Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hayo yamejiri Julai 16, 2026 mjini Salima, Malawi wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 28 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC.
Ujumbe wa Tanzania katika mkutano huo unaongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC), James Millya akiambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud.
Aidha, Mwenyekiti wa Mkutano huo ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. George Chaponda alieleza kuwa licha ya nchi za SADC kupiga hatua kubwa katika kuhamasisha mtangamano wa kikanda na utawala bora, bado majadiliano endelevu yanahitajika ili kuenzi mafanikio hayo kwa manufaa ya watu wa SADC.
Mkutano huo ulioanza na ngazi ya Makatibu Wakuu Julai 13, 2026 unajadili agenda mbalimbali zinazolenga kuhamasisha amani na usalama, demokrasia, utawala bora, maendeleo endelevu kwa kuhakikisha kuwa Kanda ya SADC inabaki tulivu wakati wote.