Nimesukumwa kuanzisha uzi huu ili tuweze kuwajua wenzetu waliotangulia/wanaotangulia mbele za haki kwa wale mnaofahamiana. Marehemu walikuwa kama sisi tu humu,wakielimisha,kuburudisha n.k lakini kwa sasa wamerudi mavumbini. Bahati mbaya wengine hatufahamiani kabisa physically,binafsi sina ninayemjua humu hivyo hata nikifa sio rahisi kupata habari zangu hivyo likitokea tutakutana Mbinguni kwa Baba.
Hivyo kwa wale mmnaojuana,ni vema mkawa mnatupa taarifa ili tuweze kuwaombea wenzetu katika sala zetu za kila siku. Mpaka sasa,kwa kumbukumbu zangu inaonyesha wanaJF wafuatao wameishafariki kadiri ya habari zinavyoripotiwa humu😔
1.Fasi Dwasi
2.Dena Amsi
3.Straton Mushi
4.Kennedy Lufulondama
Najua kuna wengine zaidi,tujuze humu...Mungu awalaze mahali pema peponi...Amina