Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)

Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)

Its sad watoto wasiokuwa na hatia wamepoteza maisha kutokana na uzembe wa dereva
 
Wale walisaidiwa na Nyalandu mwaka ule si ilikuwa miezi hii hii!!!
 
Hii lawama nawapa uongozi wa shule, nampa dereva, nawapa wazazi wa hao watoto. Na upande wa serikali mkuu wa mkoa , wa wilaya kwa sababu kitu tahadhari huwa hakizingatiwi
 
Uzembe Wa Dereva. Alionywa na madereva wa bodabida asipite eneo Hilo akatia kiburi Kuwa alipita wakati wa kwenda iweje ashindwe wakati wa kurudi? Amegharimu maisha Ya Wanafunzi watoto Wengi..

Kuna Familia ya Mama Mmoja Nesi wa Kaloleni inasadikiwa kupoteza watoto watatu huku maiti ya mtoto Mmoja ikiwa tayari imeopolewa.
 
Wazazi nao hawajifikirii kweli!? Na mvua hizi bado unaruhusu mwanao aende shule? Siku yenyewe moja tu halafu weekend mimi nisingemruhusu angesubiria jtatu na penyewe ingetegemea na hali ya hewa
Nakubaliana na wewe. Wazazi na waalim wote wanabeba sehemu ya lawama. Hata viongozi wa serikali ya wilaya nao. Mvua kama ile kwa nini wasiamuru shule zifungwe?
 
Mola ametupa akili. Dereva anaona maji lakini analazimisha kupita. Huwa siwaelewi watanzania tunapojifanya kumlilia Mungu hata wakati ambapo uzembe ulikuwa dhahiri.

Mimi na wewe popote tulipo tuna nini cha kufanya zaidi ya sala tu?

Kwamba Kwa habari zaidi ni kuwa dereva alitoka na kuwaacha watoto wale na gari, Kwa hakika haikubaliki.

Kwa hakika alipaswa kuwa mtu wa mwisho kutoka.
 
dah mbaya sana

MUNGU awake nguvu waanga wote wa tukio hili

rai yangu kwa madereva kipindi hiki cha hali mbaya ya hewa kuchukua tadhari zote wawapo barabarani
 
Nakubaliana na wewe. Wazazi na waalim wote wanabeba sehemu ya lawama. Hata viongozi wa serikali ya wilaya nao. Mvua kama ile kwa nini wasiamuru shule zifungwe?
Kweli mkuu, Sudan kusini hapo palitolewa tangazo na mamlaka za hali ya hewa kuwa patakuwa na joto kali serikali ikafunga shule wiki mbili, hapa kwetu kuna mizaha mpk yatokee maafa kama haya ndiyo utaona ndiyo hatua zinachukuliwa
 
Jinga moja tu (dereva) linaingiza familia kadhaa kwenye misiba na uchungu usiopimika.
Shetani sio rafiki yetu hata kidogo, ukiacha mlango wazi kidogo anaharibu kila kitu... Ona alivyosababisha hasara kubwa namna hii. Yamkini mzazi amelipia ada ya mtoto ya mwaka mzima, mtoto anapotea na ada yake😭
 
Mvua,hali ya hewa mbaya
Bado watu wana viherehere
Haya sasa washawaingiza watoto
Mtaroni

Ova
 
Back
Top Bottom