PreGE2025 Wanachama wengine wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu wa G55 Edward Kinabo watangaza kujivua Uanachama

PreGE2025 Wanachama wengine wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu wa G55 Edward Kinabo watangaza kujivua Uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

Platinum Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
3,054
Reaction score
8,449
Wakuu,

Mambo yanazidi kuchangamka huko, mvua inayesha tunaona panapovuja. Tusibiri saa tano kamili tuone kitakachojiri.


View: https://www.youtube.com/live/0O9B4aH_fag?si=gZorh7bK6lTU3LTJ

kada chadema.jpg

​

Edward Kinabo - Aliyekuwa Mratibu wa Habari na Mawasiliano wa kampeni za Freeman Mbowe
​
"Kauli zilizotolewa jana na Makamu Mwenyekiti John Heche, Mheshimiwa Heche alisema uongo kwa kusema kwamba eti viongozi wa Sekretariati waliojivua uanachama, kwamba hawajawahi kuchaguliwa katika nafasi yoyote ndani ya chama hichi. Mheshimiwa Heche alienda mbali na kujisifia kuwa yeye alichaguliwa na alianza kuwa diwani lakini waliozungumza juzi hata mmoja hawakuwahi kuaminiwa wala kuchaguliwa.

Huo ni uongo mkubwa sana wa Makamu Mwenyekiti kwa lengo tu la kueneza chuki na mpasuko na dharau dhidi ya kundi ambalo lilikuwa linampinga katika Uchaguzi

Mimi ambaye pia nilikuwa ni mgombea Urais wa CHADEMA kwenye jimbo la Kibaha Vijijini kwenye Uchaguzi wa 2020 napenda kutangaza rasmi kwamba nimeamua kwa uamuzi wangu mwenyewe kujivua uanachama wa CHADEMA kuanzia leo"

"Watu wote tuliomuunga mkono Mheshimiwa Mbowe ndani ya CHADEMA hatuna chetu tena. Tunanyanyaswa, tunabaguliwa, tunazushiwa uongo, tunaitwa wasaliti, tunaitwa waasi, kanda zimegawanyika, mikoa imegawanyika, kata zimegawanyika, hakuna chama tena hapa"

Elia Evarist - Kada wa CHADEMA, Mjumbe Mkutano Mkuu CHADEMA Temeke

"Ndani ya CHADEMA sasa hivi ukihoji unapewa mateso na mabezo, viongozi wakuu wanaona tunavyotukanwa na anavyotukanwa Mwenyekiti mstaafu Mbowe na nimeshangaa jana kuona Katibu Mkuu wa chama anatweet ambayo tafsiri yake inalenga kupoza joto hili na sio vingine"

"Kauli yake ni kinafiki kwa sababu kama angekuwa yuko fair angeweza kuwa ameshatoa tamko mapema sana la kulaani na kupinga matusi anayotukanwa Mwenyekiti mstaafu"

"Nachukua nafasi hii kuwaambiwa wananchi wa Tanzania, ninaona CHADEMA kwa sasa sio jukwaa salama na rafiki kwa kuweza kunifanya mimi kuendelea kupigania haki yao, sio jukwaa sahihi kabisa. Ninauvua Uanachama wa CHADEMA na nafasi zangu zote nilizokuwa nazo na roho inaniuma sana kuondoka lakini no way out"
 
Leave CDM alone, hii inaweza kuifanya CDM kuwa strong zaidi.

Wangekuwa waelevu wenye uelewa, tulipaswa kuwaona wakiendelea kussuport CDM iwe strong zaidi na sio kulazimisha wanachoamini wao basi ndio kifanye kazi, Mbona Lissu na Heche hawakumlazimisha MBOWE kuziishi fikra zao?.
 
Wale waliotimka juzi wala hawana athari hasi yoyote waliyoiacha kwenye chama kwa maana chama kimekuwa na nguvu ya wananchi badala ya viongozi kitu ambacho ni kizuri.

Ukiona mtu amehama chama halafu chama kikatetereka basi fahamu kwamba mtu huyo ni mkubwa kuliko chama.

Lakini akihama mtu ama kundi la watu na bado chama kikabaki imara basi hiyo ni dalili tosha kwamba nguvu ya chama inatokana na wananchi.
 
Hao wanao fanya conference saa tano nasikia wote walishapewa barua za kujieleza kuhusu tuhuma walizokuwa wanahusishwa nazo.

Wameamua tu kujitoa kwa kukwepa fedheha lakini kiukweli watu wengi tunajua hao ni Wachumia tumbo tu.
 
Wale waliotimka juzi wala hawana athari hasi yoyote waliyoiacha kwenye chama kwa maana chama kimekuwa na nguvu ya wananchi badala ya viongozi kitu ambacho ni kizuri.

Ukiona mtu amehama chama halafu chama kikatetereka basi fahamu kwamba mtu huyo ni mkubwa kuliko chama.

Lakini akihama mtu ama kundi la watu na bado chama kikabaki imara basi hiyo ni dalili tosha kwamba nguvu ya chama inatokana na wananchi.
Kwa kua hamtashiriki Uchaguzi subirini ruzuku ikate, ndipo mtakapojua ukubwa wa Chadema au kulishana upepo tu.
Wachagga na Wameru ndio wanaofix Finance Gap la Chama kujalizia ruzuku.
Nyaturu, Gita , Sukuma na Nyakyusa ni kelele tu.
 
Kwa kua hamtashiriki Uchaguzi subirini ruzuku ikate, ndipo mtakapojua ukubwa wa Chadema au kulishana upepo tu.
Wachagga na Wameru ndio wanaofix Finance Gap la Chama kujalizia ruzuku.
Nyaturu, Gita , Sukuma na Nyakyusa ni kelele tu.
Hoja mfu kabisa.

Wapo watu wako tayari ku finance chama hata ruzuku isipokuwepo.

Waliokuwa wanategemea ruzuku ndiyo hao wameanza kuchanja mbuga wenyewe ili chama kibaki na watu safi.

Mimi sio mfuasi wa vyama vyenu ila inapotokea jambo la kuzungumza ukweli basi huwa nasema kwasababu binadam wote tunastahili haki na uhuru sawa bila upendeleo.
 
Watu wako kwenye chama zaidi ya miaka 20, waje kuwa mamluki ndani ya uongozi wa miezi 6 ya Lissu?!!
Hiyo miaka unayosema walikuwepo ni kwasababu walipewa mirija ya kufyonza ruzuku bila jasho.

Sasa wamekuja watu wa kazi wasiotanguliza tamaa ya fedha wanataka kuimarisha chama ndiyo unaona nguchiro sasa wanatoka mashimoni kwasababu hakuna mirija tena ya bure bure.
 
Back
Top Bottom