Tindo
JF-Expert Member
- Sep 28, 2011
- 63,730
- 111,542
Naona unajifunza propaganda lakini ni kama unapishana na beat. Kwa taarifa yako kama kuombea watoto wao ulaya, viongozi wa CCM ndio wanaoongoza, na bado wanaiba chaguzi waendelee kukaa madarakani.Tanzania bado kuna safari ndefu ya kupata upinzani wa kweli. Maana waliopo sasa wanapigania matumbo yao na ya familia zao, tena siku hizi wanaonesha dhahiri kwa kwenda ikulu kila mara kulamba asali, mara kusema bila aibu tena kwa kujiamini kuwa washawakimbizia watoto wao Marekani wakaombe uraia wa huko huku wakiwahadaa watoto wa maskini kuwa wanawapambania.
Yani upuuzi mtupu.
Kaangalie maisha mfano ya watoto wa Mwigulu, na ya watoto wa watanzania wengine anaosema anawapigania. Akina Kikwete Kawa rais ana kila kitu, lakini mke na mtoto wake wako bungeni, tena kwa kura za wizi. Kwanini wasiwaachie hizo nafasi watanzania wengine wanyonge nao waonje cake ya taifa? Katika mazingira hayo ni kwanini usipeleke watoto wako ulaya, kuliko kugeuka mashahidi wa cake ya taifa kutafunwa na watu wale wale?