Wanafunzi kupigwa vibaya kisa 1500 ya mchango, walimu wa kujitolea

Watoto walete michango mwalimu ale, twisheni ipo madarasa yote na masomo yote, baada ya muda wa kawaida warudi shuleni tena jioni kwa twisheni hadi jumamosi ipo. Shule zikifungwa twisheni itaendelea kama kawaida
 
Haya matoto yanaudhi kwa kweli, walimu msihangaike na wanafunzi wajeuri waacheni watakula jeuri yao. Mkiwapiga mtawaumiza au kuwaua kabisa, taabu yote ya nini wakati mshahara mnapata bila kuulizwa mlifundishaje? Toto kama halionyeki wacha likakufilie mbali, si halitaki kusoma?
Waziri wa elimu alishafafanua kuhusu adhabu hasa viboko. Ni mkuu wa shule tu ana jukumu hilo.
 
Haya matoto yanaudhi kwa kweli, walimu msihangaike na wanafunzi wajeuri waacheni watakula jeuri yao. Mkiwapiga mtawaumiza au kuwaua kabisa, taabu yote ya nini wakati mshahara mnapata bila kuulizwa mlifundishaje? Toto kama halionyeki wacha likakufilie mbali, si halitaki kusoma?
Huwa napata tabu kujuwa logic ya waalimu wa ki Tz, kuwachapa wanafunzi, au kutishia kuwachapa kisa tu hawajalipa pesa kwa ajili ya jambo flan. Kwanini mtoto atishiwe kuchapwa ama kuchapwa kabisa wakati mnashinda naye naye darasani/ Yahani si mtafuta pesa?.
 
Taharuki imeibuka katika Shule ya Msingi Makota, Kata ya Masaka, Wilaya ya Iringa Vijijini, baada ya wanafunzi 13 wa Darasa la Saba kudaiwa kupigwa wakati wa maandalizi ya mtihani, huku baadhi yao wakifikishwa kituo cha afya kwa matibabu.

Tukio hilo limeibua mvutano kati ya wazazi na uongozi wa shule, huku wazazi wakidai watoto wao walichapwa kwa waya baada ya kushindwa kutoa Sh1,500 iliyokuwa ikikusanywa kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa walimu wawili wa kujitolea.

Hata hivyo, uongozi wa shule na mwalimu aliyetajwa katika tuhuma hizo wamekanusha madai hayo, wakisema wanafunzi walipewa adhabu kwa fimbo baada ya kukutwa wakicheza nje wakati wa muda wa kujisomea.

Kwa mujibu wa wazazi na viongozi wa kijiji, tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wameweka kambi shuleni kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Wazazi walidai baadhi ya wanafunzi walichapwa sehemu mbalimbali za miili, ikiwemo miguu, mapaja na mgongoni, huku wengine wakipata maumivu na kushindwa kutembea vizuri.
View attachment 3661077
Aisee poleni sana
 
Kuna mzazi alikuja shuleni kulalamika inakuaje mtoto wake anapanda madarasa huku huku hajui kusoma na kuandika? Nikamjibu unalalamika vema subiri apande la nne kuna mchujo utafurahi. Akazidi kukaza kishari nikamjibu tena, sasa kama wewe mzazi una IQ ndogo mtoto wako atakuaje na iq kubuwa? karithi vinasaba vyako, ondoa jazba
 
Ifikie wakati hii taaluma itangazwe rasmi ni ya watu wenye changamoto za akili.

Haiwezekani kila mara matukio ya ukatili dhidi ya watoto yanayofanana kujirudia maana yake malimu hayajifunzi kwa wenzao wanaokumbana na mkono wa sheria.

Hii kazi inafanywa na vichaa waliopaswa kuwa Mirembe. Unachapaje mtoto kisa mchango ambao yeye hana source of income?
 
Taharuki imeibuka katika Shule ya Msingi Makota, Kata ya Masaka, Wilaya ya Iringa Vijijini, baada ya wanafunzi 13 wa Darasa la Saba kudaiwa kupigwa wakati wa maandalizi ya mtihani, huku baadhi yao wakifikishwa kituo cha afya kwa matibabu.

Tukio hilo limeibua mvutano kati ya wazazi na uongozi wa shule, huku wazazi wakidai watoto wao walichapwa kwa waya baada ya kushindwa kutoa Sh1,500 iliyokuwa ikikusanywa kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa walimu wawili wa kujitolea.

Hata hivyo, uongozi wa shule na mwalimu aliyetajwa katika tuhuma hizo wamekanusha madai hayo, wakisema wanafunzi walipewa adhabu kwa fimbo baada ya kukutwa wakicheza nje wakati wa muda wa kujisomea.

Kwa mujibu wa wazazi na viongozi wa kijiji, tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wameweka kambi shuleni kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika mwezi huu.

Wazazi walidai baadhi ya wanafunzi walichapwa sehemu mbalimbali za miili, ikiwemo miguu, mapaja na mgongoni, huku wengine wakipata maumivu na kushindwa kutembea vizuri.
View attachment 3661077
Masikini na tar 9|9|2026 Papertaifa dah
 
Huwa napata tabu kujuwa logic ya waalimu wa ki Tz, kuwachapa wanafunzi, au kutishia kuwachapa kisa tu hawajalipa pesa kwa ajili ya jambo flan. Kwanini mtoto atishiwe kuchapwa ama kuchapwa kabisa wakati mnashinda naye naye darasani/ Yahani si mtafuta pesa?.
viboko ni motisha, watachapwa tu
 
Back
Top Bottom