WanaCHADEMA tukubali kukosoana. Kama pesa zinatafunwa tuseme ukweli sio kutimuana

Shida sio kutafunwa fedha, shida ni umuhimu wake kwenye chama. Hizo ni allegations tu ambazo yeyote anaweza toa. Yeye sio wa kwanza, ila chama kingeangalia uzito wa kosa na umuhimu wa mwanachama. Wangempa hata onyo la mwisho au karipio au wangempa ushauri wa kuleta ushahidi wa hicho kilichosemwa.

All in all CHADEMA bado kina watu wengi wanaojulikana na wasio julikana.
 
Dah! Hiki ndio chama kinachoamini siku moja kitachukua jukumu la kuendeaha Serikali ya nchi hii? Siamini!!
Wewe ndo umeanza kukijua leo? Mwenyekiti na genge lake walivyovuta mpunga ili wamsafishe Lowasa na kumpa ticket ya kugombea uraisi ulikuwa wapi?

Mamilioni ya Sabodo aliyotoa yajenge ofisi kuu ya chama yakatafunwa wew ulikuwa wapi? Mwenyekiti anapokwenda ikulu kulamba asali kimya kimya bila kuwashirikisha viongozi wenzake wewe uko wapi?

Mimi nilikuwa chadema damu, lakini upuuzi walioufanya mwaka 2015 na kukaa mpaka leo bila kutuomba wananchi msamaha kwa upuuzi ule, imenifanya na mimi niwapuuze viongozi wote wa upinzani na siasa zao uchwara.

Kwa sasa mtu hanidanganyi maana uchaguzi wa 2015 umenisaidia kujua mbivu na mbichi. Nani mpinzani nani sio mpinzani.
Screenshot_20220912-125326.jpg
images (1).jpeg
download.jpeg
 
Dah! Hiki ndio chama kinachoamini siku moja kitachukua jukumu la kuendeaha Serikali ya nchi hii? Siamini!!

Chama pia kina mambo yake ya ndani. Kuchukua dola haizuii kupishana kauli ndani ya chama. Mbona CCM juzi tu hapa walimsimamisha uanavhama kinana. Na Leo ndio Makamu Mwenyekiti. Haya mambo yapo.
 
Cc

CCM ilimsimamisha haikumfukuza. Nadhani ni misamiati miwili tofauti yenye maana mbili tofauti.
 
Mimi nilikuwa Chadema damu, nilipambana kukitangaza chama mpaka huku nilipo. Ila ushenzi uliofanyika mwaka 2015 umenifunza mengi. Sasa najua mbivu na mbichi, nani mpinzani wa kweli na nani sio wa kweli.
Tusamehe bas brother....japo tutiane moyo tu jaman...huenda kuna siku tukafanikiwa.But why Tanzania...democracy iko wapi?
 
Tanzania bado kuna safari ndefu ya kupata upinzani wa kweli. Maana waliopo sasa wanapigania matumbo yao na ya familia zao, tena siku hizi wanaonesha dhahiri kwa kwenda ikulu kila mara kulamba asali, mara kusema bila aibu tena kwa kujiamini kuwa washawakimbizia watoto wao Marekani wakaombe uraia wa huko huku wakiwahadaa watoto wa maskini kuwa wanawapambania.
Yani upuuzi mtupu.

Hayo matumbo yao wanayapigania wapi?
Mbona hukusikitika Mbowe alipofanyiwa dhihaka na mkuu wa Wilaya anayeitwa Byakanwa au mbona hukuona huruma Mbowe alipovunjiwa bilcanas, kufukuzwa kwenye jengo la NHC na kufungiwa akaunti zake zote na kesi ya ugaidi juu?

Au mbona hukusikitiaka msadizi wa Mbowe Saanane alipopotezwa mpaka leo? Au Lissu kumiminiwa risasi na uchunguzi kutofanyika mpka leo?.

Unapolaumu angalia situation ilivyo. CHADEMA wamekatazwa kufanya siasa miaka Saba Sasa. Unasemaje hakuna upinzani?

Unapolaumu tu bila kuangalia Mazingira unakua bias.
 
Wewe ndo umeanza kukijua leo? Mwenyekiti na genge lake walivyovuta mpunga ili wamsafishe Lowasa na kumpa ticket ya kugombea uraisi ulikuwa wapi?

Mamilioni ya Sabodo aliyotoa yajenge ofisi kuu ya chama yakatafunwa wew ulikuwa wapi? Mwenyekiti anapokwenda ikulu kulamba asali kimya kimya bila kuwashirikisha viongozi wenzake wewe uko wapi?

Mimi nilikuwa chadema damu, lakini upuuzi walioufanya mwaka 2015 na kukaa mpaka leo bila kutuomba wananchi msamaha kwa upuuzi ule, imenifanya na mimi niwapuuze viongozi wote wa upinzani na siasa zao uchwara.

Kwa sasa mtu hanidanganyi maana uchaguzi wa 2015 umenisaidia kujua mbivu na mbichi. Nani mpinzani nani sio mpinzani.

Naomba nikuulize, walivuta shilingi ngapi kutoka kwa Lowassa?.
 
Mimi nilikuwa Chadema damu, nilipambana kukitangaza chama mpaka huku nilipo. Ila ushenzi uliofanyika mwaka 2015 umenifunza mengi. Sasa najua mbivu na mbichi, nani mpinzani wa kweli na nani sio wa kweli.

Rudi kwenye chama tu mkuu, samehe. Viongozi hubadilika ila chama hubaki. Hata Mimi sikukubali Lowassa kuja CHADEMA, lakini CHADEMA ni Chama changu siwezi kuhama nimebaki mpka Lowassa kaondoka katuacha kwenye chama tunapambana. Karibu sana.
 
