Wanafunzi wa kizazi hiki wanafaulu sana. Je, ni bora kuliko nyie?

Wanafunzi wa kizazi hiki wanafaulu sana. Je, ni bora kuliko nyie?

Yap somehow angalia kama alisoma combination za zamani the like of PCB,PCM,EGM,ECA, siku hizi kuna KLA,KUNA PMC, na nyinginezo ila kama una mtoto kafaulu izo top combination jua ana maakili mengi na pia ENGLISH MEDIUM NA INTERNATIONAL SCHOOLS NYINGI ZIMECHANGIA UFAULU NDIO MAENDELEO YENYEWE HAYO
 
Waliokwenda kidato cha tano wengi wanajielewa na zaidi upatikanaji wa material ni rahisi. Zamani kitabu na material alikuwa nacho Mwalimu tu. Sasa hivi kuna vitabu cya kutosha mashuleni,mitandaoni n.k
 
Ukichunguza matokeo ya wanafunzi wa form six 1960-2014 walikua ni miamba kweli kweli, yaani mtu anatambulika karibu kijiji kizima kwamba kijana wa flani kafaulu, mimi binafsi nilikua nikikutana na mtu ameenda form five nilikua namuona watofauti saana, heshima nyingi mtaani, na matokeo yao miaka hiyo yalikua ni mabaya sana.

Refers matokeo ya ACSEE 2012. Hapa hata PCB mwenye three ya 15 alisoma udaktari...

View attachment 3042266View attachment 3042267View attachment 3042268View attachment 3042270View attachment 3042270
View attachment 3042271

Baada ya hapo kikaingia kizazi cha 2000, ambapo tunawaona kama wazinguaji, wasiokua na maadili lakini wananyoosha balaa, fikiria zamani shule zilikua zinajulikana, minaki, Milambo, pugu, n.k...

Lakini sasa hivi madogo wanaenda shule za hovyo, shule inaitwa kasangezi, sijui Ziba ya huko igunga lakini wanapasua balaa.
Miaka hii kusoma udaktari bila division 1 point 6 hupati udaktari...

View attachment 3042275View attachment 3042276

Swali je madogo wa siku hizi wanauelewa kuliko wa miaka ya zamani? Mtaala hujabadilika sana waliosoma biology 2005 bs, ndio wanachokisoma watoto wa sikuhizi.

Pia soma:Matokeo Kidato cha Sita 2024 yatoka. Ufaulu wapanda kwa asilimia 0.26
Walimu wana haki zaidi ya kutoa comments kwenye Uzi huu maana ndio wanaishi na wanafunzi.

Kwa kweli wanafunzi wanafaulu sana sio kwa sababu wana akili sana bali kwa sababu

1. Mitihani inavuja sana (nililokuwa form 5 nilishuhudia mabrothers form six wakisolve possibles na Kisha wakitoka kwenye mtihani wanafurahi kuwa possible ni Ile ile, kadhalika nilipokuwa nafanya NECTA ACSEE nimeshuhudia paper tulizokuwa tunasolve tunazikuta Kama zilivo kwenye mtihani.

2. Mfumo wa NECTA kwa sasa umeamua kuwabeba wanafunzi ili waonekane wanafaulu, Kuna program kama BRN, matumizi ya calculator O level, kuchagua math primary nk
_ wanafunzi huwa wanapata marks ndogo sana kwenye mitihani ya ndani, ila NECTA unashangaa hadi aliyekuwa anapata zero kapata two.

Ishu kubwa mfumo umeamua kuwabeba wanafunzi.

3. Mwanafunzi aliyemaliza miaka ya zamani, anaweza kupata three au two wakati huo huo kabla hajaenda advance akawa anafundisha tuition na anashusha nondo

ila kwa sasa mwanafunzi anapata threw form four au six ila hata ukimuambia afundishe hawezi.

Kimsingi imeongezeka quantity ila quality imepungua sana.

