmi za klabu yake kama sehemu ya kuipa sapoti timu..akienda uwanjani anashangilia mwanzo mwishooo..
nyie kulaleki mkienda uwanjani mnaishia kukaa kimya kama midomo inawanuka..
ifikie aibu muone aibu mashabiki wa soka tanzania..
Mtazamo / mawazo ya mashabiki sio sheria.. Hapa tunajadili jinsi tunavyoona timu ilivyo na huwezi kutuzuia.
Kujifanya unajua kila kitu na kutulinganisha na ulaya ndio kunakuponza mkuu.
Huko ulaya fans wakimzomea mchezaji na kusema ameshuka kiwango asipangwe au kucheza.. Haitachukua muda lazima ataondoka.. Sasa dharau yako kwa fans ni ipi kama uwanjani tunaingi, kadi tunalipia.
Acha ujiaji hovyo!!
 
Jamaa ana matangazo utafikiri kadi anayo peke yake...
Mkuu kadi hadi sasa kwa taarifa nilizonazo tunazo watu si chini ya 12000 hadi 15000 hivi...kati ya hao unakuta wanaolipia kadi zao kila mwaka ni watu 500 hadi 1000 unategemea timu itaendelea vipi hapo mzeee???? ok wewe unakadi sawa,,kadi yako mara ya mwisho kulipia ilikuwa lini?kama sio kwenye mkutano wa juzi ???
 
Wakuachwa: Zana,. Kwasi, juuko, bukaba, mbonde, mzamiru, mo Ibrahim, ndemla, salamba, mkude, kotei, Simba kwa Sasa imeyumba Sana kwenye eneo la kiungo,. Kotei na akina mkude wamefeli kabisa.
Jamani mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni. Yaani Mkude aachwe sababu ya mechi ya Kagera. Huwezi kukumbuka kazi nzuri ya mkude kwenye mechi ya Nkana, AS Vita, Al Ahally na TP Mazembe pamoja na mechi ngumu za TPL za Prisons na Mbeya city?
 
We iongelee timu yako ya yanga ya sisi simba hayakuhusu mkuu....hakuna timu Africa inayojaza uwanja mechi zote...sasa unataka simba afanye maajabu gani yaliyozishinda timu zote africa ajaze uwanja kila siku na mechi zenyewe hizi anacheza kila baada ya siku mbili hapa dar huko mikoani umeona nyomi lake.ligi ya mabingwa africa CAF simba ndo timu pekee africa iliyokuwa inajaza uwanja kuliko zote....huu ni mwanzo tu subirini mtapata tabu sana
ndio shida ya mashabiki maandazi kama ninyii..so unaona kama Afrika haiwezekani basi kwa Simba pia itakuwa haiwezekani sio???..then wacha kutumia hoja dhaifu eti mechi kila baada ya siku tatu..kwani kabla ya hapo watu walikuwa wanaujaza uwanja..tena kipindi kile mechi usiku kuanzia saa 12 hadi saa mbili watu hawaji uwanjani..alafu leo unakuja hapa unandika pumba za usajli

shame on you
 
Kwa dharau zako hata tuingie 50 elfu kila game bado sio kitu kwako... Unataka elfu 4/5 za getini ndio ziendeshe timu.. Udhamini una kazi gani sasa??
uta
Shekhe acha ushamba basi ndugu yangu...Mapato yenyewe milioni 300? unajua gharama za kuendesha timu mzee? bajeti ya Klabu yako ya Simba kwa mwaka huu ukitoa pesa za CAF ni Bilioni 6 kama sikosei..Vyanzo vyake kwa mujibu wa mkutano wa juzi ni Mdhamini ambaye ni Sportspes...na mikopo toka kwa watu na taasisi mbali mbali..
Yani hata hiyo get collection imewekwa mwisho kabisa kama vyanzo vya mapato vya klabu..kuiandaa timu hadi unaona wachezaji wanafika uwanjani pale si chini ya Milioni 50 kwa mechi moja kwa mechi za Dar..wewe unaleta hesabu za alinacha hapa..
Tuacheni ushabiki maandazi wazeee..pamoja ni kweli ligi yetu haina kitu wala hailipi kama zingine lakini mashabiki tukiplay part yetu vizuri mbona mamabo yanaenda mzee..tena kwa msimu huu ndio ungekuwa msimu wa kuichangia zaidi timu yetu.
 