Tusamehe bas brother....japo tutiane moyo tu jaman...huenda kuna siku tukafanikiwa.But why Tanzania...democracy iko wapi?
Tatizo mifumo yote ya vyama vya siasa iko chini ya wale jamaa wa usalama wetu (bila shaka unawajua) wao ndio humuweka kiongozi wa chama kupitia chaguzi mbali mbali za chama.

Sasa wanapoona kuna chama kinaonekana kuwa tishio kwa chama tawala na kina mpango wa kushika dola basi hutafutwa njia ya kukifubaza chama husika kupitia kwa mawakala wao ambao ndio viongozi wa juu wa vyama hivyo na matokeo yake kufifisha juhudi na jitihada za kukiondoa chama tawala madarakani.

Kwangu mimi namuona Lisu kuwa ni mpinzani madhubuti ndo maana yalimpata yaliompata. Hawa wengine wote na kesi zao za kutengenezwa na kutufubaza tu wananchi wakidhani kila mtu ni bogas wa kuamini kila anachoambiwa.
 
Cc

CCM ilimsimamisha haikumfukuza. Nadhani ni misamiati miwili tofauti yenye maana mbili tofauti.

Sawa ilimsimamisha ambayo kwa kiingereza ni suspension. Sasa hujiulizi inakuwaje mtu aliyesimamishwa uanachama kwa kumsema Mwenyekiti, leo ni makamu mwenyekiti.?. Hata Dr Albanie anaweza samehewa na Kuna kuwa Katibu Mkuu wa chama.
 
Tatizo mifumo yote ya vyama vya siasa iko chini ya wale jamaa wa usalama wetu (bila shaka unawajua) wao ndio humuweka kiongozi wa chama kupitia chaguzi mbali mbali za chama.

Sasa wanapoona kuna chama kinaonekana kuwa tishio kwa chama tawala na kina mpango wa kushika dola basi hutafutwa njia ya kukifubaza chama husika kupitia kwa mawakala wao ambao ndio viongozi wa juu wa vyama hivyo na matokeo yake kufifisha juhudi na jitihada za kukiondoa chama tawala madarakani.
So sad
 
Rudi kwenye chama tu mkuu, samehe. Viongozi hubadilika ila chama hubaki. Hata Mimi sikukubali Lowassa kuja CHADEMA, lakini CHADEMA ni Chama changu siwezi kuhama nimebaki mpka Lowassa kaondoka katuacha kwenye chama tunapambana. Karibu sana.
Mimi namkubali sana Lisu, yule jamaa japo alikuwa miongoni mwa waliomeza matapishi yao kipindi kile, lakini bado anaonesha misimamo ya kichama mara kwa mara.

Ila bwana mkubwa yeye ni kukipeleka peleka tu chama kama gari bovu.
 
Wewe mwenyewe ni zaidi ya gari bovu
 
Naomba nikuulize , walivuta shilingi ngapi kutoka kwa Lowassa?.
Mkuu hata haya aliyoongea huyu kamanda kama asingeongea usingeyajua.
Kikubwa ujue tu kwamba wanasiasa wa Tanzania iwe wa upinzani au wa tawala wote wapo kwa ajili ya kupigania matumbo yao na ya familia zao.

Usiache kufanya shughuli zako za kujitafutia riziki eti ukiamini kuwa mwanasiasa fulan akishika dola maisha yangu yatakuwa mazuri, Never hakuna kitu kama hicho labda kwa wanasiasa wa nchi zingine ila sio Tanzania. Watanzania sasa tunajuana.
 
Tukimpoteza huyu, sijui. Huyu pamoja na bananga na Amani Golugwa ndio walikuwa washauri wa Lissu kwenye kampeni za 2020. Na walitembea naye kampeni nzima. Hebu tupime kosa na umuhimu wa Dr Albanie tufanye maamuzi sahihi.

Taarifa zitafika tu kwa Viongozi wa juu.

Hata mimi niliona huko twitter account ya mtu anayejiita Marcos Albanie akiseme amefukuzwa CDM kwa kuhoji matumizi ya fedha. Nilipuuza maana baada ya kufuatilia post zake nyingine niliona akitoa hoja nyepesi na nyingine sio za hadhi yake. Nikahisi ni parody tu linalojifanya ni Marcos Albanie. Kwangu Marcos Albanie alipaswa kuwa katibu Mkuu wa CDM mara baada ya kutoka Dr. Slaa na sio Mashinji. Je taarifa hizi ni kweli?

Hata hivyo bila kujali ukweli wa taarifa hii, mimi nimekuwa nikisema Mbowe hastahili tena kuwa mwenyekiti wa CDM, na hili nililisema mara baada ya kumpokea Lowassa. Na sasa nazidi kusisitiza kuwa Mbowe sio kiongozi sahihi tena wa CDM. Ni juu ya wanachama wa CDM kumkataa hadharani maana anakipotezea chama brand yake, kisha anajifichia kwenye maridhiano ya kitapeli. Inshort Mbowe kashafikia mwisho.
 
Mkuu hata haya aliyoongea huyu kamanda kama asingeongea usingeyajua.
Kikubwa ujue tu kwamba wanasiasa wa Tanzania iwe wa upinzani au wa tawala wote wapo kwa ajili ya kupigania matumbo yao na ya familia zao.

Usiache kufanya shughuli zako za kujitafutia riziki eti ukiamini kuwa mwanasiasa fulan akishika dola maisha yangu yatakuwa mazuri, Never hakuna kitu kama hicho labda kwa wanasiasa wa nchi zingine ila sio Tanzania. Watanzania sasa tunajuana.

Ila viongozi wa CCM wakikaa madarakani ndio utafaidi.
 
Back
Top Bottom