Haiwezekani shule za mkoa wa MTWARA karibu zote ukute hazina zero wala four

Haiwezekani shule inayochukua wanafunzi wa kawaida ije kupata one nyingi kuliko jumla ya two na three.
 
Attachments

  • Screenshot_20240713-135026.png
    Screenshot_20240713-135026.png
    248.5 KB · Views: 9
Wazee mimi ntaleta mrejesho mwaka kesho nta_reseat japo imepita miaka 12 toka nihitimu kidato cha sita. ntarudia mtihani PCM matoke ntayopata ndo nta comfirm nachokiamini kuwa saivi elimu yetu kila mtu ni kufaulu tu.

mwaka huo tuliosoma PCM hakuna mtu naemjua alie pata one
, physics kuna mtu mmoja tu ndo namjua aliye pata C, kuna mshikaji wangu ni engineer alikuwa na E physics.

Mwaka jana kuna mdogo wangu PCB alipata one ya nane nilikuwa namfanyia application cha kushangaza akawa hapati chuo(alikuwa anataka medicine), huyu dogo O'level alikuwa na one ya 11 form two one ya 7, lakini nilikuwa namfundisha naona kabisa kichwani mweupe yaani hana maajabu yoyote.
Ukipata fursa ya kuwafundisha Hawa madogo ndio utajua kuwa hizo one a two ni mipango tu
 
1.

ELIMU SASA HIVI RAHISI , UJIO WA INTERNET NA UPATIKANAJI WA COMPUTER UMEFANYA MAMBO YAWE MEPESI. ENZI ZETU UNAWEZA KUTAFUTA TAFSIRI YA NENO NUSU SAA NZIMA SASA HIVI UKIWEKA TU GOOGLE KITU IMOOO

PILI ZAMANI ELIMU ILIKUA NI FURSA SEREKALI HAIKUA NA UWEZO WA KUHUDUMIA WANAFUNZI WENGI HIVYO PALIKUA NA JUHUDI ZA MAKUSUDI ZA KUFELISHA WANAFUNZI. UNAWEZA UKAKUTA SOMO RAHISI KAMA HISTORIA LAKINI INATUMIKA LUGHA NGUMU KUULIZA MASUALI ILIMRADI TU MFELI, NDO MAANA UKAKUTA MTU AKIPASI MAANA YAKE HUYO NI KICHWA.
Wanafunzi wengi hawatumii hizo computer na internet kwa kuwa hazipo mashuleni pia simu haziruhusiwi.

Kwa sasa ufaulu ni kwa kuwa mfumo wa NECTA upo weak, wameamua kuingiza siasa
 
Mpime mtoto wako aliyefaulu vizuri kwenye vitu vya kawaida tu hapo ndio utaelewa. Shida inaweza kuwepo, mm toka napoona(ga) humu graduates wa sasa hata kuandika kiswahili vizuri hawezi huwa napata hasira sana

Au angalia EATV kipindi cha skonga. Dogo wa form three anaulizwa "kochi, viti, meza" kwa jina la pamoja kwa kiingereza vinaitwaje
Dogo anakuna kichwa, anaangalia juu anaumiza akili, alafu mwishoni anasema kwa kiingereza ni "vegetables"
😀😀😀😀😀 umeua
 
Nafikiri sababu kuu ni mfumo wa elimu kuingiliwa na siasa, sawa kwa sasa upatikanaji wa maarifa umekua rahisi kutokana na utandawazi lakini tukumbuke kwamba wanafunzi karibu wote wanategemea material na kile walichofundishwa darasani na walimu kama wanafunzi wa zamani tu.

Kuna mtoto wa ndugu yangu nilikua namsaidia katika masomo yake kila ninapopata nafasi kwaiyo uwezo wake nilikua naujua kwa kusema za ukweli uwezo wake darasani ni mdogo sana ila matokeo yalivyotoka nae amepasua balaa moja kwa moja nikajua kuna njia za panya zimetumika hapa.
 
