adrenaline
JF-Expert Member
- Jun 17, 2015
- 4,727
- 8,093
Si kweli, wapo Professors kadhaa ndani ya nchi yetu hawakupita A-level na wameweza kufanya vizuri sanaaa pengine kuzidi hata wale waliopita A-level. Mmoja namfahamu alishawahi kuwa waziri ndani ya nchi yetu na ni mtu mashuhuri tuu. Ameiheshimisha nchi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Advance ukienda uwe na akili zako timamu. mzigo kama wa PCB ni zaidi ya diploma aiseeFamasiala nini?
Sasa kwenye advance umetaja PCB, unataka na sisi tukutajie Electrical Engineering? AU Mechanical Engineering? AU Civil Engineering?Advance ukienda uwe na akili zako timamu. mzigo kama wa PCB ni zaidi ya diploma aisee
Ni kweli mkuu, makali ya technical schools yameisha kabisaaaa. Kuna mtu mzima mmoja aliwahi niambia miaka ya nyerere waliokuwa wanapelekwa technical schools ni wale walifaulu vizuri sanaaaa(yaani ile cream hasa ndo wanapelekwa huko Musoma Technical, Moshi Technical n.k) lakini kaangalie hali ilivyo sasa kwenye hizi shule za technical utalia machozi. Hii nchi ni kama ina laana vile Mungu atusaidie..ukisoma historia ya baadhi ya vyuo vikuu kwenye nchi za wenzetu unaambiwa nyingine zilikuwa just a school lakini leo hii ni chuo kikuu chenye heshima yake.Wapo na yupo Professor mmoja yeye alianzia certificate kabisa, ila wahitimu wa enzi hizo walikuwa competent hasa.......siku hizi elimu imekuwa kama bora liende na hii ni kutokana na serikali kutelekeza elimu ya umma na wao kuanza kusomesha watoto wao private.
Nyerere angefanya kama wanavyofanya sasa hivi sidhani kama wangefika hapo walipo maana wengi walitokea familia zenye umaskini wa kutupa lakini Nyerere aliwasomesha bure elimu ya umma hadi wamepata hadhi hizo walizo nazo sasa.
Wengine ndo hao walikuwa wachunga mbuzi kijijini akina madelu ila sasa kwa kuwa wanasomesha watoto wao Feza schools hawaoni umuhimu wa kuifanya elimu ya umma kuwa bora ili watoto wa wanyonge kama walivyokuwa wao enzi hizo nao watimize ndoto zao kupitia elimu. Pesa ambayo ingeboresha hali ya elimu yakiwemo maslahi bora ya walimu ndo inayolambwa asali na kupimwa kwenye urefu wa kamba, na huenda ndo zinazoagiza hayo mabasi mia mbili yanayosemwa.
Hakuna ugumu wowote ni kupoteza muda tu na resources haina maana yoyote unaenda kusoma huko unaenda chuo kikuu UNAMALIZIA hakuna Ajira Mahala popoteUtafiti wa Wizara ya elimu unaonesha kwamba kumekuwa na Wimbi kubwa la Wanafunzi Kukacha Kidato Cha 5 na 6 badala yake Kujiunga Vyuo Vya Elimu vya kati ngazi ya Diploma.
Kwani Kuna nini huko Advance na huku Diploma Kuna nini wanakimbilia?
Je inaweka kuwa wanaona Elimu ya Kidato cha 5 na 6 haiwasaidii mtaani kulinganisha na Elimu ya ngazi ya Diploma?
Je, pengine ukijiunga A level unaenda Bachelor na Sokoni Bachelor haiziki kama Diploma?
Shida nini Wanafunzi mnakimbia Ugumu au?
View attachment 2568366
Uko sahihi kabsaa, tatizo linakuja kwenye kuweza kuwathibiti hao watoto, waliowengi uharibikia hapohapo, serikali ilipobadirisha umri wa kuanza shule haikubadiri masharti/kanuni za mwanachuo anapokuwa chuoni, kwahiyo wamekuwa wakiwaachia kama watu wazima kumbe ni watoto.Huo ndio umri mzuri wa kuanza kujenga profession yake. Tena angetakiwa akiwa na 18 ameshakuwa Technician wa Electronics au Laboratory afanye vitu vya maana! Siyo 18, hana analolijua zaidi ya kukariri majibu ya mitihani ya advance
Hazifui dafu kwa pcb acha uzombie wwSasa kwenye advance umetaja PCB, unataka na sisi tukutajie Electrical Engineering? AU Mechanical Engineering? AU Civil Engineering?
Hasa comb za sayansi, mweeeehA level pia sio kwa mchezo mchezo.
Hizi hoja ni za walioshindwa msuli wa PCM/PGM.Odinary diploma/ FTC inatengeneza watendaji wa vitendo wazur hasa fani za sayansi na engineering. Kwa sabb wahitimu wanakuwa competent kwa kuwa kule unaelewa fani yao kwa vitendo. Engineer aliyepitia udsm direct kutoka advance level anajua ledership na design tu ila njoo site sasa. Akutane na Fundi mchundo aliyetoka must/dit/arusha tech atakachomshinda ni design tu ila kuhusu kujua kaz sidhani atamfikia hata Robo. Nimekutana na graduate wengi waliotoka direct from chuo kikuu ni weupe mno katika utendaji wa vitendo
Ufaulu wako ukojeee??Mada muhimu kweli. Na mimi nipo katika wakati huo huo mgumu, nimemaliza form four mwaka jana na nimefaulu vizuri sana ila hapa ninawaza na kuwazua sana niende advance au chuo..??
Phy Una ngapi?Sayansi nimekosa A ya physics tu.
Ongezaaa sautiiii.Huwezi kutengeneza wahitimu mahiri wa degree bila vijana kwenda A-level......ni muhimu vipanga wapitie chekeche la A-level ili wajipime ukipanga wao. Wale wenye uelewa wa kawaida ni sahihi kabisa kwenda diploma maana ukijipendekeza A-level ni rahisi sana kutaga mayai.