Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nduweni wamshukuru Mbunge Prof. Mkenda kwa zawadi za fedha kwa waliofanya vizuri

Wanafunzi wa Shule ya Msingi Nduweni wamshukuru Mbunge Prof. Mkenda kwa zawadi za fedha kwa waliofanya vizuri

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wanafunzi wa Shule ya msingi Nduweni Kata ya Tarakea motamburu wilaya Rombo wamemshukuru Mbunge wa jimbo la Rombo Prof Adolf Mkenda ambae pia ni Waziri wa elimu sayansi na Teknojia nchini kwa zawadi za fedha kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo kwa mwaka 2024

Akizungumza kwa niaba ya Mbunge December 10,2024 Diwani wa kata ya Tarakea motamburu Feliches Atanasi Owiso wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa wanafunzi wa shule hiyo waliofanya vizuri amewapongeza wanafunzi na walimu kwa kazi kubwa wanayofanya huku wa kimshukuru Mbunge wa jimbo hilo Prof Mkenda kwa zawadi aliyotoa na kuzidi kuwapa motisha wananfunzi wanao fanya vizuri shuleni hapo

Kiasi cha Tsh Laki saba (700,000) hutolewa kila mwaka na Mbunge kama pongezi kwa wanafunzi walifanya vizuri katika shule ya Msingi Nduweni kwanzia Darasa la Kwanza mpaka darasa la Saba ambapo kwa mwaka huu 2024 walianya vizuri walikabidhiwa zawadi hizo kutoka kwa Mbunge

Aidha kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Miraji Shakidinda amemshukuru Mbunge wa Rombo na kupongeza mchango na ujali wake kwa wanafunzi wa shule ambapo takribani milioni 50 zimetolewa kwa ajili ya kuboresha shule katika maeneo mbalimali ikiwemo maboresho ya paa sambamba na kupaka rangi majengo ya shule hiyo huku matundu ya choo 16 yakiwa mbioni kukamilika matundu nane kwa wa vulana na matundu nane kwa wasichana.
 
Back
Top Bottom