Asante kwa somo mkuuAsilimia kubwa ya tabia za watoto hujengwa na wazazi/walezi, japo kuna suala la mazingira, na asili.
Wazazi/walezi tukibadili aina ya malezi natumaini na watoto wetu watabadilika.
Mithali 22 : 6 "Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha hata atakapokua Mzee"
Pole kwa kugadhabika.
Na amsamehe kwa kweli maana huenda ikawa hajui atendalo kutokana na malezi aliyopitia kuanzia chini hivyo anajionea sawa tu.Mungu anisamehe ila yule anaonekana anaenda shule kusindikiza wenzie tu. Form four yake naona zero kabisa
Sababu moja situkanani na mtu nisiemjua humu ni hiyo.Mkiwalumu wazazi mtakosea hata ninyi mnastahili pia kwa kulaumia kwa kusababisha tabia mbaya kwa hao vijana. Unalaumu hapa vijana hawana adabu, baadae tunakukuta katka jukwa la siasa unawatukana babu zako. Na hao wanafunzi wapo humu wanajifunza nini kutoka kwetu, ndio matokeo hayo. Kuharibika kwa maadili ya vijana sote tunachangia katik jamii, wazazi, marafiki, mitandao, michezo, burudani, nk ambazo humo zi wazazi tu peke yao wanaohusika na sisi pia tupo.
Kati ya watu nawatetea kwenye daladala ni wanafunzi. Tena nikisikia konda anamwambia mpishe mkubwa nitalipa nauli ya huyo mwanafunzi ili akae tu kwenye siti. Hata mimi nikiona mtu mzima sana au mtu mwenye tatizo nampisha siti anakaa bila kuambiwa.Wadau.
Wakati nikiwa mwanafunzi wa kidato cha tatu niliwahi kuhudhuria semina ya wiki ya nenda kwa usalama.
Hakuna sheria inayotaka mwanafunzi asimame.
Hakuna sheria inayozuia idadi ya wanafunzi kuzidi.
Sheria inataka basi kua levo siti kwakua ajali ikitokea bima itakava levo siti tu.
Tiketi ni lazima kwa kila abiria kwakua mwenye tiketi ana nafasi kubwa ya kuhudumiwa na bima.
Watu wazima waTanzania mmelemazwa mno na huu utaratibu wa chini ya mwamvuli wa maadili. Utakuta kasista du kamepanda gari kanataka kapishwe na mwanafunzi.
Halafu akiingia mama mjamzito au mzee hako hako kasista du hakasimami hapo maadili tena tupa kule.
Mnapandikiza chuki mbaya sana kwa wanafunzi. Mwanafunzi anasoma Mbweni halafu anaishi Magereza, kakaa kuanzia Mwenge mtu anapanda Tabata anataka apishwe na huyu mwanafunzi.
Hayo majibu machafu ya huyo mtoto yametokana na hii tabia shit. Mwanafunzi akizuiwa kupanda gari hakuna anayeongea mnajifanya mpo kimya hamuoni leo abiria mwenzenu kagewa za uso ndiyo mmeona tatizo?
Ila sishangilii alichofanya ila pia sioni kosa.
Lazima alijisikia vibaya kujibishwa na mtu kama binti yake halafu anamwambia mwanao angekua kalingana na mimi angekua kwenye hili gari. Yule mtoto ana dharau sanaMaskini sijui huyo mama alijisikiaje. Sio kwa Dar pekee, watoto wengi wamekua na maadili mabaya.
Halafu nidhamu inaanzia nyumbani, kila mzazi ni lazima amjenge mwanae kitabia na kiimani ili ajue kuishi na jamii inayomzunguka.
Hata kama analipa nauli ndogo bado ana haki ya kukaa. Mtizamo upo kwamba mwanafunzi ni mdogo anatakiwa kumpisha mkubwa kiti. Hii sio kwenye daladala tu hata majumbani mwetu iko. Huwezi kukaa kwenye kiti wakati aliekuzidi umri amesimama. Ila kama mtoto ana kitu kinachomfanya ashindwe kusimama anajibu tu kwa adabu sio majibu ya kujiona mbabeInasikitisha sana.
Nadhani mtazamo wa kuwa mwanafunzi anasimama kwa sababu analipa nauli kamili nao unachangia kuleta tatizo hili. Wanafunzi/watoto wanachukulia kuwa wanasimama kwa sababu wanalipa nauli kidogo na sio kwamba ili kuwapisha wakubwa wakae. Siku akilipa nauli kamili hatambui kuwa bado anastahili kuwapisha waliomzidi umri!
Kuwarudisha kwenye mstari kunaanza kwako na mimi... ingawa tuna kazi ya ziada, Mungu aingilie kati.
