Nimejikuta na maswali mengi sana, hasa pale nilipowaza courage ya huyo mama kubeba watoto mpaka uwanja wa taifa, watoto wadogo ambao pengine hata hawawlewi maana ya msiba au maiti, ninewaza pia kuhusu mume ambae amewaruhusu watoto kupelekwa uwanja wa taifa kuaga mwili, watoto ambao bado ni wadogo na wangeweza kuangalia kwenye TV yukio zima
Nimewaza ile porpulation ya uwanja wa taifa, especially panapokua na shughuli za kitaifa
Tukijiukiza sana tutamkufuru Mungu ila tupate funzo kwa kila mmoja wetu, akina mama na akina baba, sio kila tukio lazima ubebane na watoto, the world is digitalized na unaweza kuangalia mitandaoni au kwenye TV , yale yanayokwepeka tuyakwepe, pia hata kama sio vifo ila tunawatesa hawa watoto na tunawaweka kwenye hatari tunapowapeleka sehemu zenye matukio ya namna hiyo tena mchanganyiko wa watu tofauti
Mungu awafariji wafiwa hasa Mume ambae amepoteza watoto na mke, lakini pia tuwaombee marehemu wapumzike kwa amani