Wanafunzi wa kizazi hiki wanafaulu sana. Je, ni bora kuliko nyie?

Huwezi hata kuandika kwa usahihi, wala kupangilia hoja zako na unawalaumu waliokuletea uhuru na kutengeneza miundombinu yote unayotumia?

Gen Z hamjafanya lolote mpaka sasa. Ninyi ni watoto ambao ndiyo kwanza mnaanza kujitafuta. Hivyo, kuwa mpole, jifunze na ujiendeleze kimaarifa.
 
Enzi zetu kata nzima anafaulu mtoto mmoja au Jimbo zima ukifaulu unajulikana ila sasa ni hatari ,scholarship za China,Urusi kupitia TIRDO walikuwa wanapata watu hawazidi kumi na mitihani mnafanyia KISUTU sekondari ila kuna kipindi Scholarship zikaja wakapata kama watu 300 hadi vilaza πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Wazee mimi ntaleta mrejesho mwaka kesho nta_reseat japo imepita miaka 12 toka nihitimu kidato cha sita. ntarudia mtihani PCM matoke ntayopata ndo nta comfirm nachokiamini kuwa saivi elimu yetu kila mtu ni kufaulu tu.

mwaka huo tuliosoma PCM hakuna mtu naemjua alie pata one
, physics kuna mtu mmoja tu ndo namjua aliye pata C, kuna mshikaji wangu ni engineer alikuwa na E physics.

Mwaka jana kuna mdogo wangu PCB alipata one ya nane nilikuwa namfanyia application cha kushangaza akawa hapati chuo(alikuwa anataka medicine), huyu dogo O'level alikuwa na one ya 11 form two one ya 7, lakini nilikuwa namfundisha naona kabisa kichwani mweupe yaani hana maajabu yoyote.
 
Personally nilipata Mathematics O-Level D mwaka 1978. Wanangu 2 walikuwa weak kwenye somo hilo na mimi nikawa ndiyo mwalimu wao. Mmoja alifanya NECTA mwaka 2009 alapata hesabu "A: na mwingine mwaka 2011 akapata hesabu "C".

Na wanakiri kuwa mimi ndiye mwalimu wao na hawanizidi mpaka leo.

Ushhuhuda tu, conclusion weka mwenyewe
 
Wanafaulishwa, wanakaririshwa ma past papers - sample questions, possibles n.k
Miaka hii division one kimekua kitu cha kawaida sana both 4 & 6...mpaka haina utamu tena. Kuna shida mahali - elimu haijawahi kuwa nyepesi kiasi hicho
 
Miaka hii kupata MD kazi sana labda kcmc
 
Ni kweli, alieishia darasa la saba 1960-1980 anajua kusoma vizuri na kuandika vizuri kuliko darasa la saba wa miaka hii.
 
Wanafaulu class Ila mtaani wanapoteana kuliko kipindi chote cha historia ya nchi.
Hivyo, kwa sasa hali ni kinyume na kichwa cha mada
 
1.
ELIMU SASA HIVI RAHISI , UJIO WA INTERNET NA UPATIKANAJI WA COMPUTER UMEFANYA MAMBO YAWE MEPESI. ENZI ZETU UNAWEZA KUTAFUTA TAFSIRI YA NENO NUSU SAA NZIMA SASA HIVI UKIWEKA TU GOOGLE KITU IMOOO

PILI ZAMANI ELIMU ILIKUA NI FURSA SEREKALI HAIKUA NA UWEZO WA KUHUDUMIA WANAFUNZI WENGI HIVYO PALIKUA NA JUHUDI ZA MAKUSUDI ZA KUFELISHA WANAFUNZI. UNAWEZA UKAKUTA SOMO RAHISI KAMA HISTORIA LAKINI INATUMIKA LUGHA NGUMU KUULIZA MASUALI ILIMRADI TU MFELI, NDO MAANA UKAKUTA MTU AKIPASI MAANA YAKE HUYO NI KICHWA.
 
'D' ya miaka hiyo ni 'A' ya miaka hii. Siku hizi si ajabu kukuta mtoto aliyefeli form two anafaulu form four.
 
Hakuna kizazi cha RUSHWA chenye mfumo wa elimu bora hata siku moja. Ila wasomi wenye akili wapo sema mfumo wa RUSHWA umeharibu kila kitu...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…