DOKEZO Wanafunzi Shule ya Misingi Kitonga (Dar) wanaenda na viroba shuleni kwa ajili ya kukalia kama mbadala wa dawati

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Na hapo bado mama anaupiga mwingi. Hiyo shule ipo ilala ambako ndipo iko ikulu (nikikosea mnisahihishe). Mikoani kukoje? Hela zipo, ufisadi ndio tatizo. Kama waziri mmoja inaweza daiwa ana fedha kuzidi budget ya wizara, kama inadaiwa waziri mmoja anaweza kununua mabasi 200 ya UTONG kwa kampuni ya mke wake, kama inadaiwa kiongozi mmoja anaweza kusambaza pikipiki zaidi ya arobaini kwa kila mkoa, nk nk, ni pesa ipi itabaki kwa maendeleo?
 
Wewe ni mmojawapo ya wazazi wale wanaowaambia watoto wao wakatafute chochote kitu ili wachangie mkao wa mezani!

Serikali imeshindwa jukumu lake kama mzazi anayeshindwa jukumu lake kwa mwanaye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…