Wanafunzi wa shule ya sekondari Minaki wanateswa na Polisi Kisarawe

Wanafunzi wa shule ya sekondari Minaki wanateswa na Polisi Kisarawe

Upelelezi huru ndo kutandika watoto vipigo,? Acha kushabikia ujinga we Guruguja..
Kwanza una hakika gani kwamba watu wanakula vipigo kweli? Na una hakika gani Kama wanaokula kipigo si wahusika? Wakati unasoma, kuliwahi tokea tukio la shule kuchomwa Moto? Unakumbuka/ kufahamu usumbufu walioupata wanafunzi kwa kukosa sehemu ya kulala? Tuwe wakweli, biashara ya kuchoma Moto mashule ni ushamba na ulimbukeni, dawa yake n kupitisha kisago kitakatifu( Wasiue tuu) ili iwe fundisho kwa wanafunzi wengine.

N.B Nikiwa advance niliwahi organise mgomo kisa walimu wamepita kukagua simu, baadae nilikuja kujilaum kwa yaliyonikuta. Nilistahili kisago/kipigo.
 
je walianza na hatua gani? Siamini kama polisi walianza na vipigo tu nooo nafikiri walianza na njia ya watoto kupewa karatasi kila mmoja kwa usimamizi wa walimu na polisi ili waandike wahusika and wakapotosha au hawakuandika kitu.....kama ni hivo basi polisi wapo sawa na kama sio hivyo basi polisi hawapo sawa
 
Bora na hao wanapigwa kuna wengine wanalala nje eti kisa shule inakarabatiwa na mvua hizi wanapata tabu kweli TARIME SEC SCHOOL
 
Duuh shule yangu hiyo wamekuwaje wakachoma tena kipindi chetu waalimu walizingua tukakiwasha ila tulijizuia kufanya uharibifu wa mabweni madarasa nk ila tukahamishia uharibifu kwenye nyumba za wale waalimu wakuda na maduka yao na polisi hawakufua dafu pamoja na kuwaleta FFU wa ukonga
 
Mitoto ya siku hizi. Unachoma shule ili iweje. Hiyo shule alisoma Kighoma Malima na Makamba na mkuu wa mkoa fulani. Wangeichoma hao leo wangeikuta?
 
Mitoto ya siku hizi. Unachoma shule ili iweje. Hiyo shule alisoma Kighoma Malima na Makamba na mkuu wa mkoa fulani. Wangeichoma hao leo wangeikuta?
Mmmhh japo sitetei kilichofanyika ila zipo zilizowahi kuchomwa na bado zipo mpk leo.

Jambo la muhimu ni viongozi wawe na muda wa kuzungumza na wanafunzi kujua changamoto na kuzitatua kwa wakati ili kuepusha majanga kama hayo na siyo kutumia nguvu kubwa baada ya janga kutokea
 
Ni upuuzi mtupu hapo ninauhakika kuna wengi wanaumia na hawajui chochote
 
Nimeshuhudia hapa Kisarawe wanafunzi wa vidato vya tano na sita wa shule ya Minaki wanateswa na polisi ili wataje walioshiriki kuchoma moto shule hiyo siku ya Jumanne.

Kama una mtoto wako Minaki, chukua hatua haraka. Ni siri kubwa na watoto wanapigwa na kupewa mateso mengine.

Wanasheria wasaidieni hawa watoto.
Kwa nini walitaka kuchoma shule?
 
Mateso sio njia bora ya upelelezi, kwa askari mwenye weledi hahitaji kutesa mtu kwani hao sio magaidi.
Njia ya kutesa ni mazoea ya kijinga tu.
Upelelezi kwa wanafunzi ni rahisi mno.

Hata hivyo nimesikitika kusikia shule yangu imechomwa.
Hiyo shule imepitia mengi na inanikumbusha mbali sana

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
Shule imejengwa kwa gharama halafu wajinga wachache tu wanaichoma..
Unajua samaki mmoja akioza wote wameoza.
Acha watandikwe hadi waeleze ukweli
 
Duuh shule yangu hiyo wamekuwaje wakachoma tena kipindi chetu waalimu walizingua tukakiwasha ila tulijizuia kufanya uharibifu wa mabweni madarasa nk ila tukahamishia uharibifu kwenye nyumba za wale waalimu wakuda na maduka yao na polisi hawakufua dafu pamoja na kuwaleta FFU wa ukonga
We nina uhakika tulikuwa wote kwenye mgomo ule.
Mwl. Mlaki, Bambucha wote hao nina uhakika uwajua

Gonga like tu[emoji23]
 
Umenena. Ziongezi neno. Labda nukta
Yaani wakitandikwa vizuri watasema ukweli.
Ukweli wanaujua ila hawataki kusema..ifike muda tuache kuwaonea huruma zisizostahili.
Yaani kwa upumbavu wao wachome shule halafu wasipigwe??
Wapigwe tu,hata angekuwepo mwanangu hapo naye angetandikwa tu kama asipotaka kueleza ukweli.
 
Waache polisi wafanye kazi yao. Wewe huenda huwezi hata kubaini mwizi uliyekaa nae kwenye gari. Unajua Kuna mbinu ngapi za kubaini wahalifu? Huko mahakamani utawapeleke watu bila ushahidi? Utawashitaki kwa kosa gani?
Kazi ya polisi siyo kutesa. Kazi ya polisi siyo kutesa. Kazi ya polisi siyo kutesa! Una mawazo ya kijima sana. Polisi wa siku hizi wana maelfu ya mbinu za kufanya upelelezi na kupata majibu bila kutesa. Mtu anayefikiri kama wewe moja kwa moja anawekwa kwenye kundi la watu ambao hawajastaarabika aka washenzi! Wataalam wameshafanya utafiti mwingi na wa kina wakagundua kuwa kutumia mateso kama njia ya kupeleleza kwa polisi kuna hasara nyingi kuliko faida. Duniani kote nchi zenye wastaarabu wameshaachana na mambo ya polisi kutesa washukiwa.
 
We nina uhakika tulikuwa wote kwenye mgomo ule.
Mwl. Mlaki, Bambucha wote hao nina uhakika uwajua

Gonga like tu[emoji23]
Ha ha ha mkuu nilishawasahau hadi majina umenikumbusha yule teacher mwenye duka mchaga sijui yule ndiyo alipata hasara sana

Kuna wadau walizama dukani wakatoka na pedi wakijua ni mikate ha ha ha
 
Yaani wakitandikwa vizuri watasema ukweli.
Ukweli wanaujua ila hawataki kusema..ifike muda tuache kuwaonea huruma zisizostahili.
Yaani kwa upumbavu wao wachome shule halafu wasipigwe??
Wapigwe tu,hata angekuwepo mwanangu hapo naye angetandikwa tu kama asipotaka kueleza ukweli.
Ukijua yaliyowapelekea kufanya hivyo unawezakuta hata wewe ungekuwa wao ungechoma pia usiwe mwepesi kuhukumu
 
Back
Top Bottom