WanaCHADEMA tukubali kukosoana. Kama pesa zinatafunwa tuseme ukweli sio kutimuana

Naona unajifunza propaganda lakini ni kama unapishana na beat. Kwa taarifa yako kama kuombea watoto wao ulaya, viongozi wa CCM ndio wanaoongoza, na bado wanaiba chaguzi waendelee kukaa madarakani.

Kaangalie maisha mfano ya watoto wa Mwigulu, na ya watoto wa watanzania wengine anaosema anawapigania. Akina Kikwete Kawa rais ana kila kitu, lakini mke na mtoto wake wako bungeni, tena kwa kura za wizi. Kwanini wasiwaachie hizo nafasi watanzania wengine wanyonge nao waonje cake ya taifa? Katika mazingira hayo ni kwanini usipeleke watoto wako ulaya, kuliko kugeuka mashahidi wa cake ya taifa kutafunwa na watu wale wale?
 
Kwahiyo lengo la kuanzisha vyama vya upinzani ni kufanya yale yale yanayofanywa na chama tawala au sio?
Kwamba kwa vile Kikwete ana watoto nje basi na Mbowe au Zito na wao wawe na watoto nje?

Wapinzani kufanya makosa yanayofanywa na viongozi wa chama tawala sio ukombozi bali ni kuendeleza ukiritimba wa miaka na miaka.
Kwa lugha nyingine hakuna viongozi mbadala wa kujitofautisha na hawa waliopo madarakani. Wote ni wale wale tu wanawachora wadanganyika kupitia siasa uchwara zisizokuwa na kichwa wala miguu.
 

Ni kweli amefukuzwa mkuu. Lakini kwenye ngazi ya Wilaya. So bado anaweza kukata rufaa. Ila yeye amedai kuwa ni mwanchama wa CHADEMA. Amehaidi kutoa press conference.

Huyu anafaa Sana kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ana misimamo na elimu kubwa .

Kuhusu Mbowe Ni vizuri akaondoka kwa amani maana majembe ni mengi ya kushika nafasi hiyo. Heshima yake itabaki na ataendelea kuwa mshauri wa chama.
 
Nikisema mimi inakuwa kosa. Sema wewe sasa
 

Uivyoongea kuhusu watoto wa Lisu kwenda US ni kama kufanya propaganda chafu, bila kujua hiyo hali ni ya kawaida sana huko CCM. Kwa taarifa yako kila mtu anaweza kupeleka familia yako kokote atakako dunia hii ili mradi havunji sheria. Labda useme ni sheria gani Lisu amevunja kwa watoto wake kwenye Amerika.
 
Mimi nilikuwa chadema damu, lakini upuuzi walioufanya mwaka 2015 na kukaa mpaka leo bila kutuomba wananchi msamaha kwa upuuzi ule, imenifanya na mimi niwapuuze viongozi wote wa upinzani na siasa zao uchwara.
Hauko peke yako mkuu, hata mimi toka 2015 niliamua kujiweka kando na chadema baada ya upuuzi ule. Ulikuwa ni unafiki wa kiwango cha juu sana.
 

Ngoja tusubiri press conference yake. Mbowe yeye kwa sasa kafikia mwisho. Hapo alipo hana jipya zaidi ya kuharibu haiba ya CDM. Ashauriwe akae pembeni haraka iwezekanavyo.
 
Viongozi wa CHADEMA wameshakuwa CORRUPTED..lobbied.. hamna kitu tena humo..
 
Kuongea ukweli kuhusu utafunwaji wa fedha za chama. Huko mwenyekiti na genge lake wakitafuna fedha za chama hautakiwi kuuliza wala kuhoji utafunwaji huo.
Chadema ina ela gani?? We umekichangia shs ngapi?? Ebu hacha porojo zako za kijinga
 
Nadhani wata solve hili tatizo, maana lipo ngazi ya Chini. Hilo sio kosa la kufukuzwa chamani. Tafadhali, huyu mtu wa muhimu Sana. Very intelligent tusimpoteze.
Hana umuhimu wowote, hawa ni mamruki toka ccm
 
Aliyepo kwa sasa je

Aliyepo kwa Sasa yupo vizuri, lakini tunahitaji new strategies and ideologies za kupambana na mfumo wa CCM . Sio huu wa maridhiano ya Ikulu ya CCM.
 
Hana umuhimu wowote, hawa ni mamruki toka ccm

Sidhani, huyo siyo mamluki wa CCM . Mamluki wote waliondoka kipindi Cha Magufulii. Ila huyu ndio alikuwa campaign adviser wa Lissu 2020 .kumbuka pia aligombea ubunge mwaka 2015 Morogoro mjini.
 
Ngoja tusubiri press conference yake. Mbowe yeye kwa sasa kafikia mwisho. Hapo alipo hana jipya zaidi ya kuharibu haiba ya CDM. Ashauriwe akae pembeni haraka iwezekanavyo.

Mbowe akilazimisha kugombea Tena Kuna kitu kitapungua CHADEMA. Lakini akistaafu na kumwachia Heche au Lissu Kuna kitu kipya kitaongezeka CHADEMA. Nadhani ashauriwe mapema.
 
Chadema ina ela gani?? We umekichangia shs ngapi?? Ebu hacha porojo zako za kijinga

Safi Sana. Hao wanaongea tu bila kujua lolote. Chama kwa Sasa kinaendeshwa kwa kujitolea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…