Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

Wanafamilia 5 waliokufa uwanja wa Uhuru kuzikwa leo. Mchungaji Mastah aongoza ibada

Msaada utolewe kadiri inavyokuwa, mathalani gharama za maziko, lakini hii wangechangia zaidi majirani. Role ya serikali kama Serkali ni ndogo.
 
Serikali ikisaidia familia moja, isaidie pia familia zingine zilizopoteza watu na watoto.
 
Tunasikitika kwa sababu ni vifo lakini ni ujinga kuwachukua watoto wadogo kiasi kile kanakwamba wanaenda matembezini na wao wakaone wasibaki nyumbani.
 
Rambirambi sawa, lakini neno kifuta jasho naamini linatumika kumaanisha ujira au malipo baada ya kazi fulani.
 
Watoto walifuata nini kwenye kuaga mwili wa marehemu. Haya mambo ya kutaka kuandika historia yanatakiwa kuwa nayo makini.
Kuweka historia ya kuagwa marehemu na watu bilioni nne duniani kote! Hakuna sababu nyingine zaidi ya hii.
 
Kifuta jasho kwa kazi gani au kitasaidia nini?
 
Nimejikuta na maswali mengi sana, hasa pale nilipowaza courage ya huyo mama kubeba watoto mpaka uwanja wa taifa, watoto wadogo ambao pengine hata hawawlewi maana ya msiba au maiti, ninewaza pia kuhusu mume ambae amewaruhusu watoto kupelekwa uwanja wa taifa kuaga mwili, watoto ambao bado ni wadogo na wangeweza kuangalia kwenye TV yukio zima

Nimewaza ile porpulation ya uwanja wa taifa, especially panapokua na shughuli za kitaifa

Tukijiukiza sana tutamkufuru Mungu ila tupate funzo kwa kila mmoja wetu, akina mama na akina baba, sio kila tukio lazima ubebane na watoto, the world is digitalized na unaweza kuangalia mitandaoni au kwenye TV , yale yanayokwepeka tuyakwepe, pia hata kama sio vifo ila tunawatesa hawa watoto na tunawaweka kwenye hatari tunapowapeleka sehemu zenye matukio ya namna hiyo tena mchanganyiko wa watu tofauti

Mungu awafariji wafiwa hasa Mume ambae amepoteza watoto na mke, lakini pia tuwaombee marehemu wapumzike kwa amani
 
Back
Top Bottom