DOKEZO Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga (Dar) wanaenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia kama mbadala wa dawati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Kutokana na uhaba wa madarasa pamoja na madawati, Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala) wamekuwa wakilazimika kwenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia.

Kuna kipindi 'member' mmoja alileta uzi hapa jukwaani kuhusu miundombinu ya Shule hiyo kuhusu uhaba wa walimu na vyumba vya madarasa, baada ya hapo tulishuhudia ujenzi wa madarasa matatu mapya licha ya kwamba hayajakamilika vyema.

Hoja ya awali - Shule ya Msingi Kitonga (Dar) ina Wanafunzi 4,000, Walimu 14, Madarasa 13

Hata hivyo licha ya kujengwa kwa madasa hayo lakini bado hali ni tete ambapo Wanafunzi wanalazimika kuja na viroba kwa ajili ya kukalia jambo ambalo sio rafiki.

Darasa moja unakuta lina Wanafunzi zaidi 600 ambao wanatumia madarasa mawili. Kwa mazingira hayo Mwanafunzi anatoboaje? Walimu wetu kwenye Shule hiyo wanawezaje kumudu hali hiyo?

Kuna wakati kulikuwepo na tetesi kwamba mamlaka zinapanga kujenga Shule nyingine kwa ajili kuwagawa Wanafunzi ili kupunguza idadi kubwa iliyopo sasa, lakini hadi sasa hatujasikia kauli rasmi kuhusu jambo hilo, hatujaliona katika uhalisia japo endapo likitekelezwa linaweza kuwa msaada zaidi.

Nitoe wito kwa mamlaka hususani TAMISEMI kufuatilia changamoto hii ili kuona namna bora ya kuitatua, ambapo itakuwa vyema ikajengwa Shule nyingine katika mwambao huo ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi ambao unapelekea uhaba wa miundombinu hali ambayo inawafanya wakae chini.

Sanjari na hilo Wanafunzi wengi wamekuwa wakipata changamoto kufika shuleni hasa kipindi cha mvua ikiwa ni kutokana na miundombinu mibovu ya barabara inayotumika kuelekea kwenye Shule hiyo.
Utoe wito kwa TAMISEMI au utoe WITO KWA WANAJESHI WAPINDUE SERIKALI YA TANZANIA??

Kama nchi zilizo chini ya utawalaz wa kijeshi wananchi wake wana unafuu wa maisha kwanini SERIKALI YA TANZANIA nayo isipinduliwe na WANAJESHI??
 
Hapo ni kuongea na wazazi vizuri Kila mzazi mtoto anaporipoti shule darasa la kwanza aje na kiti kizuri
Shule inawapa sample nzuri yenye kudumu wazazi wanatengeneza Kisha mtoto anapanda nacho hadi darasa la sita akiondoka anakiacha shule baada ya mda shule inakuwa na viti vya kutosha
Akienda sec same project hii itaondoa tatizo kabisa la madawati katika shule zenye shida hiyo
Sasa mnachukua Kodi zetu za Nini?
Kwanini mtangaze elimu bure?
Wekeni ada tutawapeleka kwenye shule nzuri tutalipa hiyo pesa.
 
Sasa mnachukua Kodi zetu za Nini?
Kwanini mtangaze elimu bure?
Wekeni ada tuawapeleka kwenye shule nzuri tutalipa hiyo pesa.
Umewahi kunipa Kodi Yako!?
Kama ushauri haufai achana nao ila jua anaeteseka hapo shule sio huyo uliempa Kodi
 
Screenshot_20250402_224431_Chrome.jpg
 
Halafu utakuta wazazi wao ni wafia chama tawala chini ya " MAMA"
 
Kutokana na uhaba wa madarasa pamoja na madawati, Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala) wamekuwa wakilazimika kwenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia.

Kuna kipindi 'member' mmoja alileta uzi hapa jukwaani kuhusu miundombinu ya Shule hiyo kuhusu uhaba wa walimu na vyumba vya madarasa, baada ya hapo tulishuhudia ujenzi wa madarasa matatu mapya licha ya kwamba hayajakamilika vyema.

Hoja ya awali - Shule ya Msingi Kitonga (Dar) ina Wanafunzi 4,000, Walimu 14, Madarasa 13

Hata hivyo licha ya kujengwa kwa madasa hayo lakini bado hali ni tete ambapo Wanafunzi wanalazimika kuja na viroba kwa ajili ya kukalia jambo ambalo sio rafiki.

Darasa moja unakuta lina Wanafunzi zaidi 600 ambao wanatumia madarasa mawili. Kwa mazingira hayo Mwanafunzi anatoboaje? Walimu wetu kwenye Shule hiyo wanawezaje kumudu hali hiyo?

Kuna wakati kulikuwepo na tetesi kwamba mamlaka zinapanga kujenga Shule nyingine kwa ajili kuwagawa Wanafunzi ili kupunguza idadi kubwa iliyopo sasa, lakini hadi sasa hatujasikia kauli rasmi kuhusu jambo hilo, hatujaliona katika uhalisia japo endapo likitekelezwa linaweza kuwa msaada zaidi.

Nitoe wito kwa mamlaka hususani TAMISEMI kufuatilia changamoto hii ili kuona namna bora ya kuitatua, ambapo itakuwa vyema ikajengwa Shule nyingine katika mwambao huo ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi ambao unapelekea uhaba wa miundombinu hali ambayo inawafanya wakae chini.