Mtazamo / mawazo ya mashabiki sio sheria.. Hapa tunajadili jinsi tunavyoona timu ilivyo na huwezi kutuzuia.
Kujifanya unajua kila kitu na kutulinganisha na ulaya ndio kunakuponza mkuu.
Huko ulaya fans wakimzomea mchezaji na kusema ameshuka kiwango asipangwe au kucheza.. Haitachukua muda lazima ataondoka.. Sasa dharau yako kwa fans ni ipi kama uwanjani tunaingi, kadi tunalipia.
Acha ujiaji hovyo!!
Sijazuia mawazo yetu hewa..ila nazuia kutumia command as if tunachangia saaana klabu yetu kiasi cha kwamba tunahusika moja kwa moja kwenye hata tu kuwalipa posho..maana wewe unachangia kadi je hiyo 12000 unayolipa ndio inamfanya kagere au okwi andelee kusalia na kujituma kwa moyo vile????

ndio maana nikasema mashabiki wa soka Tanzania tujitafakari kama tunatosha kuuashabiki huu mchezo..achilia mbali kutoa tu maoni kama hivi wadau wanavyofanya
 
Zana Colibaly naona siku hizi kazi inayomfaa ni kuzungusha kiuno tu.
 
Hata Manula aondoke aje yule aliyekuwa wa Yanga (jina limenitoka kidogo)
 
Kwa dharau zako hata tuingie 50 elfu kila game bado sio kitu kwako... Unataka elfu 4/5 za getini ndio ziendeshe timu.. Udhamini una kazi gani sasa??
uta
Broo,,hao Sportpesa walikuja Simba na Yanga wakiamini ndio klabu zenye Fans wegi sio..wao waliamini wakidipsly neno Sportpesa popote zilizpo timu hizi watapata kuonekana na kuzidi kunufaika...ndio maana wakakubali kutoa bilioni 1 kila mwaka kwa hizi timu..

Sasa kukusaidia maana inaonekana hujui...Hizo pesa wanazotoa Sportpesa Bilioni 1 hazitoshi Ng'ooo..hazitoshi kabisa maana ukisema timu isikae kambi bado hazitoshi hata kwa mishaara ya wachezaji..maana kama unawachezaji 5 tu unaowalipa milioni 108 kwa mwaka kila mmoja katika hiyo pesa ya sportpesa unabakiwa na kama milioni 300 na kitu hivi..

Kumbuka hapo umelipa wachezaji 5 tuu,,kuna wengine 25 jumlisha timu za vijana achilia mbali makocha maana huko ndio kabisa haitoshi .kwani kocha mkuu peke yake kwa mwaka anaweza kuwa analipwa nusu ya bilioni 1.

Utasema tuna Azam na Mo Energ..Azam kama sitakosea mkataba wao wanatoa nadhami milioni 150 jinsi ilivyotangazwa..jumlsha ile milioni 250 za mo energy unaona milioni 400 kwa mwaka ukijumlisha na Sportpesa unapata 1.4 Blioni..hazitoshii kabisa kwa timu,,ndio maana Bajeti yetu ili timu ijitosheleze kwa msimu ilisomwaga Bilioni 6 nakumbuka.

Nadhani umeona umuhimu hapo wa sisi mashabiki kuichangia timu yetu..kwa kujazana uwanjani kila mechi..maana kama tukilijaza uwanja ,timu haikosi milioni 150 kwa mwezi..ni ndogo nazo lakini kidogo zinapunguza ugumu wa maisha kwenye kuendesha timu.

Kama hujaelewa uliza
 
Mkuu kadi hadi sasa kwa taarifa nilizonazo tunazo watu si chini ya 12000 hadi 15000 hivi...kati ya hao unakuta wanaolipia kadi zao kila mwaka ni watu 500 hadi 1000 unategemea timu itaendelea vipi hapo mzeee???? ok wewe unakadi sawa,,kadi yako mara ya mwisho kulipia ilikuwa lini?kama sio kwenye mkutano wa juzi ???
Wewe sio mpelelezi mkuu hata nkikujibu point yako ishajulikana...
Kama watu 1000/2000 ndio wanalipia kadi kwa mwaka, vipi wanaoingia uwanjani japo game 15 per season?.. Utalinganisha na wanaolipia kadi then uwanjani kuja kwa mbinde?
Cha msingi fans tutambue wajibu wetu... Sio umvae mtu kama anachanga au ana kadi utafikiri unamjua au wewe ni Nyange Kaburu.
 
