Mimi huwa namkumbuka sana yule mwenzetu aliyejiita Mpenzi wa Islam. Huyu alinigusa sana kwa jinsi alivyokuwa mpole na kutumia lugha ya kistaarabu katika majadiliano katika jukwaa la dini. Pamoja na baadhi ya wachangiaji walikuwa wakitumia matusi na kashfa nzito nzito dhidi ya dini ya Kiislam, Mpenzi wa Islam hata siku moja hakukashifu, kumtukana mtu/dini au kutumia lugha ambazo si za kistaarabu bali alijibu kwa kujaribu kuwaelewesha wachangiaji hao. Nilipenda sana kusoma michango yake na hadi nikamuomba urafiki hapa jamvini. Nilipenda sana kukutana naye na tayari nilishapanga kumtafuta pindi nafasi ingeruhusu lakini kabla ya kufanikiwa kufanya hivyo akafariki. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu na wengine wote waliowahi kuwa wanachama wa jamvi hili mahali pema peponi~AMEN.