Sanjari na hilo Wanafunzi wengi wamekuwa wakipata changamoto kufika shuleni hasa kipindi cha mvua ikiwa ni kutokana na miundombinu mibovu ya barabara inayotumika kuelekea kwenye Shule hiyo.
Zile pesa ~400bn zilizotumika bila tija au zile zilizotolewa ruzuku atcl, trl, au zile za kununua ndege, G700 zingeweza kujenga au kukarabati shule zote za msingi nchini, kuongeza mishahara na kutoa mikopo kwa wanafunzi wote vyuo vikuu.
 
Hapo ni kuongea na wazazi vizuri Kila mzazi mtoto anaporipoti shule darasa la kwanza aje na kiti kizuri
Shule inawapa sample nzuri yenye kudumu wazazi wanatengeneza Kisha mtoto anapanda nacho hadi darasa la sita akiondoka anakiacha shule baada ya mda shule inakuwa na viti vya kutosha
Akienda sec same project hii itaondoa tatizo kabisa la madawati katika shule zenye shida hiyo
Elimu bure ya kisiasa ndio changamoto mkuu.

Miaka ya nyuma kijijini kwetu kulikua na huo utaratibu, mtoto anapoanza shule analipiwa/kutengenezewa dawati na mzazi.

Kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari hakukua na shida ya viti/madawati kabisa.

Hii elimu bure ya kisiasa ndio shida, kwasasa mzazi sio rahisi kukubali akiamini walimu ni wezi maana elimu ni bure yeye hatakiwi kulipa chochote.
 
Kutokana na uhaba wa madarasa pamoja na madawati, Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga iliyopo katika Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam (Ilala) wamekuwa wakilazimika kwenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia.

Kuna kipindi 'member' mmoja alileta uzi hapa jukwaani kuhusu miundombinu ya Shule hiyo kuhusu uhaba wa walimu na vyumba vya madarasa, baada ya hapo tulishuhudia ujenzi wa madarasa matatu mapya licha ya kwamba hayajakamilika vyema.

Hoja ya awali - Shule ya Msingi Kitonga (Dar) ina Wanafunzi 4,000, Walimu 14, Madarasa 13

Hata hivyo licha ya kujengwa kwa madasa hayo lakini bado hali ni tete ambapo Wanafunzi wanalazimika kuja na viroba kwa ajili ya kukalia jambo ambalo sio rafiki.

Darasa moja unakuta lina Wanafunzi zaidi 600 ambao wanatumia madarasa mawili. Kwa mazingira hayo Mwanafunzi anatoboaje? Walimu wetu kwenye Shule hiyo wanawezaje kumudu hali hiyo?

Kuna wakati kulikuwepo na tetesi kwamba mamlaka zinapanga kujenga Shule nyingine kwa ajili kuwagawa Wanafunzi ili kupunguza idadi kubwa iliyopo sasa, lakini hadi sasa hatujasikia kauli rasmi kuhusu jambo hilo, hatujaliona katika uhalisia japo endapo likitekelezwa linaweza kuwa msaada zaidi.

Nitoe wito kwa mamlaka hususani TAMISEMI kufuatilia changamoto hii ili kuona namna bora ya kuitatua, ambapo itakuwa vyema ikajengwa Shule nyingine katika mwambao huo ili kupunguza msongamano wa Wanafunzi ambao unapelekea uhaba wa miundombinu hali ambayo inawafanya wakae chini.

Sanjari na hilo Wanafunzi wengi wamekuwa wakipata changamoto kufika shuleni hasa kipindi cha mvua ikiwa ni kutokana na miundombinu mibovu ya barabara inayotumika kuelekea kwenye Shule hiyo.
Wapo viumbe wanasema wanawatoa watotoEMS wanawarudisha st.Kayumba wapitie nyuzi hizi.
 
Hizo jengo ndio sehemu ndoto za wengi huuwawa na watu kulazimishwa wafanane Mawazo na kile wanataka kuwa.
Likud endelea kuwadanganya wenzio.
 
Elimu bure ya kisiasa ndio changamoto mkuu.

Miaka ya nyuma kijijini kwetu kulikua na huo utaratibu, mtoto anapoanza shule analipiwa/kutengenezewa dawati na mzazi.

Kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari hakukua na shida ya viti/madawati kabisa.

Hii elimu bure ya kisiasa ndio shida, kwasasa mzazi sio rahisi kukubali akiamini walimu ni wezi maana elimu ni bure yeye hatakiwi kulipa chochote.

Watanzania huwa likiongelewa tatizo badala ya kuleta suluhisho tunaanza lawama
Mwanasiasa yeye na mtoto wake hawapo hapo shuleni na October tutawachagua tena kwa nderemo Cha msingi ni kutafuta Suluhu ya matatizo huku chini wenyewe sio nasi kugeuka wanasiasa
 
Ndio jamii zetu zishaaminishwa kua serikali inalipa kila kitu, ni wachache wanaokubali kuingia hizo gharama
 
Ukiwakuta sasa wanavyoimba nyimbo za kusifu...
 
Hatari sana hii,Shule ya msingi Msewe Ubungo pia wanafunzi wanakaa chini.Ila wasanii wanasombwa kwenye mikutano na kulipwa mamilioni ya fedha ya kodi za walalahoi ila mambo ya msingi kama haya hayazingatiwi.
 
Back
Top Bottom