Naona dalili ya Azam kutuharibia mbio za Ubingwa.
 
Sijazuia mawazo yetu hewa..ila nazuia kutumia command as if tunachangia saaana klabu yetu kiasi cha kwamba tunahusika moja kwa moja kwenye hata tu kuwalipa posho..maana wewe unachangia kadi je hiyo 12000 unayolipa ndio inamfanya kagere au okwi andelee kusalia na kujituma kwa moyo vile????
ndio maana nikasema mashabiki wa soka Tanzania tujitafakari kama tunatosha kuuashabiki huu mchezo..achilia mbali kutoa tu maoni kama hivi wadau wanavyofanya
Timu ni yetu lazima tujadili.. Timu ni watu na watu ndio sisi.
Huyo Kagere anaweza kuja simba bila kuletwa na watu.. kwa hiyo unataka kusema viingilio vya mlangoni havina msaada wowote kwa klabu?.. Sasa mbona unalalamikia uchache wao.
 
Wewe sio mpelelezi mkuu hata nkikujibu point yako ishajulikana...
Kama watu 1000/2000 ndio wanalipia kadi kwa mwaka, vipi wanaoingia uwanjani japo game 15 per season?.. Utalinganisha na wanaolipia kadi then uwanjani kuja kwa mbinde?
Cha msingi fans tutambue wajibu wetu... Sio umvae mtu kama anachanga au ana kadi utafikiri unamjua au wewe ni Nyange Kaburu.
Nasikitika kukuambia kuwa unashindwa kunielewa..lakni pia unashindwa kuelewa maana halisi ya kadi hizi za uawanachama..kwa jinsi navyoelewa hadi kufikia hatua ya kuwa unania ya kupata kadi inamaana uko tayari kwa lolote,,yani unakuwa miongoni mwa jamii husika..

Inapotokea timu inacheza ,,kama kweli wewe ni mwanasimba na unakadi hutaacha kwenda uwanjani kutazama chama lako ..labda uwe unaumwa ama upo nnje ya eneo kikazi..

Tofauti na shabiki..shabiki ni kama wale wanaobishana na kutoa maoni kama hivi tunavyofanya hapa kwamba nani aachwe nani asajiliwe..shabiki yeye kazi yake ni hiyo tu basi,,anaishia kuwaona wachezaji kwenye tv au magazeti,,sasa mtu kama huyu ni sawa na KUPE tu..

Wapo kweli mashabiki wanaojitoa kwa timu..timu hata iende wapi nao wapo ..timu hata iwe mbovu kaisi gani lakini yeye uwanjani lazima awepo ..mtu kama huyu ukichunguza kwa makini anakadi yake ya uanachama na anailipi kila mwaka..ndio maana anaona uchungu...

leo kama ni shabhi hapa utaona kuna wanaojiita mashabiki wa Simba hapa wanasema mtu kama Kotei eti aachwe,,ukimuuliza kwa nini sababu yao etu amechoka...?sasa unajiuliza yeye Kotei asichoke amaekuwa mashine au roboti?hao ndio mashabiki maandazi kazi yao ni kufuata upepo na hawana faida kwenye timu .

hao ni kupiga porojo ambao inatakaiwa ifie mahali mfumo uwateme
 
Timu ni yetu lazima tujadili.. Timu ni watu na watu ndio sisi.
Huyo Kagere anaweza kuja simba bila kuletwa na watu.. kwa hiyo unataka kusema viingilio vya mlangoni havina msaada wowote kwa klabu?.. Sasa mbona unalalamikia uchache wao.
Ndugu jaribu kuelewa Point yangu ya Msingi basi
 
Mzee Mimi sio kama nyie baadhi yenu hapa hata hamuichangii timu yenu..katika orodha ya wanchama 1000 wa kwanza wa SSC Mimi nipo..kadi yangu ya uanachama nalipia kila mwaka ..na sidaiwi mpka miaka mitano mbele...shame on you shabiki maandazi
Unapata wapi huo ujasiri wakusema watu wanao changia kwenye huu uzi hawana kadi! Au una jicho la kiroho. Kwakua hapa hatutumii majina halisi hauna haki ya kutu judge mzee. Unaonekana kama una stress hivi. Acha kujichosha, hatausemeje watu wata toa mawazo yao. Mwingine hana ata buku ya kuchangia ila anaipenda Simba na akiona mchezaji ana zingua atasema tu. Siku akipata atasaidia timu yake. Wewe piga kimya
 
