Inside10
Platinum Member
- May 20, 2011
- 34,776
- 42,933
Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imesema kati ya mwezi Septemba na Oktoba 2025, imekamata jumla ya kilogramu 10,763.94 za aina mbalimbali za dawa za kulevya, pamoja na kilogramu 6,007 na lita 153 za kemikali bashirifu katika operesheni zilizofanyika katika maeneo mbalimbali nchini na Jumla ya watuhumiwa 89 walikamatwa kuhusiana na uhalifu huo.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Kamishina wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Aretas Lyimo amesema, Katika operesheni Walizozifanya Septemba na Oktobawamefanya na eneo la Mlalakuwa, wilayani Kinondoni, jijini Dar es Salaam, watuhumiwa Bright A. Malisa (26), Humphrey G. Safari (26), Novatus A. Kileo (26) na Chriss P. Mandoza (26) walikamatwa wakitengeneza biskuti za bangi kwa ajili ya house party ya wanafunzi wa vyuo vikuu.