Wanafunzi kukacha kidato cha 5 & 6 na kujiunga Vyuo vya Diploma, tatizo ni nini?

Advance ni kupoteza muda sio issue ya uwezo mdogo au mkubwa, waliopitia wamejifunza watakueleza ukweli, nakumbuka namaliza 4 kuna jamaa zangu wao walipangiwa na Serikali kwenda kusoma diploma jamaa wakaenda somea masuala ya umeme, walipomaliza wakapata kazi sisi tuliomaliza Six tunahangaika na vyuo, uwezo upi unazungumzia?
 
Hujanielewa nilichokimaanisha hapo ..ni kwamba mfano mtu alisoma diploma ya Mining akitaka kwenda degree anaweza badilisha fani akaenda chukua Civil Engineering.

Kwa maana hiyo huyo aliyepita diploma hata akija maliza hiyo degree ya civil Engineering atakuwa na wigo mpana wa ajira yaani anatumia cheti chake cha diploma ya Mining na muda huo huo anatafuta kazi za civil engineering.

Unaua ndege wawili kwa wakati mmoja ...Diploma unakuwa multipurpose zaidi.
 
Mimi nikienda advance nikawa na moyo na bidii angalau ya kusoma nitafaulu vizuri tu maana hata O level nimepata point nzuri tu lakini moyo huo sina na lazima kule mambo yatakuwa mengi sana
Amua sasaivi tu

Either diploma au advance ili usije ukaanza kulialia baadae huko
 
Uwezo wa kuelewa masomo ya advance na kujibu mitihani ili afaulu mtihani wa NECTA apate sifa ya kwenda chuo kikuu.
 
Siyo jambo jipya, lipo tangu kitambo sana, hasa kwenye engineering field. Kulikuwa na Dar Tech, Mbeya Tech na Arusha Tech, vyuo hivi vilikuwa vinachukua waliomaliza form four na ambao walikuwa hawataki kwenda form 5 & 6. Kupita njia hiyo sijui kwanini unaiita/wanaiita ni tatizo
 
Diploma pia Ina uzuri tena ukimaliza Diploma unaajiriwa hata ukiwa na GPA ya 2.0, form six ukimaliza unaajiriwa wapi?
Kifupi unaanza kupata PROFESIONALISM toka level za chini..!! EMbu niambie, mtu aliyemaliza Ifunda Tech (let say umeme) halafu akaenda Technical college (let say umeme pale Mbeya Tech wakati huo) halafu mkakutane naye Faculty of engineering UDSM (umeme). Wa hivi professionally anakuwa vizuri sana
 
Na huo ndio ukweli wenyewe mkuu, Ila kuna watu wanaopinga wanaona mtu wa Advance ndio anakua nondo kuliko wa Diploma
 
Na huo ndio ukweli wenyewe mkuu, Ila kuna watu wanaopinga wanaona mtu wa Advance ndio anakua nondo kuliko wa Diploma
Nimekuwa nao wa hivyo..!! We mtu nikiwa pale FoE enzi hizo, technical drawing niliyoisoma nikiwa Form two technical school, tunasoma naye mwaka wa kwanza FoE..!!!
 
Si kweli, wapo Professors kadhaa ndani ya nchi yetu hawakupita A-level na wameweza kufanya vizuri sanaaa pengine kuzidi hata wale waliopita A-level. Mmoja namfahamu alishawahi kuwa waziri ndani ya nchi yetu na ni mtu mashuhuri tuu. Ameiheshimisha nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu Wengi huharibu malengo yao advance

Kwanza kuchaguliwa combination ambayo inafiti na career unayoipenda ni kipengele

Unaweza Ukawa unapenda program za afya huku wakakuchagua CBG/PCM/PGM/arts au biashara na hapo ndio mwisho wa ndoto zako


2. Kutoboa (kufaulu) ni kipengele
Ingawa Kwa Sasa ni ngumu kufeli advance ila kufaulu kumudu ushindani sio rahisi

MWISHO
Nikijitolea mfano mwenyewe na washikaji zangu, advance imetufanya tusome program za ajabu (university) ambazo hatujawahi kuzifikiria.


Watu wa degree ndio wanaoongoza kusoma program za hovyo ambazo hawakuwahi kuzitamani
 
Kwasasa ni muhimu zaidi kusoma diploma Kwa sababu zifuatazoo,

1:Urahisi wa Upatikanaji wa ajira.
Kuna baadhi ya course zinaingiliana kiuetandaji mfano za afya,uhandisi,kilimo na mifugo n.k.
Unakuta kazi anayofanya mwenye diploma Haina tofauti sana na mwenye degree. Sasa Serikali inaona nivema kuajiri wenye diploma kwasababu mshahara wao ni mdogo kidogo na watapatikana watumishi wengi kulingana na bajeti ya mwaka.Wenye degree mshahara mkubwa, hivyo bajeti inakuwa haikizi viwango vya bajeti Ili waajiriwe.

2:Kubadirishwa Kwa vigezo vya kujiunga na vyuo vikuu.
Zamani ilikuwa, ukiwa ata na division 4 una nafasi ya kujiunga na chuo kikuu. Lakini Sikuhizi nadhani mwisho ni division 3(D,D ya 50) ya mwanzo kabisa.

3:Kujifungia uwanja wa kutumiza malengo Yako.
Unakuta mwanafunzi anachaguliwa combination ambayo hakuwa na ndoto nayo na shule aliyopelekwa Ina michepuo asiyo na malengo nayo. Hivyo inamlazimu kusoma kitu ambacho hakuwahi kukipenda na kukifikiria.Kutokana na Hali ya uchumi wao.

Mwisho,
Advance ni kuzuri kwa wale waliochaguriwa masomo ya arts, wenye uhakika wa kufahuru Kwa daraja la kwanza hadi la pili(kwamsaada wa tution) na wale wanao weza kusoma private hasa kwa masomo ya science.
 
Hawa vijana hawajui walisemalo.Nisawa na mtu kushauri eti usiende jkt
 
"Kipengele"
 
Ushauri ni mzuri ila watoto ni wadogo sana, miaka 18 anamaliza form 6

Huo ndio umri mzuri wa kuanza kujenga profession yake. Tena angetakiwa akiwa na 18 ameshakuwa Technician wa Electronics au Laboratory afanye vitu vya maana! Siyo 18, hana analolijua zaidi ya kukariri majibu ya mitihani ya advance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…