Huu ni msimu wa 3 sijawahi kukosa mechi yoyote ya Yanga ya kimataifa hapa nyumbani ila hii sitoenda, uamuzi wa kumfuta kazi Gamondi umenikera sana.
Timu ikishinda sawa, isiposhinda sawa pia.
Binafsi naweza nikawa natofautiana na wewe au na wengi ambao mnaona kufukuzwa kwa Gamondi haikuwa jambo sahihi.
Mimi naona viongozi wamefanya jambo sahihi sana na wasingefanya hivyo, kuna uwezekano wa kupoteza tena mechi inafuata.
Mazingira ya kocha kufanya vizuri ndani ya uwanja hutokana na muunganiko kati ya wachezaji, benchi la ufundi lenyewe na viongozi. Wachezaji hujituma kwaajili ya timu na pia kufuata maelezo ya kocha wao.
Graph ya performance ya Yanga ilikuwa inashuka kadri siku zinavyozidi kwenda, mashabiki wakaona ni kwavile timu zinaikamia Yanga ndio sababu ya mechi za Yanga kuwa ugumu lakini hapo hapo hatujiulizi mbona msimu uliopita timu zilikuja kwa kuikamia Yanga lakini walikuwa wanakula vichapo vya maana kama wataruhusu goli ndani ya kipindi cha kwanza, ila msimu huu ile timu ikipata goli dakika za mapema unaomba mpira uishe maana hakuna jitihada za kutaka magoli mengi zaidi ya Yanga kukoswa koswa wao. Yanga ikicheza na timu pungufu bado unaona magoli machache.
Kuna mambo kadhaa ambayo pengine ndiyo kiini cha kushuka timu, mojawapo inaweza kuwa wachezaji wameamua kumtoa kutokana na mambo yao ya nje ya uwanja ( ubaguzi wa wachezaji, ujeuri, nk)
Wachezaji kama hawamtaki kocha hapo hakuna namna unaweza fanya ukairudisha timu katika hali ya kawaida.
Jambo lingine nililoiona kwa upande wangu ni starehe kwa kocha na wachezaji wake na hii yote imetokana na kusifiwa kupita kiasi hivyo kocha na wachezaji wakabweteka, je kama kocha yupo hivyo ni nani wa kusimamia nidhamu ya wachezaji?
Hakuna kitu huwa kinauzi kama kumuona Azizi Ki akiendelea kupoteza mipira ovyo huku benchi kuna watu wa maana wanaoweza kuchukua nafasi yake, wachezaji wengi wanapoteza ubora wao kisa tu yeye kukariri watu wale wale kucheza. Abuya ni usajili mzuri sana msimu huu ila apewi nafasi. Mkude aliyeonekana lulu mbele ya Mamelodi leo hii sijui yuko wapi. Kibwana Shomari anaonekana ni mzigo ndani ya Yanga kiasi kwamba hana uwezo wa kucheza hata kwenye mechi dhidi ya mid table team.
Nilimkubali sana Gamondi ila msimu huu niliambulia performance nzuri ya timu ni kwenye mechi za pre season tu hasa dhidi ya wale wajerumani.