Sidhani kama kufeli kwa form six wa zamani na kufaulu wachache sana ni sifa njema. Kuna factors nyingi zilizopelekea wengi kufeli kipindi hicho. Mimi nitataja chache hapa:

1. Ukosefu wa materials za kutosha (Chand zenyewe ulikuwa unakuta ipo Moja darasa zima, waalimu wa tuition wachache, gharama za material kubwa, and things alike).
2. Nidhamu mbovu, wanafunzi wa zamani walikuwa wakorofi sana, wanapiga waalimu, migomo kama yote, mademu wao, kudoji kama kote kwa sababu walimu waliwaogopa wanafunzi kuepuka kipigo, n.k.
3. Kusoma wakiwa umri umeenda sana. Ukisoma umri umeenda sana mambo yanakuwa mengi mbali na kuwa unajielewa hii inapunguza concentration ya shule. Wee form six wa kipindi hicho unakuta anasoma kidevu kigumu kweli, ndevu mpaka shingoni😆. Wengine walidiriki kusoma wakiwa na familia zao nyumbani. Ukilinganisha na watoto hawa wa 2000+, form six unakuta ana miaka 18 19, kwa nini asiwaze masomo tu.
4. Shule za serikali usimamizi ulikuwa duni kipindi hicho, performance imeanza kuongezeka kwa Kasi aliposhika wizara Ndarichako chini ya Rais JPM. Strategies za wizara ya Elimu hazikuleta matokeo sahihi sana kipindi hicho. Tukisema mitihani ya Sasa ni rahisi kuliko ya zamani, sio kweli, kwa sababu mitihani mingi ya sasa Afisa mitihani anachukua maswali ya mitihani ya zamani. Tena katika syllabus ya 2020 inaeleza kwamba mitihani itungwe kwa kupima uelewa zaidi ya kukariri, ila hapo sidhani kama implementation yake inafanyika inavyostahili.

"Kwa changamoto hizo zote, mwanafunzi aliyetoboa kipindi hicho alikuwa bora kweli kweli kuliko mwanafunzi anayetoboa kipindi hiki"

Sababu zinazopelekea ufaulu wa sasa kuwa mkubwa kuliko zamani, nionavyo mimi ni:

1. Kuongezeka kwa materials za kujifunzia. Toka 2019 Wizara ilipondaa vitabu vizuri vya kiada (text books) chini ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TIE), vimerahisha sana elimu ya Advance ukilinganisha na zamani. Hakuna tena kuhangaika na mi Chandi, BS, Tom Dancun, University physics, Ally Abdallah, Mgote, Elias Kiyombo, you mention them. Baada ya vitabu vya TIE vilivyotengenezwa mwaka 2014 kufeli, awamu hii wamefaulu ktk hilo. Mbali na vitabu kuwa vingi, walimu ni wengi sana siku hizi, tuition center kila Kona, technolojia ndio usiseme. Kwa nini vijana wasifaulu bana.

2. Nidhamu imeongezeka sana, wanaosoma siku hizi ni watoto sana, ukiwatisha kidgo tu wanatii. Mwanafunzi mtiifu shuleni ana high chance ya kufaulu kuliko mtovu wa nidhamu.

3. Shule za A' level zimeongezeka sana hivo ushindani umekuwa mkubwa. Private schools kama zote na zote zinataka wanafunzi hivyo lazima waakikishe outputs zao zinakuwa nzuri na nyingi ili kuvutia umma japo zipo baadhi zinazotumia mbinu danganyifu lakini nyingi wanakuwa really. Kwa hivyo, hii lazima iongeze % ya ufaulu compared to old school.

Maoni yangu ni hayo machache, ziko nyingine nyingi sababu, sema tu ni vile watu hawataki kuzitaja.

Anyways, By for Now!
 
Ukichunguza matokeo ya wanafunzi wa form six 1960-2014 walikua ni miamba kweli kweli, yaani mtu anatambulika karibu kijiji kizima kwamba kijana wa flani kafaulu, mimi binafsi nilikua nikikutana na mtu ameenda form five nilikua namuona watofauti saana, heshima nyingi mtaani, na matokeo yao miaka hiyo yalikua ni mabaya sana.

