Wanafunzi Saba wahofiwa kupoteza Maisha baada ya School Bus kuanguka kwenye korongo (Sinoni, Arusha)

Wazazi tubadilike

Mvua imenyesha usiku kucha...unatoa mtoto asbh aende wapi???

Kuna vitu vinaweza kuepukika
Unaweza kuepuka ukuta utakaonguka usiku ukiwa umelala ukaua?
 
Pole sana kwa wazazi inauma sana magari yenyewe hayaeleweki ukaguzi hakuna polisi wanakula tu hela barabarani, ukiunganisha na hao machalii wanaoendeshs hizo gari basi unapata jibu kuwa Tanzania sio sehemu salama tena kwa kitu chochote kile.Ukiuliza sana utasikia tunamshukuru mama kwani wangekufa wengi zaidi.
 
Everthing ni GOD plan
Kila mtu atakuwa na njia yake kikubwa mwisho mwema pia kupunguza vifo visivyokuwa na lazima kama hivi “
Pia uboreshaji wa miundombinu ni muhimu kwenye barabara zetu ata kama upo kwenye pikipiki kuna barabara zingine zinakuita tu kaburini muda wote
 
Kuna taarifa nimeipata kutoka kwa jamaa yangu flani yupo Arusha ananiambia amepita mitaa ya Dampo, Sinoni anadai kuna basi mali ya Shule ya Msingi Ghati Memorial limeanguka kwenye korongo kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha pande hizo kuanzia usiku wa kuamkia leo Tarehe 12 hadi alfajiri.

Inadaiwa kulikuwa na Wanafunzi kadhaa kwenye basi hilo ila hana uhakika, mliopo Arusha tujuzeni kinachoendelea.

========== ==============

Wanafunzi Saba wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la Shule ya Msingi Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji Mitaa ya Dampo, Sinoni.

Inadaiwa chanzo ni dereva kushindwa kulidhibiti gari alipofika eneo la tukio kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia usiku hadi alfajiri ya leo Aprili 12, 2024.

Taarifa kutoka eneo la tukio imedaiwa Wanafunzi saba hawajulikani walipo, Watatu wameokolewa na mwili mmoja umepatikana, Dereva wa gari naye ameokolewa na yupo chini ya ulinzi.

JamiiForums ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema “Nipo kwenye msafara, ila hizo taarifa nimezipata, kikosi cha Uokozi nipo eneo la tukio na Wanafunzi saba hawajulikani walipo wengine wameokolewa, taarifa kamili tutaitoa baadaye.”

====== ====

WANANCHI WASHIRIKI KUTAFUTA WATOTO WALIOKUWA KWENYE ‘SCHOOL BUS’
Diwani wa Kata ya Sinoni, Michael Kivuyo amesema Wananchi wakishirikiana na Kikosi cha Uokozi wanashiriki zoezi la kutafuta Wanafunzi Saba ambao hawajulikani walipo baada ya Gari la Shule walilopanda kuanguka kwenye korongo, Asubuhi ya leo Aprili 12, 2024.

Amesema “Waliokuwa kwenye gari ni Wanafunzi 11, Dereva na Matroni. Wanafunzi Watatu, Dereva na Matroni wameokolewa, mwili mmoja umepatikana, Wananchi wameingia mtoni, wengine wamepewa usafiri kufuata uelekeo wa mto ili kuwatafuta ambao hawajapatikana.”

Aidha, inadaiwa Dereva wa ‘School Bus’ alipofika eneo la tukio alionywa na Bodaboda kutopita wakimsisitiza kuwa kasi ya maji ni kubwa, akalazimisha kupita akiwaambia alipita hapo awali, baada ya ajali na dereva kuokolewa, Bodaboda hao wakaanza kumshambulia kwa kumpiga, akaokolewa na Wasamalia wema.
pole kwa wazazi, vp bashite anasemaje
 
Unaweza kuepuka ukuta utakaonguka usiku ukiwa umelala ukaua?
Ndo mana nilisema kuna vitu vinaweza kuepukika. (Tahadhari)
Huyo dereva si alionywa na ma bodaboda kuwa usipite hapo maji ni mengi...alilazimisha ya nini??

KWa namna maji yalivyo mengi hakuna mzazi mwenye akili anaweza kutoa mtoto aende shule.
Mkuu we nyamaza tu
 
Kuna taarifa nimeipata kutoka kwa jamaa yangu flani yupo Arusha ananiambia amepita mitaa ya Dampo, Sinoni anadai kuna basi mali ya Shule ya Msingi Ghati Memorial limeanguka kwenye korongo kutokana na mvua kubwa ambayo imenyesha pande hizo kuanzia usiku wa kuamkia leo Tarehe 12 hadi alfajiri.

