DOKEZO Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga (Dar) wanaenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia kama mbadala wa dawati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Utoe wito kwa TAMISEMI au utoe WITO KWA WANAJESHI WAPINDUE SERIKALI YA TANZANIA??

Kama nchi zilizo chini ya utawalaz wa kijeshi wananchi wake wana unafuu wa maisha kwanini SERIKALI YA TANZANIA nayo isipinduliwe na WANAJESHI??
 
Sasa mnachukua Kodi zetu za Nini?
Kwanini mtangaze elimu bure?
Wekeni ada tutawapeleka kwenye shule nzuri tutalipa hiyo pesa.
 
Sasa mnachukua Kodi zetu za Nini?
Kwanini mtangaze elimu bure?
Wekeni ada tuawapeleka kwenye shule nzuri tutalipa hiyo pesa.
Umewahi kunipa Kodi Yako!?
Kama ushauri haufai achana nao ila jua anaeteseka hapo shule sio huyo uliempa Kodi
 
Halafu utakuta wazazi wao ni wafia chama tawala chini ya " MAMA"
 
Zile pesa ~400bn zilizotumika bila tija au zile zilizotolewa ruzuku atcl, trl, au zile za kununua ndege, G700 zingeweza kujenga au kukarabati shule zote za msingi nchini, kuongeza mishahara na kutoa mikopo kwa wanafunzi wote vyuo vikuu.
 
Elimu bure ya kisiasa ndio changamoto mkuu.

Miaka ya nyuma kijijini kwetu kulikua na huo utaratibu, mtoto anapoanza shule analipiwa/kutengenezewa dawati na mzazi.

Kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari hakukua na shida ya viti/madawati kabisa.

Hii elimu bure ya kisiasa ndio shida, kwasasa mzazi sio rahisi kukubali akiamini walimu ni wezi maana elimu ni bure yeye hatakiwi kulipa chochote.
 
Wapo viumbe wanasema wanawatoa watotoEMS wanawarudisha st.Kayumba wapitie nyuzi hizi.
 
Hizo jengo ndio sehemu ndoto za wengi huuwawa na watu kulazimishwa wafanane Mawazo na kile wanataka kuwa.
Likud endelea kuwadanganya wenzio.
 

Watanzania huwa likiongelewa tatizo badala ya kuleta suluhisho tunaanza lawama
Mwanasiasa yeye na mtoto wake hawapo hapo shuleni na October tutawachagua tena kwa nderemo Cha msingi ni kutafuta Suluhu ya matatizo huku chini wenyewe sio nasi kugeuka wanasiasa
 
Ndio jamii zetu zishaaminishwa kua serikali inalipa kila kitu, ni wachache wanaokubali kuingia hizo gharama
 
Ukiwakuta sasa wanavyoimba nyimbo za kusifu...
 
Hatari sana hii,Shule ya msingi Msewe Ubungo pia wanafunzi wanakaa chini.Ila wasanii wanasombwa kwenye mikutano na kulipwa mamilioni ya fedha ya kodi za walalahoi ila mambo ya msingi kama haya hayazingatiwi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…