Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)

Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)

Wazazi nao hawajifikirii kweli!? Na mvua hizi bado unaruhusu mwanao aende shule? Siku yenyewe moja tu halafu weekend mimi nisingemruhusu angesubiria jtatu na penyewe ingetegemea na hali ya hewa
bora unyamaze tu usilaumu mzazi, kwani imewahi kutokea huko Arusha hata ukasema 'wangezuia watoto?'
 
Hii isikie tuu,
Huyo dereva kabisaa ba Bichwa lake anatoka anakimbia anaviacha vitoto? Mimi angenikuta ningemsukumia huko...

Halafu huyo Matron vipi? Hatajwi yupo kundi gani nakati wanasema alikuwepo ndani, kwamba hata ushauri hakutoa?
Mbona kesi za maji ni nyingi watu hawajifunzi?
Kwa ufupi maji ukishayaona yamefunika barabara yanapita juu, hapo haina kupima kina, ni kusimama yaishee.
 
Huu mwaka umekuwa na matukio mengi sana ya kutisha, Eee Mungu tunakuomba utuepushe na majanga
 
Mkuu kwa mvua ya usiku wa leo jamaa ana hoja...wapo watu hawatoi watoto mvua ikiwa kwa kiwango hiki wanasema labda ampeleke yeye shule kwa usafiri wake wengi tu na wengine wanatoa taarifa mvua ikiwa inanyesha nyingi apigiwe simu amfate yeye mwanae shuleni mbona kawaida hiyo mkuu au...
Uko sahihi
Shule ya msingi moja hivi Dar mvua ikiwa imeanza shuleni mkuu wa shule anaruhusi wanafunzi wa darasa la kwanza mapema sana waondoke maji yasije kujaa wakazama
Na kama mvua ikiwa kubwa kuanzia usiku watoto hawaendi ni shule ya serikali tu
Mimi mwenyewe mvua ikizidi wanangu hawatoki
 
Kama ni utelezi, hiyo uisikie kwa mwingine.
Sasa kama ni derva mzuri na hajaweka kileo chochote kichwani si unashuka tu kwenye gari kujihakikishia kama kweli mahali unataka kupita na gari Pana Usalama?
 
Sasa kama ni derva mzuri na hajaweka kileo chochote kichwani si unashuka tu kwenye gari kujihakikishia kama kweli mahali unataka kupita na gari Pana Usalama?

Si mtetei mpuuzi huyo aliyetelekeza gari na kuwaachia watoto kufa kinyama vile.

Kwamba yeye kapona, au mwalimu sijui matron wamepona; nina hasira sana naye mkuu. Watu wazima hao hawakupaswa kuokoka bila kuhakikisha watoto wote wako salama

ZIngatia magari huteleza, likiteleza unaweza shindwa kidhibiti Tena hata likaenda mdogo mdogo Hadi kusikojulikana.

Hoja yangu pia ilikuwa kabla ya taarifa zaidi ambapo taarifa ya awali ilikuwa gari kutumbukia tu.
 
Back
Top Bottom