Inadaiwa kulikuwa na Wanafunzi kadhaa kwenye basi hilo ila hana uhakika, mliopo Arusha tujuzeni kinachoendelea.

========== ==============

Wanafunzi Saba wanahofiwa kupoteza maisha baada ya gari la Shule ya Msingi Ghati Memorial kuanguka kwenye korongo linalopitisha maji Mitaa ya Dampo, Sinoni.

Inadaiwa chanzo ni dereva kushindwa kulidhibiti gari alipofika eneo la tukio kutokana na mvua kubwa iliyonyesha kuanzia usiku hadi alfajiri ya leo Aprili 12, 2024.

Taarifa kutoka eneo la tukio imedaiwa Wanafunzi saba hawajulikani walipo, Watatu wameokolewa na mwili mmoja umepatikana, Dereva wa gari naye ameokolewa na yupo chini ya ulinzi.

JamiiForums ilipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema “Nipo kwenye msafara, ila hizo taarifa nimezipata, kikosi cha Uokozi nipo eneo la tukio na Wanafunzi saba hawajulikani walipo wengine wameokolewa, taarifa kamili tutaitoa baadaye.”

====== ====

WANANCHI WASHIRIKI KUTAFUTA WATOTO WALIOKUWA KWENYE ‘SCHOOL BUS’
Diwani wa Kata ya Sinoni, Michael Kivuyo amesema Wananchi wakishirikiana na Kikosi cha Uokozi wanashiriki zoezi la kutafuta Wanafunzi Saba ambao hawajulikani walipo baada ya Gari la Shule walilopanda kuanguka kwenye korongo, Asubuhi ya leo Aprili 12, 2024.

Amesema “Waliokuwa kwenye gari ni Wanafunzi 11, Dereva na Matroni. Wanafunzi Watatu, Dereva na Matroni wameokolewa, mwili mmoja umepatikana, Wananchi wameingia mtoni, wengine wamepewa usafiri kufuata uelekeo wa mto ili kuwatafuta ambao hawajapatikana.”

Aidha, inadaiwa Dereva wa ‘School Bus’ alipofika eneo la tukio alionywa na Bodaboda kutopita wakimsisitiza kuwa kasi ya maji ni kubwa, akalazimisha kupita akiwaambia alipita hapo awali, baada ya ajali na dereva kuokolewa, Bodaboda hao wakaanza kumshambulia kwa kumpiga, akaokolewa na Wasamalia wema.
= wasamaria
 
Daah kumbe dereva alipita mtoni kabisa harafu gari ikazima katikati ya mto akakimbia kwenda kuomba msaada daah kama watoto kijinga sana pamoja na mwalimu wa kike...
 
Everthing ni GOD plan
Kila mtu atakuwa na njia yake kikubwa mwisho mwema pia kupunguza vifo visivyokuwa na lazima kama hivi “
Pia uboreshaji wa miundombinu ni muhimu kwenye barabara zetu ata kama upo kwenye pikipiki kuna barabara zingine zinakuita tu kaburini muda wote
Kwa hiyo hii ajali ni God Plan?

Huyo God pamoja na wewe ni pumbavu kabisa..
 
Wazazi nao hawajifikirii kweli!? Na mvua hizi bado unaruhusu mwanao aende shule? Siku yenyewe moja tu halafu weekend mimi nisingemruhusu angesubiria jtatu na penyewe ingetegemea na hali ya hewa
Ulimbukeni wa wazazi ndio unaghalimu maisha ya watoto waoWatoto wangu Leo nimewazuia wasiende
 
Huyo dereva hata kama ana leseni, hana busara, anadharau, hastahili kuendesha gari ya abiria. Angesikiliza maneno ya bodaboda janga halingetokea.
 
Dereva ,wakumkanda ,hajui kwamba maji yanaweza pungua au ongezeka kutokana na mvua imenyeshaje
 
Wazazi nao hawajifikirii kweli!? Na mvua hizi bado unaruhusu mwanao aende shule? Siku yenyewe moja tu halafu weekend mimi nisingemruhusu angesubiria jtatu na penyewe ingetegemea na hali ya hewa
Punguza ujuaji
 
Daah kumbe dereva alipita mtoni kabisa harafu gari ikazima katikati ya mto akakimbia kwenda kuomba msaada daah kama watoto kijinga sana pamoja na mwalimu wa kike...
Poleni sana!
Isanga wewe pia una shida ya L na R !?
Harafu = Halafu.
 
mvua imenyesha nadhani krb nchi nzima usiku...
Mungu awasaidie wapatikane wakiwa hai...
 
Back
Top Bottom