Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wanafamilia 5 waliokufa wakati wa kumuaga hayati Magufuli uwanja wa uhuru wanazikwa leo nyumbani kwao Kimara.

Ibada.jpg

Ibada ya kuwaombea marehemu inafanyika katika Kanisa la KKKT Kimara na inaongozwa na mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo.

Mkuu wa wilaya ya Ubungo na mbunge wa Kibamba wamehudhuria ibada ya mazishi.

Mbunge wa Kibamba mh Mtemvu amesema leo alitakiwa kuwa Chato kwenye mazishi ya hayati Magufuli lakini ameahirisha ili aweze kushiriki msiba wa wapiga kura wake.

Imeelezwa Kanisani hapo hata yule house girl " dada" ambaye naye alikuwa hajulikani alipo naye amepatikana akiwa amekufa.

Hivyo jumla ya wanafamilia waliofariki katika tukio hilo ni 6.

RIP Magufuli
 
Fidia?

Naomba ufafanuzi.
Serikali kwa ujumla wake inahusika na ule uzembe wa kuruhusu maelfu ya watu kuingia uwanja wa Taifa, tena katika kipindi hiki ambacho tumekumbwa na janga la corona!

Walitakiwa watu wachache tu kumuaga marehemu na watanzania wengine wangeambiwa wabakie majumbani mwao huku wakifuatilia hilo tukio kwenye luninga zao.
 
Huyu Mama alikua mjinga sana amesababisha watoto wafe kifo kibaya mno, na inaonekana walidondoka wote kwa pamoja na watu wakawalalia
Sio ujinga ndugu,hicho kifo sio cha kawaida kuna kitu kilikuwa kinamsukuma huyo mama aende huko tena na familia yote can u imagine?....muulize ndugu Mshana Jr sema hawez kuelezea hili anaogopa wanakijani watamvamiaa[emoji23]
 
Serikali kwa ujumla wake inahusika na ule uzembe wa kuruhusu maelfu ya watu kuingia uwanja wa Taifa, tena katika kipindi hiki ambacho tumekumbwa na janga la corona!

Walitakiwa watu wachache tu kumuaga marehemu na watanzania wengine wangeambiwa wabakie majumbani mwao huku wakifuatilia hilo tukio kwenye luninga zao.
Laiti serikali ingekuwa ya watu kwa ajili ya watu, PM alitakiwa ajiuzulu kwa hiari au kwa lazima, baada tu ya mazishi Chato.
 
Yule MTU tangu Enzi na mama yake wanatuhumiwa ' Kujua mengi'. Watu WA lake zone wanajua .Ipo hata habari kuwa makazi wanayoishi SASA waliyapata toka kufukuzwa baada ya kujulikana wanajua mengi ya kidunia.
Duh!
 
Serikali kwa ujumla wake inahusika na ule uzembe wa kuruhusu maelfu ya watu kuingia uwanja wa Taifa, tena katika kipindi hiki ambacho tumekumbwa na janga la corona!

Walitakiwa watu wachache tu kumuaga marehemu na watanzania wengine wangeambiwa wabakie majumbani mwao huku wakifuatilia hilo tukio kwenye luninga zao.

Ulitaka kuongelea hapo kwa Corona,povu jingine ni blah blah blah tu.
 
Back
Top Bottom