Wanaccm wenzangu tambueni takwa la katiba Sio la CHADEMA ni la wananchi na wenye nchi ambao hata Mwenyekiti anawajibika kwao

Wanaccm wenzangu tambueni takwa la katiba Sio la CHADEMA ni la wananchi na wenye nchi ambao hata Mwenyekiti anawajibika kwao

Makomredi
Tusipoteze muda kwa kupiga sarakasi na kufanya uharamia kwa vyama vya siasa vya upinzani nchini.

Tutambue takwa la katiba ni la wananchi na wenye nchi ambao Mwenyekiti wetu anawajibika kwao.

Tumshauri aachane na sarakasi za kuzuia mchakato huo kwa visingizio visivyo na mashiko mwambieni akubali asibishane na wakati.

Hata mzee Warioba ni mwanaccm na anajua wakati ni Sasa na huyo mzee hamzidi uzoefu wa kuwa mwanachama wa ccm ni mkongwe ndani ya chama ashirikiane nae Ili mchakato uanze sasa.

Ujanja ujanja wake utamkosanisha na wananchi na Wenye NCHI na kupoteza vingi!akubaliane na ukweli kuwa katiba Sio dudu linalo uma ni kitabu cha thamani KWA wananchi.

Sarakasi na uharamia havitomsaidia wala kisaidia chama zaidi ya kukiaibisha chama na Serikali.

Naamini katibu,makamu na mwenezi wa chama mtamfikia Mwenyekiti na kumwambia Mama wakati ni sasa!
Asanteni
Aiseeee !!!
 
we kijana unabii uliupatia wapi ?
Katiba mpya ni agizo la Dola Sio matakwa ya mbowe na CHADEMA! Mbowe na CHADEMA wanatumiwa na Dola kufanikisha Hilo!!
Sasa wahuni ndani ya ccm walidhani wanaweza ku twist mchakato!
Nikawaonya wakaonyeka Sasa wametubu na kurudi Relini!!
 
Unaonyesha unaakili ndogo sana hao wananchi 50milioni wanaamuaje bila political will ya wenye mamlaka? Ukitaka wananchi waamue bila mamlaka kuongoza mchakato ndio haya yanayoleta fujo kwenye nchi nyie ndio UVCCM mnaorukaruka mwendo wa mnyakuo huku akili ziro kabisa nakwambia bila utashi wa kisiasa wa wenye mamlaka hiki unachokisema hapa ni fujo! Ikiwa wanachama wa chadema wasiozidi 20 milioni mnawakataza wasifanye mihadhara ya wazi je hawa wananchi 50 milioni unataka wakutane wapi kuamua mustakabali wa katiba yao?
uoga wako ni furaha ya CCM...

hao unao waita wana siasa, katiba imetamka wazi kuwa madaraka wana yapata kutoka kwa wananchi... yani madaraka waliyo nayo ni wenye nchi (wananchi) wameamua...

akili zako kubwa lakini ni bure
 
Back
Top Bottom