Refers matokeo ya ACSEE 2012. Hapa hata PCB mwenye three ya 15 alisoma udaktari...

View attachment 3042266View attachment 3042267View attachment 3042268View attachment 3042270View attachment 3042270
View attachment 3042271

Baada ya hapo kikaingia kizazi cha 2000, ambapo tunawaona kama wazinguaji, wasiokua na maadili lakini wananyoosha balaa, fikiria zamani shule zilikua zinajulikana, minaki, Milambo, pugu, n.k...

Lakini sasa hivi madogo wanaenda shule za hovyo, shule inaitwa kasangezi, sijui Ziba ya huko igunga lakini wanapasua balaa.
Miaka hii kusoma udaktari bila division 1 point 6 hupati udaktari...

View attachment 3042275View attachment 3042276

Swali je madogo wa siku hizi wanauelewa kuliko wa miaka ya zamani? Mtaala hujabadilika sana waliosoma biology 2005 bs, ndio wanachokisoma watoto wa sikuhizi.

Pia soma:Matokeo Kidato cha Sita 2024 yatoka. Ufaulu wapanda kwa asilimia 0.26
Matokeo ya mtihani wa taifa ni "political results" sio "educational results"
 
Elimu ya leo ni ya kisiasa zaidi ... Fikiria mtu hajui kama Tanganyika ni nchi lakini kwenye somo la CIVICS amepata A .
 
Ukichunguza matokeo ya wanafunzi wa form six 1960-2014 walikua ni miamba kweli kweli, yaani mtu anatambulika karibu kijiji kizima kwamba kijana wa flani kafaulu, mimi binafsi nilikua nikikutana na mtu ameenda form five nilikua namuona watofauti saana, heshima nyingi mtaani, na matokeo yao miaka hiyo yalikua ni mabaya sana.

Refers matokeo ya ACSEE 2012. Hapa hata PCB mwenye three ya 15 alisoma udaktari...

View attachment 3042266View attachment 3042267View attachment 3042268View attachment 3042270View attachment 3042270
View attachment 3042271

Baada ya hapo kikaingia kizazi cha 2000, ambapo tunawaona kama wazinguaji, wasiokua na maadili lakini wananyoosha balaa, fikiria zamani shule zilikua zinajulikana, minaki, Milambo, pugu, n.k...

Lakini sasa hivi madogo wanaenda shule za hovyo, shule inaitwa kasangezi, sijui Ziba ya huko igunga lakini wanapasua balaa.
Miaka hii kusoma udaktari bila division 1 point 6 hupati udaktari...

View attachment 3042275View attachment 3042276

Swali je madogo wa siku hizi wanauelewa kuliko wa miaka ya zamani? Mtaala hujabadilika sana waliosoma biology 2005 bs, ndio wanachokisoma watoto wa sikuhizi.

Pia soma:Matokeo Kidato cha Sita 2024 yatoka. Ufaulu wapanda kwa asilimia 0.26
Kuna ujinga mwingi unafanyika ili wafaulu.
 
Kizazi cha sasa hivi wanatumia CALCULATOR kwenye masomo!
Harafu wanatengenezewa format ya kujibu mitihani!
Enzi zetu tulikuwa hatuna vitu kama hivyo ilikuwa Kichwa na Four Figure! Sasa utalinganisha hapo wa sasa na enzi zetu?
 
Tukubali au tukatae vijana wa sasa wanasoma wengi wapo vizuri na wanafaulu sana! Sisi vijana wa zamani usela mavi na uhuni usio na msingi ulikuwa mwingi sana.

Sijajua lengo la mleta mada ila kufaulu kwa vijana wetu ni jambo jema na tujivunie badala ya kufananisha enzi zile na Sasa.

Hongereni vijana kwa kupasua.
 
Back
Top Bottom