Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Taharuki imeibuka katika Shule ya Msingi Makota, Kata ya Masaka, Wilaya ya Iringa Vijijini, baada ya wanafunzi 13 wa Darasa la Saba kudaiwa kupigwa wakati wa maandalizi ya mtihani, huku baadhi yao wakifikishwa kituo cha afya kwa matibabu.
Tukio hilo limeibua mvutano kati ya wazazi na uongozi wa shule, huku wazazi wakidai watoto wao walichapwa kwa waya baada ya kushindwa kutoa Sh1,500 iliyokuwa ikikusanywa kila mwezi kwa ajili ya kuwalipa walimu wawili wa kujitolea.
Hata hivyo, uongozi wa shule na mwalimu aliyetajwa katika tuhuma hizo wamekanusha madai hayo, wakisema wanafunzi walipewa adhabu kwa fimbo baada ya kukutwa wakicheza nje wakati wa muda wa kujisomea.
Kwa mujibu wa wazazi na viongozi wa kijiji, tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku wakati wanafunzi hao wakiwa wameweka kambi shuleni kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa Darasa la Saba unaotarajiwa kufanyika mwezi huu.
Wazazi walidai baadhi ya wanafunzi walichapwa sehemu mbalimbali za miili, ikiwemo miguu, mapaja na mgongoni, huku wengine wakipata maumivu na kushindwa kutembea vizuri.