Wanafunzi wa advance Chamwino wamnunulia mwalimu wa hesabu baiskeli kwa kutambua mchango wake!

Mungu ambariki sana huyu mwalimu. Hawa walimu wanaokuwa bize na kazi ya ualimu huwa wanafaulisha sana wanafunzi lakini kimaisha wanakuwa nyuma kwa sababu muda mwingi wanautumia katika kazi ya ualimu kuliko kutafuta pesa.

Tazama huyo mwalimu alikuwa hana hata baiskeli mpaka kanunuliwa na wanafunzi.

Walimu wengine kama Mpwayungu village wanatumia muda mwingi kutafuta pesa kuliko kufundisha watoto ili wajiongezee kipato kwa sababu wanaona serikali imewatelekeza.



Sent from my Infinix X612 using JamiiForums mobile app
 
Walimu msinipopoe jamani mie ligi siwezi

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hawa madogo wameupiga mwingi
 
Bila comment ya Mpwayungu uzi ni batili
 
We utakuwa mwalimu ila kilaza una wivu na mwalimu mwenzako kwa kupendwa na wanafunzi.

Mwalimu kilaza huwachukia wanafunzi kwni hana kingine zaidi ya ukali.
 
Tunaweza kumpongeza mwalimu kwa moyo wake wa kujitolea leo lakini kwa jinsi mifumo ilivyo kwenye hii nchi ajue tu watakaoumia baadae ni watoto wake.
Atenge muda afanye mambo yake atengeneze uchumi wa familia yake.
 
Tunaweza kumpongeza mwalimu kwa moyo wake wa kujitolea leo lakini kwa jinsi mifumo ilivyo kwenye hii nchi ajue tu watakaoumia baadae ni watoto wake.
Mwalimu kama huyo usije tarajia kuona wanawe wakihangaika haiwezekani Anajitoa sana kwa watoto wa wengine na Mungu atasaidia wa kwake

Watu kama huyo mwalimu Mungu mwenyewe huwasimamia mambo yao na uzao wao

Biblia imeatamka hivyo

Zaburi 37:25 inasema​

Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula.
 
Kwani yanajitambua bc
 
Hata wangenunua kalamu mbili na kumpa kama ishara ya asante ingempa sana moyo mwalimu. Hicho kinaweza kuwa kitu kidogo lakini kina maana kubwa sana kwake.
Ni kweli kabisa Hata wangempa shilingi 500 ina maana kubwa mno kwake
 
Hongera Sana kipaho uyu jamaa nampata MUNGU amuongezee baraka tele kwa kazi yake
 
Mkeo angekuwa anahitaji huduma ya kusaidiwa kujifungua mahali ambapo ni mbali na hospitali na kuna nesi yuko kwake amejipumzisha akaja kumsaidia usingeongea PUMBA kama hizi wewe hata kama unakwenda kanisani au msikitini unapoteza muda wako.
 
Nimemkumbuka mwalimu wetu wa biology Mzumbe high school mwaka 1985 mwl Mlelwa tulimpenda kiasi ambacho alitaka kwenda kwenda kulima madarasa yote matatu siku ya jumamosi tukaenda kumsaidia kwa hiari yetu ndani ya lisaa limoja shamba lote tukawa tumemaliza nina uhakika kwa wakati ule utakuwa umestaafu sasa.
 
Mkeo angekuwa anahitaji huduma ya kusaidiwa kujifungua mahali ambapo ni mbali na hospitali na kuna nesi yuko kwake amejipumzisha akaja kumsaidia usingeongea PUMBA kama hizi wewe hata kama unakwenda kanisani au msikitini unapoteza muda wako.
Complete moron,tafuta hela fanya kazi kulingana na mwongozo tofautisha hospital na shule ndo maana mnakufa maskini

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…