PreGE2025 Wanachama wengine wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu wa G55 Edward Kinabo watangaza kujivua Uanachama

PreGE2025 Wanachama wengine wa CHADEMA wakiongozwa na Katibu wa G55 Edward Kinabo watangaza kujivua Uanachama

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
"Watu wote tuliomuunga mkono Mheshimiwa Mbowe ndani ya CHADEMA hatuna chetu tena. Tunanyanyaswa, tunabaguliwa, tunazushiwa uongo, tunaitwa wasaliti, tunaitwa waasi, kanda zimegawanyika, mikoa imegawanyika, kata zimegawanyika, hakuna chama tena hapa"
Waende kwa Amani! CHADEMA ni imani Sio VIONGOZI
 
Wakuu,

Mambo yanazidi kuchangamka huko, mvua inayesha tunaona panapovuja. Tusibiri saa tano kamili tuone kitakachojiri.


Edward Kinabo - Aliyekuwa Mratibu wa Habari na Mawasiliano wa kampeni za Freeman Mbowe
​
"Kauli zilizotolewa jana na Makamu Mwenyekiti John Heche, Mheshimiwa Heche alisema uongo kwa kusema kwamba eti viongozi wa Sekretariati waliojivua uanachama, kwamba hawajawahi kuchaguliwa katika nafasi yoyote ndani ya chama hichi. Mheshimiwa Heche alienda mbali na kujisifia kuwa yeye alichaguliwa na alianza kuwa diwani lakini waliozungumza juzi hata mmoja hawakuwahi kuaminiwa wala kuchaguliwa.

Huo ni uongo mkubwa sana wa Makamu Mwenyekiti kwa lengo tu la kueneza chuki na mpasuko na dharau dhidi ya kundi ambalo lilikuwa linampinga katika Uchaguzi

Mimi ambaye pia nilikuwa ni mgombea Urais wa CHADEMA kwenye jimbo la Kibaha Vijijini kwenye Uchaguzi wa 2020 napenda kutangaza rasmi kwamba nimeamua kwa uamuzi wangu mwenyewe kujivua uanachama wa CHADEMA kuanzia leo"

"Watu wote tuliomuunga mkono Mheshimiwa Mbowe ndani ya CHADEMA hatuna chetu tena. Tunanyanyaswa, tunabaguliwa, tunazushiwa uongo, tunaitwa wasaliti, tunaitwa waasi, kanda zimegawanyika, mikoa imegawanyika, kata zimegawanyika, hakuna chama tena hapa"

Elia Evarist - Kada wa CHADEMA, Mjumbe Mkutano Mkuu CHADEMA Temeke

"Ndani ya CHADEMA sasa hivi ukihoji unapewa mateso na mabezo, viongozi wakuu wanaona tunavyotukanwa na anavyotukanwa Mwenyekiti mstaafu Mbowe na nimeshangaa jana kuona Katibu Mkuu wa chama anatweet ambayo tafsiri yake inalenga kupoza joto hili na sio vingine"

"Kauli yake ni kinafiki kwa sababu kama angekuwa yuko fair angeweza kuwa ameshatoa tamko mapema sana la kulaani na kupinga matusi anayotukanwa Mwenyekiti mstaafu"

"Nachukua nafasi hii kuwaambiwa wananchi wa Tanzania, ninaona CHADEMA kwa sasa sio jukwaa salama na rafiki kwa kuweza kunifanya mimi kuendelea kupigania haki yao, sio jukwaa sahihi kabisa. Ninauvua Uanachama wa CHADEMA na nafasi zangu zote nilizokuwa nazo na roho inaniuma sana kuondoka lakini no way out"

Si walisema hakuna kuhama chama?🤣🤣🤣

Kumbe ni nyumbu wanahamia Kenya msimu ukifika?🤣🤣🤣
 
Kwa kua hamtashiriki Uchaguzi subirini ruzuku ikate, ndipo mtakapojua ukubwa wa Chadema au kulishana upepo tu.
Wachagga na Wameru ndio wanaofix Finance Gap la Chama kujalizia ruzuku.
Nyaturu, Gita , Sukuma na Nyakyusa ni kelele tu.
Ukiwaambia hivyo wanaskia ila hawataki kuelewa,wale wachaga na wameru utashindana nao wakati wako nchi nzima,na huwa wana tabia ya kuungana mkono wale jamaa.Na bahati mbaya kwao wana hela angalau ya kusimamia maamuzi yao.
 
Nadhani ndio maana nchi zinakuwa na mifumo ya kuchuja mambo yaliyo katika jamii. Katika kipindi hiki viongozi wa chadema wanabaini kwamba kundi kubwa la wafuasi wao ni wajinga na wasio na uwezo wa kuchanganua mambo.
Screenshot_20250509-180914.jpg
 
hivi matusi watu huwa wanatukana sa ngapi, mbona kina Ngoto na Sugu hatuwasikii wakisema wanatukanwa
 
Back
Top Bottom