Wanaomtetea huyo mtoto sijui wanawaza nini. Wanadhani hapa kinachoongelewa kumpisha siti mtu mzima.Ila ndugu yangu nimecheka kama mazuri ujue.
Naona watu wanamtetea huyo mtoto ila wanasahau kwamba huyo mtoto angeweza kukaa kimya ni jibu pia. Huwezi kusema eti kisa mtoto anakaa mbali na anakwenda mbali basi ndio awe na majibu machafu.
Mie naona angenyamaza ingetosha sababu sidhani kama wangeweza kumyanyua kwa lazima.
Mngemshusha tu maana kumpiga ingewapa kesi nadhani unaona majibu ya baadhi ya wadau (inasikitisha)Ingekua kijijini angekula fimbo. Sema yule anaonekana hata kwao anawasumbua. Unapata wapi ujasiri wa kumsema vibaya mama mtu mzima tena bila woga kwenye daladala ilojaa jamani.
Kama yule alikua anamuona yule mama atamwambia nini sasa. Kuna muda naogopa sana malezi ya watoto wetu zama hizi. Nikiona watoto wengine nawaza wangu itakuaje akifika hapa. Wakati mwinginr hata wazazi wanakua wameshachoka ila ndo mtoto keshakengeuka huna namnaSasa mwanafunzi kama huyo unaweza kukuta kashalala na wazee wakubwa sana.
Heshima kwa wakubwa lazima ipotee.
Usiangalie tabia yake tu.
Angalia jamii nzima inavyopitia mmomonyoko wa maadili na hilo linavyosababisha tabia hizi.
Wababa wanaowatongoza na kuwalala hawa wanafunzi wanachangia wanafunzi hawa kukosa heshima kwa wakubwa.
Na wao wanafunzi wanajiona wakubwa tayari.
Hakuomba ampishe yeye. Yule mama alikaa dirishani na yule mwanafunzi alikaa siti inayofuata. Ingekua pia kama laana fulani mtu mzima aliekaa dirishani ampishe mtu wakati kuna mwanafunzi kwake yeye kumpisha ilikua rahisi zaidi.Huyo mama naye kataka kujibiwa hovyo huwezi kumwambia mtu akupishe yeye mwenyewe anatakiwa ajue wajibu wake na tabia ya kutopisha siti wagonjwa au wazee mnayo sana wanawake unaweza kukuta mama mjamzito kasimama pembeni ya mwanamke mwenzie lakini hampishi
Umerukia hata kichwa cha habari sikuandika mwanafunzi ampishe mtu mzima kiti ila majibu ya dharau. Hata asingempisha kiti kwangu mimi ingekua poa tu kwa sababu hakuna sehemu mwanafunzi anatakiwa ampishe mtu mzima kiti. Nilichoongelea ni majibu aliyotoa yule mwanafunzi kabla hajatoka kwenye kiti.Mi sipendagi UNAFIKI, tupunguze ubinafsi na kunyoosheana vidole. Kwani, suala la mzee kupishwa kiti ni la kikatiba au kiubinadamu?
Namna nzuri ya kumkosoa na kumfundisha aliye mdogo kwako ni kwa mifano. Ninayo imani wengi wa wachangiaji hawajui kuwa nao wana wajibu wa kumpisha huyo mzee, wanalisukumia kwa mwanafunzi. Huyo mwanafunzi hana adabu, kama walivyo wengine wote waliokuwamo kwenye basi na ndio maana ukazuka mjadala as if wengine wasingeweza kumpisha.
Jamii hii ifundishane upendo na sio kuwalazimisha wengine kukidhi matarajio yao. Mleta mada anaamini mambo yangekuwa sawa kama mwanafunzi angejibu politely 'nalipa nauli ya mtu mzima' ... seriously? Kwa hiyo akilipa nauli ya mtu mzima, huyo mzee wenu anapata nafuu ya kusimama kwake? Kwa mentality hii, atapatikana kweli mkubwa wa kumsaidia mdogo endapo itatatokea mdogo kachoka sana?
Huyo mwanafunzi ni zao la hizi firka zetu mbovu.
Hahahahahaaa. Eti anamuuliza mwenzie kwani leo lini?? Aah kumbe mwisho wa mwezi ndo maana mama anataka kik kwangu kumbe ana stress za mshaharaila huyo mwanafunzi mdomo wake mchafu unaohusu "stress za kutokulipwa mshahara" umenifunza kitu!!....Kumbe hata watoto wadogo siku hizi wanaelewa kuwa kuajiriwa ni utumwa,haya ndiyo maendeleo tunayoyataka katika nchi!!....Asante mtoto kwa mdomo wako mchafu ulionifunza kitu!!