Sidhani kama kufeli kwa form six wa zamani na kufaulu wachache sana ni sifa njema. Kuna factors nyingi zilizopelekea wengi kufeli kipindi hicho. Mimi nitataja chache hapa:
1. Ukosefu wa materials za kutosha (Chand zenyewe ulikuwa unakuta ipo Moja darasa zima, waalimu wa tuition wachache, gharama za material kubwa, and things alike).
2. Nidhamu mbovu, wanafunzi wa zamani walikuwa wakorofi sana, wanapiga waalimu, migomo kama yote, mademu wao, kudoji kama kote kwa sababu walimu waliwaogopa wanafunzi kuepuka kipigo, n.k.
3. Kusoma wakiwa umri umeenda sana. Ukisoma umri umeenda sana mambo yanakuwa mengi mbali na kuwa unajielewa hii inapunguza concentration ya shule. Wee form six wa kipindi hicho unakuta anasoma kidevu kigumu kweli, ndevu mpaka shingoni😆. Wengine walidiriki kusoma wakiwa na familia zao nyumbani. Ukilinganisha na watoto hawa wa 2000+, form six unakuta ana miaka 18 19, kwa nini asiwaze masomo tu.
4. Shule za serikali usimamizi ulikuwa duni kipindi hicho, performance imeanza kuongezeka kwa Kasi aliposhika wizara Ndarichako chini ya Rais JPM. Strategies za wizara ya Elimu hazikuleta matokeo sahihi sana kipindi hicho. Tukisema mitihani ya Sasa ni rahisi kuliko ya zamani, sio kweli, kwa sababu mitihani mingi ya sasa Afisa mitihani anachukua maswali ya mitihani ya zamani. Tena katika syllabus ya 2020 inaeleza kwamba mitihani itungwe kwa kupima uelewa zaidi ya kukariri, ila hapo sidhani kama implementation yake inafanyika inavyostahili.
"Kwa changamoto hizo zote, mwanafunzi aliyetoboa kipindi hicho alikuwa bora kweli kweli kuliko mwanafunzi anayetoboa kipindi hiki"
Sababu zinazopelekea ufaulu wa sasa kuwa mkubwa kuliko zamani, nionavyo mimi ni:
1. Kuongezeka kwa materials za kujifunzia. Toka 2019 Wizara ilipondaa vitabu vizuri vya kiada (text books) chini ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), vimerahisha sana elimu ya Advance ukilinganisha na zamani. Hakuna tena kuhangaika na mi Chandi, BS, Tom Dancun, University physics, Ally Abdallah, Mgote, Elias Kiyombo, you mention them. Baada ya vitabu vya TIE vilivyotengenezwa mwaka 2014 kufeli, awamu hii wamefaulu ktk hilo. Mbali na vitabu kuwa vingi, walimu ni wengi sana siku hizi, tuition center kila Kona, technolojia ndio usiseme. Kwa nini vijana wasifaulu bana.
2. Nidhamu imeongezeka sana, wanaosoma siku hizi ni watoto sana, ukiwatisha kidgo tu wanatii. Mwanafunzi mtiifu shuleni ana high chance ya kufaulu kuliko mtovu wa nidhamu.
3. Shule za A' level zimeongezeka sana hivo ushindani umekuwa mkubwa. Private schools kama zote na zote zinataka wanafunzi hivyo lazima waakikishe outputs zao zinakuwa nzuri na nyingi ili kuvutia umma japo zipo baadhi zinazotumia mbinu danganyifu lakini nyingi wanakuwa really. Kwa hivyo, hii lazima iongeze % ya ufaulu compared to old school.
Maoni yangu ni hayo machache, ziko nyingine nyingi sababu, sema tu ni vile watu hawataki kuzitaja.
Anyways, By for Now!