Wakuu,
Mambo yanazidi kuchangamka huko, mvua inayesha tunaona panapovuja. Tusibiri saa tano kamili tuone kitakachojiri.
Edward Kinabo - Aliyekuwa Mratibu wa Habari na Mawasiliano wa kampeni za Freeman Mbowe
"Kauli zilizotolewa jana na Makamu Mwenyekiti John Heche, Mheshimiwa Heche alisema uongo kwa kusema kwamba eti viongozi wa Sekretariati waliojivua uanachama, kwamba hawajawahi kuchaguliwa katika nafasi yoyote ndani ya chama hichi. Mheshimiwa Heche alienda mbali na kujisifia kuwa yeye alichaguliwa na alianza kuwa diwani lakini waliozungumza juzi hata mmoja hawakuwahi kuaminiwa wala kuchaguliwa.
Huo ni uongo mkubwa sana wa Makamu Mwenyekiti kwa lengo tu la kueneza chuki na mpasuko na dharau dhidi ya kundi ambalo lilikuwa linampinga katika Uchaguzi
Mimi ambaye pia nilikuwa ni mgombea Urais wa CHADEMA kwenye jimbo la Kibaha Vijijini kwenye Uchaguzi wa 2020 napenda kutangaza rasmi kwamba nimeamua kwa uamuzi wangu mwenyewe kujivua uanachama wa CHADEMA kuanzia leo"
"Watu wote tuliomuunga mkono Mheshimiwa Mbowe ndani ya CHADEMA hatuna chetu tena. Tunanyanyaswa, tunabaguliwa, tunazushiwa uongo, tunaitwa wasaliti, tunaitwa waasi, kanda zimegawanyika, mikoa imegawanyika, kata zimegawanyika, hakuna chama tena hapa"
HIVI MHESHIMIWA SUGU MBONA HASIKIKI AU NAYE TAYARI KISHAJIONDOA CHADEMA? YAANI HATA KUMTAFUTA MDUDE HAANGAIKI YUPO KIMYA