Timu ni yetu lazima tujadili.. Timu ni watu na watu ndio sisi.
Huyo Kagere anaweza kuja simba bila kuletwa na watu.. kwa hiyo unataka kusema viingilio vya mlangoni havina msaada wowote kwa klabu?.. Sasa mbona unalalamikia uchache wao.
fungua akili na unielewe usitake kushupaza shingo itavunjika ndugu...mashabiki wa Tanzania hawana msaada na itaendelea kuamini katika hilo,..haijalishi hata kama watalipa kiingilio cha laki kwa mechi..wengi wetu hatujui kuzipa hamasa timu(hii ni mada nyingine)

Unapaswa ujue faida ambazo klabu inazipata kulingana na mashabiki wake

Moja..kiuchumi- kwa maana hapa mashabiki watalipa viingilio na kununua bidhaa za klabu so klabu itanufaika sana na kuweza kujiendesha..mfano klabu kubwa zinavyofanua huko ulaya..

Pili - Hamasa- klabu inapokuwa na mashabiki wenye hamasa..hata kama hawatalipa viingilio kuingia uwnajani..wakawa wanaingia buree tuu ule uwepo wao tu uwanjani ni hamasa tosha ya kuwafanya wachezaji kujua jukumu lao..na matokeo ya hili ndio timu kushinda mataji mbalimbali ambayo yanathamani kubwa za pesa...

Sasa mashabiki wa Kitanzania huko kote hawapo..hawapo katika mashabiki wenye faida za kuchumi au hamasa...na hapo ndipo tulipokwama..wewe unafikiri ile mechi ya kwanza ya Afcon u 17 kati ya Serengeti na Nigeria uwanja mzima ungekuwa unashangilia Dk zote 90 kwa kupokezana ufikiri kama madogo wangejiona wana deni na wangepambana kulilipa..lakini matokeo yake ikawaje?

Mfano mdogo ni mechi ya Stars dhidi ya Uganda..ile mechi pamoja na kwamba Uganda walikuwa hawana cha kupoteza lakini Uwepo wa nyomi la Mashabiki pamoja na Kelele za Dk 90 uliwafanya Stars wajione wanadeni..deni kubwa katika maisha yao..yani kiuhalisia mioyo yao ilikuwa imejizatiti kufia uwanjani..

sasa aina hiyo ndio tunaikosa ..nina hakika mechi na Mazembe..mashabiki wangefurika,,japo walijitokeza ila hawakufurika uwanja mzima,,kelele za hamasa na amsha amsha zingekuwa nyingi..Mazembe angekufa si chini ya Goli 3 hapa TZ
 
Sijazuia mawazo yetu hewa..ila nazuia kutumia command as if tunachangia saaana klabu yetu kiasi cha kwamba tunahusika moja kwa moja kwenye hata tu kuwalipa posho..maana wewe unachangia kadi je hiyo 12000 unayolipa ndio inamfanya kagere au okwi andelee kusalia na kujituma kwa moyo vile????
ndio maana nikasema mashabiki wa soka Tanzania tujitafakari kama tunatosha kuuashabiki huu mchezo..achilia mbali kutoa tu maoni kama hivi wadau wanavyofanya
Unaposikia Al Ahly ina kikosi cha 80BL ni washabiki ndio wanatoa au udhamini uliopo.
Kumbe timu zetu zipate wadhamini zaidi, kwa vyovyote vile viingilio na kadi ya uanachama haviwezi kukontrol timu.
Ingekuwa hivyo Mo tusingekuwa nae wala Sport Pesa... Sipingi watu kuingia kwa wingi uwanjani ila mtu tu kunizuia kujadili ya timu yangu.
Eti ela yangu haiwezi kumlipa Okwi.. sasa kila fans akiwa na uwezo huo utakuwa sio mpira sasa.
 
Mkuu pia ukumbuke Simba ndio inaongoza kuingiza mapato ya mlangoni toka msimu jana, na huu itaongoza pia.
Halafu sio lazima kila mechi tujae uwanjani kama Ulaya.. hapa ni bongo hatujafika level ya Ulaya.
Na kwa Africa tumeongoza ata mashabiki wa Mazembe na Mamelodi wakasome.
 
Back
Top Bottom